Wema Sepetu, Sabuni Utakayoogea ndio Utakayonukia

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kwako Wema I. Sepetu ninakuandikia maneno haya, uyashike, uyakumbuke siku zote za maisha yako na kuyasimamia ili uweze kufika katika kilele cha mafanikio ambacho weengi hutamani kufika lakini wanaishia kupiga mbizi kwenye Kokoto.

Dunia nzima kwa sasa kumekuwa na mlolongo mkuubwa sana wa wasanii na hata watu wanaoishi kiujanja ujanja ili kufanikisha malengo yao kimaisha.

Kumekuwa na mlolongo mkuubwa sana wa vijana ambao wanaingia kwenye tasnia ya sanaa pasipo kuwa na Elimu wala weredi wa Sanaa hio, lakini goal lao kuu lipo katika kuusaka umaarufu na kuwa na majina makubwa.

Ukichungulia kwenye boti ya wasanii wa filamu utakutana na lundo la vijana kwa wazee ambao wamechumpa huko ili wapate shavu na siku moja wawe miongoni mwa nyota katika medani hio.

Ukija kwenye sanaa ya uimbaji, utakutana na lundo la Vijana kwa wazee, na wote hawa wanatamani siku 1 magazeti yapambwe na habari zao.

Kundi kuubwa la vijana wa kike kwa kiume wamekunja madaftari na kuachana nayo pia kuipa elimu Kisogo na kujikita katika sanaa. Imefika hatua kijana anatiririka mistari ya wimbo katika mtihani wake wa mwisho wa kidato cha 4... Hii yote ni katika kuusaka umaarufu ambao ndio lengo kuubwa kwa mlio wengi wenu.

Mifano ipo mingi. Ila kwa leo nataka nikupe shubiri na ujikaze umeze tu maana ndio itakayokuponya.
na kama ukikaidi basi ukae ukijuwa ipo siku utakwenda ogelea baharini na kopo.

Rekodi zinaonesha Wema ulipata kuwa Miss Tanzania mnamo mwaka 2006 na kufanikiwa kukwea pipa mpaka Warsaw Poland kwenda kuliwakilisha Taifa la Tanzania katika kinyang'anyiro cha Miss World.

Ushindi wako haukuwa msafi kama Sanda kwani kuna utata ulijitokeza kati yako na mwanadada Jokate ambae kuna kundi la watu mpaka sasa hawataki kuamini kuwa ulimgaragaza kihalali Mrembo huyo.

Nikitafakari zaidi naona kuwa Wema si Miss Tanzania wa kwanza au wa mwisho ktk Taifa hili. Ni dhahiri shahiri kuwa kuna Mamiss walitangulia kabla yako na kuna wengine walifuata baada yako lakini wanaishi maisha ya heshima na taadhima. Wanaitumikia jamii na kufanya kazi zao halali na zenye kuwapatia mapato halali.

Mifano miwili tu kwanza nianze na Mama ya Mama HOYCE TEMU na pia nimtaje ANGELA DAMAS ambao wamesimama imara na kufanya mambo makubwa katika jamii na pia wamekuwa wakikusanya na kujiingizia mapato halal.

wanasema starehe ya Mbwa ni kuukalia mkia wake lakini Wema wewe tangu ulipokuwa Miss mwaka 2006 mpaka hivi sasa umekuwa ni mtu wa kuusaka umaarufu kupitia kila njia ambayo unaona itasaidia kukubakiza midomoni mwa watu. Umekuwa ni mtu wa kucheza na vyombo vya habari ili uweze kulibakiza jina lako on top...

Kwa hili umefanikiwa mno, umefanikiwa jina lako kudumu katika midomo ya watu, umefanikiwa jina lako kudumu kwenye baadhi ya vipindi vya Redio na Runinga, na kama hio haitoshi Mama nakupongeza kwa kufanikiwa kulidumisha jina lako kwenye vichwa vya habari vya Magazeti, japo kwa akili ya kikubwa ni wazi kuwa hapa unamaliza kuni kwa kuchemsha mawe.

Lakini je watu uliowalenga walijadili jina lako wana tija yoyote ama wana faida yoyote wanakupatia?
Au hivyo vipindi vya redio na runinga vinavyotumia jina lako kusukuma siku je vinawalenga watu wenye tija katika jamii ambao wanaweza wakakuunganisha na taasisi fulani au NGO ili uweze kuanza kufanya makusanyo halali ya pesa?

Hebu tafakari kwa mapana je hayo magazeti ya marangi rangi ambayo kila Alfajiri yanaibuka na habari kukuhusu wewe je yanasomwa na watu makini au je yamewekwa kwenye kundi gani katika jamii?

Sitaki kuchuma dhambi kwa kujiaminisha kuwa eti wewe ni msichana mreembo sana so utabakia on top for the rest of your life.

