Vifo vya Watoto Kanisani kwa Gwajima Bado ni Utata.

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

MKAZI wa Mbezi Juu David Oturo, amesema yupo katika maandalizi ya kuwasafirisha watoto wake wawili  waliopoteza maisha  Mei 17 mwaka huu  baada ya kupigwa shoti ya Umeme   katika Kanisa la Ufufuo na Uzima lililopo katika Viwanja vya Tanganyika Peakas Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na jana baba mzazi wa watoto hao Oturo alisema kuwa anatarajia kuwasafirisha watoto wake ambao ni Sarah David(10) na Goodluck David(04) leo au kesho kuelekea Mkoani Musoma kwa ajili ya mazishi.

Alisema kifo cha watoto wake ni cha utata kutokana na kwamba watoto walikuwa ni wengi katika eneo hilo lakini ameshangaa watoto wake wote wawili kupigwa  na shoti ya umeme na wote baada ya hapo walipelekwa katika Hospitali ya TMJ na kuhamishiwa katika Hospitali ya Mwananyamala lakini wote walipoteza maisha.

Akizungumzia suala la ushiriki wa kanisa katika msiba huo alisema kuwa Askofu Gwajima pamoja na waumini wake wanafika nyumbani kwake lakini hawajashiriki kitu chochote.

“Kwa sasa nipo katika maandalizi ya kuwasafirisha watoto wangu kwenda Musoma kwa ajili ya mazishi, ingawaje katika maandalizi yangu  Askofu Gwajima na waumini wake hawajatoa kitu chochote kwa ajili yamaandalizi ya safari hii.

Mimi ninachong’ang’ana  ni kuhakikisha kuwa wanangu ninawasafirisha kwenda kuwapumnzisha nyumbani kwetu nilipozaliwa ambako ni Musoma na si vinginevyo,” alisema  Oturo.

Kwa upande wake Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima alipotafutwa kuzungumzia swala hilo simu yake iliita bila kupokelewa na wakati mwingine ilikuwa ilikuwa haipatikani kabisa.

Pamoja na jitihada za kupiga simu kwa askofu huyo kugongwa mwamba, lakini ilisikika  miito ya nyimbo pamoja na mahubiri  mbalimbali katika simu yake.

Moja ya muito huo ulisikika ukisema  “Biblia ni njia kwa waliopotea, Biblia ni njia kwa waliokata tama, Biblia ni uponyaji kwa wagonjwa, Bibilia ni faraja kwa walio na dhiki,” yalisikika maneno hayo.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad