IMEBAINIKA Timu ya Simba Imedanganya Kumsomesha Mchezaji Ramadhani Singano

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

SIKU mbili baada ya Simba kudai imemsomesha mshambuliaji wake, Ramadhan Singano ‘Messi’, walimu wa shule aliyosoma ya Al-Farouq Islamic Seminary wameibuka na kukanusha madai hayo.
Mtandao huu umefika shuleni hapo na kukutana na mwalimu wa Singano, Abuu Rashid Laizer anayefundisha masomo ya Historia na Geografia pamoja na mlezi wake Hashimu Omary Poli.
zai1
Shule aliyosoma Singano
Mwalimu Laizer katika maelezo yake amesema: “Ramadhan Singano amelelewa hapa kuanzia darasa la pili mpaka anamaliza kidato cha nne mwaka 2010”.
“Hapa alikuwa analelewa katika idara zote, tukiwa na maana katika malezi yake kama kijana, kielimu na mambo mengine yanayomuhusu. kwanza ni mtoto yatima, hana baba wala mama”.
“Shirika la Africa Muslim Agency lilichukua jukumu kutoka kwa ndugu zake kwa lengo la kumuwezesha kupata elimu. kama mnavyojua, unapomsaidia yatima kuna mafanikio ambayo mwenyezi Mungu atakuwezesha mbele ya safari. Moja ya sera ya shirika ni kusaidia yatima, Ramadhan ni miongoni mwao”
“Kuna vitu vingine watu wanazungumza labda kutokana na maslahi yao na wanajaribu kupotosha umma, lakini kiuhalisia huyu bwana (Singano) alikuwa hapa na patroni wake yupo”.
“Alikuwa anatokaje hapa mpaka alipoonana na Simba? Wengi wanadhani alitoka Simba B, lakini Simba walimuona akicheza shuleni kupitia kwa kocha wake aliyekuwa akiitwa kibonge na aliondoka mwaka 2007 wakati sisi tunaingia. Licha ya kuondoka,  kibonge bado alikuwa na ushirikiano na kijana wetu pamoja na kaka yake Ramadhan Hamis”.
“Kuna vitu vingine inabidi tuseme ili tusionekane kumbeba mtu fulani. Mwaka 2007 nikiwa mwalimu wa michezo nikimsaidia mwalimu anayeitwa Saleh Haruna, nilikuwa nahusika kutoa vibali kwa Singano kwenda kukutana na wachezaji wenzake wa Simba B”
“Ni muda mrefu, lakini imekuja kuonekana hivi juzi kuwa Singano ni moja ya wachezaji wanaoweza kuisaidia Simba.  Kuanzia 2009 mpaka 2011 timu kubwa iliona anaweza kufaa, lakini yeye ni yatima na wakati anasoma kila kitu kuanzia kula, kulala mpaka madaftari viligharamiwa na shirika”
“Vitu vyote walikuwa wanapewa na shirika pindi wakifungua shule. Hakuna mtu aliyekuwa akimlipia ada, mimi sijaona, labda kama mtu anazo risiti alizokuwa anamlipia alete tuzione na kuthibitisha”.
“ Utaratibu wetu wa ada ya watoto yatima huwa inakatwa moja kwa moja Damam, Quwait, ambako ni makao makuu ya Idara ya elimu ya ‘Africa Muslim Agency’ duniani, lakini kwa Tanzania kuna tawi  lake hapa Dar es salaam na Sheikh Kassim Mzee ndiye aliwatafuta akina Singano na wenzake”.
zai22
Baada ya kuzungumza na mwalimu, tukapata fursa ya kuonana na mlezi wa watoto yatima shuleni hapo, Hashimu Omary Poli ambaye amefanya kazi toka mwaka 1997 mpaka leo.
Katika malezo yake Poli amefafanuwa kuwa:
“Ramadhan Singano nilimpokea toka mwaka 2001 akiwa darasa la nne. Amesoma hapa mpaka alipomaliza kidato cha nne chini ya udhamini wa shirika la Africa Muslim Agency”.
“Kijana huyu toka alipokuwa mdogo kipaji chake kilidhihirika kwenye suala la michezo, alionesha uwezo mkubwa na kwa bahati nzuri kulikuwa na mwalimu Kibonge aliyekuwa karibu nao sana.  Mwalimu huyu alipewa fursa kubwa sana ya kuwa nao na kukuza vipaji vyao”.
“Nashukuru Mwenyezi Mungu mpaka anafika ‘fomu foo’ alikuwa kijana anayependa sana mpira na akapata bahati ya kujiunga na Simba. Tukawa tunamsikia Ramadhani Yahya Singano ni mchezaji na alikuwa anakuja kuwasalimia wenzake na wakati mwingine anawaletea misaada”.
“Tunashukuru kwamba anakumbuka fadhila za Maustadh wake, anakumbuka jinsi alivyolelewa, aliishi na wenzake vizuri,  tunamuombea kila la kheri”.
“Ninachokifahamu mimi kama mlezi nilimpokea akiwa mdogo. Suala zima la kimalezi, udhamini wa kusomeshwa shule ilikuwa chini ya Shirika la Africa Muslim Agency. Wao ndio waliomdhamini na walimpokea akiwa mdogo kama wanavyowapokea watoto wengine yatima”. Amesema Poli.
zai5zai4
Baadhi ya nyaraka za Singano katika shule aliyosoma
Mwanzoni mwa wiki hii Msemaji wa Simba, Hajji Sunday Manara alisema klabu hiyo imegharamia masomo ya Singano na wanashangaa kijana wao kukosa fadhila.
Manara alisema:  “Hivi mnajua Messi tumemtoa wapi Simba? Unajua Ramadhan Singano amesomeshwa na klabu ya Simba? Mnafahamu hilo? Kasomeshwa  IT na klabu ya Simba,  Mnajua fadhila ambayo klabu ya Simba imemfanyia?”
“Hao wanaosema wazazi wake walikuwa wapi wakati klabu ya Simba inamsomesha? Nauliza, walikuwa wapi? Klabu ya Simba imegharimia haya. Ninyi waandishi ndio mnaandika vilabu havithamini wachezaji chipukizi. Sisi ndio klabu pekee yenye wachezaji zaidi ya asilimia 75 tuliowatoa kwenye mpango wetu wa soka la vijana. Hawa tunawakuza na bado tunawapa ofa ya usajili”
Singano ameingia kwenye mgogoro na klabu yake akidai imeghushi mkataba wake.
Simba ina mkataba wa miaka mitatu uliosainiwa mei 1, 2013 na unatakiwa kumalizika julai 1, 2016, wakati Singano ana nakala ya mkataba wa miaka miwili aliosaini mei 1, 2013 na unamalizika julai 1, 2015.
Nakala ya mkataba wa miaka mitatu waliyonayo Simba pia ipo TFF, lakini Singano anadai hakusaini mkataba huo na anautambua wa miaka miwili.
Licha ya suala hilo la mkataba, bado Singano hajatimiziwa baadhi ya stahiki zake katika mkataba wake miaka miwili ikiwemo suala la kodi ya nyumba.
Muonekano wa shule aliyosoma Messi

Tanzania Hottest Celebrity Gossip New
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. manara ameudhihirishia umma jinsi timu ya simba ilivyo na ubabaishaji

    ReplyDelete

Top Post Ad