Macho yangu yalipata kumuona Aminata Juma mwishoni mwa miaka ya 90 akisoma Sekondari ya Jangwani na kisha Zanaki.

Aminata alikuwa Mashalaah alieumbika katika kila Idara na akili ya Darasani pia, aliposimama Aminata basi Kajala hakuthubutu kusogea na mara zote aliishia kulekule jeshini Jitegemee.

Alipofungua kinywa chake Aminata na kuongea Lugha yoyote ile iwe Lugha mama ya Taifa ama iwe Lugha ile ya kigeni basi Amina Chifupa hakuthubutu hata kupiga chafya...

Sitaki na sintoruhusu kuaminishwa kuwa wewe Wema ni mzuri zaidi ya aliepata kuwa Msomi wa Chuo Kikuu kitivo cha Sheria Sylvia Bahame ambae alipata pia kuwa Miss Tanzania mwaka 2003, huko ni sawa na kumfunika Nyuki kwa tenga.

Sifa unazozisaka sasa na umaarufu unaoufurahia sio kitu cha msingi kwa mtu makini. Kumbuka umesha jidharirisha saana ili mradi tu jina lako libaki midomoni mwa watu. Familia yako imeshajadiliwa saana na wewe umelifurahia hilo ili mradi tu ubaki on top.

Wenzio wakaenda mbaali zaidi na kumdhalilisha mpaka Mama yako kwa kubandika picha kwenye mitandao akiwa mtupu.

Najuwa huu ni mfumo mlionao wasanii wa leo kwa kupenda kutokelezea kwenye headlines katika Media tofauti ati mkiamini kuwa ndio mnauza na mtadumu milele...lakini mwamuzi wa kweli anaeweza kukudumisha juu milele ni bidii katika kazi yako halal.

Wema wewe tangu umejikita kwenye tasnia ya maigizo huna movie hata 1 ambayo unaweza kuitaja kuwa ni bora na ipo kwenye viwango vya ubora kwa baadhi tu ya sinema za hapa Afrika ya Mashariki.

Wema wewe huwezi kujifananisha na wasanii wa Luninga kutoka hapo Kenya, lets say wasanii walioshiriki katika tamthiria ya Sumu la Penzi.

Kama hio haitoshi Wema wewe huna kipaji cha kuigiza kumzidi msanii yeyote wa kike katika tamthiria ya Siri ya Mtungi.
Hivyo ni wazi kuwa huna

Tofauti na mkia wa Mbuzi...haustiri uchi na wala haufukuzi Nzi.

Jipange sasa;

Hakuna binadamu vigeugeu katika hii Dunia kama wabongo. Na kuna harufu ya wabongo kukuchoka Mama kwa skendo zako za kujitengenezea ili ubaki ukijadiliwa bila faida.

Alikuwepo MR NICE;
Nadhani unakumbuka ni jinsi gani alishika na kubamba jamii.
Lakini leo hii anakesha Corner Bar akiomba (200) mia mbili ili acheze pool table.

Alikuwepo SINTA;
Eskimo huyu alitamba katika maigizo ya Runinga, lakini zake zilipopita zilikwenda na hazikurudi na hazitorudi ng'o.

Pakawepo na JUMA KASIMU maarufu kama JUMA NATURE;
Yaani aliishika Bongo kiasi kwamba chochote alichokiimba kilibamba.

INSPEKTA HAROUN na RAY C;
Hakika walitamba mno, lakini leo hii wabongo wamewachoka na kuwaona kama kopo la chooni. Kwa kifupi wamepotea kama harufu ya ushuzzi.

Sasa Mama jitathmini upya, maana painukapo leo basi patainama Kesho, je kwa miaka takriban 10 ambapo umedumu midomoni mwa watu kwa series yenye episode nyiingi za kujitengenezea wewe mwenyewe je umepata faida ipi? Au ndio yaleyale ukipenda vitamu basi utahalalisha vya haramu.

Alinena Gang Chomba "If you don't change your self, changes will change you".

THINK BIG!

Shifta/JF
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. yaani toka 2006 yuko famous anafanya kazi lakini mpaka leo hata nyumba hana daah only in tanzania someone can be that famous lakini anakaa nyumba ya kupanga angekuwa anatumia u famous wake vizuri angekuwa mbali sana ki maisha

    ReplyDelete
  2. Dah, hatari! Jamaa nimemsoma na nimemuelewa,kweli huyu mwandishi bora, maana anaandika ki2 na kukutolea mifano ilio wazi kbs, kweli sabuni utakayo ogea ndio utakayonukia nayo!!

    ReplyDelete
  3. KAHABA WA TAIFA AWE MBUNGE HICHO CHA UKAHABA NA KUGOMBEA MABWANA NANI BADALA YAKE ?

    ReplyDelete
  4. tunasubiri kuona hali itakuwaje maana wabongo hawanaga vizuri siku zote wanajua vibaya tu

    ReplyDelete

Top Post Ad