CHADEMA wamsahau Dk.wilbroad Slaa..Kisa LOWASSA

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Hili limejitokeza mara baada ya Lowassa kutangaza kuingia UKAWA kupitia CDM, Kufuatia jambo hili upepo wa Dk.Slaa kupendwa na kuaminiwa na wana CHADEMA unaelekea ukingoni kufuatia ingizo jipya, na huenda asisikike tena katika mbio za uchaguzi mkuu akiwa mgombea wa urais wa chama hicho kufuatia wengi kumsahau kuanzia viongozi na wanachama wa chama hicho na sasa ni historia tu!

Dk. Slaa Kwa takribani miaka 10 ya uongozi wake amekuwa muhimili wa CHADEMA na amekua kipenzi cha Wafuasi wa chama hicho hasa vijana kwa ahadi zake na utumishi wake!
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ndio ujue hawana msimamo,kwani mara umeshasahau ya Zito Kabwe?

    ReplyDelete
  2. Nimefuatilia picha za ukaribisho wa Lowasa akikumbatiwa na viongozi wa Ukawa lakini nikashangaa kutomwona Dk Slaa kufanya hivyo. Pia hadi sasa sijapata kusikia tamko lake.
    Kama Mtanzania nijifunze nini katika hili?. Mimi sina tatizo na mtu ambaye anapenda kuleta maendeleo na maisha bora kwa Watanzania kutoka chama chochote. Ila tatizo langu ni ule uongo wa wanasiasa ambao kwa malumbano yao wanadiriki hata kusema kwa miaka hamsini nchi yetu haijabadilika. Nilizaliwa mwaka 1948 na kusoma wakati wa mkoloni na baadaye tukapata Uhuru wetu ........nakumbuka tuklikotoka na hapa tulipo sasa mtu hawezi kunidanganya kwani nimeyashuhudia mabadiliko makubwa. Inavyoonekana sasa Dk. Slaa atapigwa chini kuhusu nafasi ya kugombe Urais (eti kwa sababu Lowasa atafuatwa na wana CCM kujiunga na UKAWA) ambao hata yeye alikuwa na shauku nao wakati akitwanga maneno ya ufisadi wa Lowasa. Sasa Lowasa ndani ya CDM? Hapa nawaachia wenyewe.

    ReplyDelete
  3. Na ndivyo ilivyo hadi sasa watu wanamjali na kumuheshimu sana tu, usijaribu kujifanya unafeel pit on him, hutamuweza huyo ni Kasisi, he listening more from God than human being... kula ndimu tu zinakuhusu mpendwa.

    ReplyDelete
  4. Na hasa ile hotuba yake aloitoa akimponda 'Edo' kwamba ni mwizi, fisadi, na ushahidi wote anao, anasubiri aingie madarakani ampeleke mahakamani ili aishie jela, ndio itazidi kumuumiza akifikiria atamnadi au kukanusha vipi yale alosema, na clip za hiyo hotuba zipo!! Na kwa sasa EDO ndio malaika ktk chama chake!! PATAMU HAPO ( in Soudy Brown's voice)

    ReplyDelete
  5. Hehehe tuangalieni Movie Mungu anajua kuwaumbua wanafiki ...natakakuiona movie ya october tuu basi

    ReplyDelete
  6. Cha msingi nimesoma hapa kwetu hakuna mwanasiasa mkweli na kamwe tusishikilie tunayoambiwa na viongozi wetu tutumie macho yetu kupembua chuya na mchele...

    WANANCHI WAMEKUA BENDERA ..UPEPO UNAPOPEPEA NDIKO WANAKOELEKEA.NILIMPENDA SANA LOWASSA ILA NIMEPATA SANA MASHAKA CHADEMA KUMCHUKUA HUKU HAWAJASAFISHA YALE WALIYOMTUHUMU...HAKUNA WA KULAMBA NDIMU KWA SASA ILA TUTAONA ATAKAE LAMBA NDIMU HAPO OCTOBER..HASA NYIE WENYE USHABIKI MAANDAZI USIONA FIKRA....

    ReplyDelete
  7. kuna msemo aliusema "NIKIKOSA KWA MLANGONI NITAPITA KWA DIRISHANI "ilinichukua muda sana kumuelewa,ingawa wenzangu na mie walifurahia kwa staili yao ya heeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee lakini mie nilibaki najiuliza kivipi dirishani?alipokosa nikazidi kuwaza mbona dirishani hapiti? sasa nimepata majibu dirishani ndio alipo.....je anahisi dirisha ni kubwa kumuwezesha kuingia ndani?vipi kama dirisha ni refu akaruka na kuvunjika mguuuu? simuombei hayo ila NIMEJIFUNZA KUA MAKINI NA MATENDO NA MANENO YA VIONGOZI KUEPUKA KUA BENDERA .

    ReplyDelete

Top Post Ad