Lowassa na Majibu ya Hasira kwa Swali la Msingi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Wadau Habari; jana ilikuwa siku ya kipekee sana kwa historia ya Tanzania ambayo tuliahidiwa na tuliisikia minong'ono mingi na tetesi za kila leo juu ya kuhama chama kwa aliyekuwa mgombea urais kwa tiket ya CCM ndugu, EL.

Binafsi nampongeza kwa kuitumia haki yake ya kidemocrasia na kufanya maamuzi magumu; kama mtanzania nisiyefungamana na upande wowote nimestaajabishwa sana na mambo mawili makubwa.

Mosi ni juu ya umiliki wake wa card ya CCM, EL inasemekana ana miliki card namba 15 ya Uwanachama ndani ya CCM, lakini siku ya jana alijivua uwanachama na kupewa rasmi card ya CDM, sasa bado najiuliza imekuaje kamanda huyu amejiondoa CCM na kwenda CDM lkn bado anamiliki card ya chama hicho? Maana jana sikuona akiirudisha card ya CCM ili ichanwe chanwe pale mbele ya macho yetu.

Lakini kama hiyo haitoshi bado najiuliza inawezekanaje Kiongozi mkubwa kama yeye anathubutu kutoa majibu ya hasira mbele ya Taifa hili juu ya swali la msingi ambalo lilimchafua yeye na baadhi ya Viongozi wa wizara husika.

Kwa kusema kwamba NANUKUU; "Nilipoitisha kikao cha "Government negotiation team" nikawauliza mbona nasikia huu mkataba una matatizo?

mimi nina uzoefu wa kuvunja mikataba na huu tuuvunje! wakaomba ruhusa watoke nje kwa saa moja, baada ya hapo waliporudi wakasema wamepigiwa simu toka mamlaka ya juu mkataba usivunjwe "what else could I have done?"

Mwisho wa KUNUKUU, Sasa najiuliza hapa inawezekanaje PM umeitisha kikao cha subordinates wako alafu anatokea wa kukuambia kuwa et nimewasiliana na wakuu wamekataa hilo, nani basi mwenye kupaswa kufanya consultation na Wakuu wenzake kati ya watu hawa wawili EL kama PM au Subordinates?

Lakini pia napata shaka pale namna ambavyo swali la msingi lilivyojibiwa kwa kusema kwamba, NANUKUU; "Am sick of Richmond, mtu yoyote mwenye ushahidi wa mimi kuhusika na Richmond aende mahakamani, kama huna just shut up. Nilichukua uamuzi kwa niaba ya serikali.

Nimeondoka madarakani miaka nane iliopita, mambo haya yameongezeka yamepungua, mikono yangu ni misafi na mtu mwenye ushahidi acha kupigapiga kelele, peleka mahakamani" mwisho wa KUNUKUU; Kwa uelewa wangu wa kawaida kabisa unyeti wa jambo hili haukutaka jibu la namna hii bali watanzania tungeridhishwa zaidi endapo tungepata majibu mazuri kwa kina na yenye kujitosheleza badala ya kuwa mkali kiasi ambacho inatuacha na maswali mengi kwamba ile ni namna ya kututisha na kutuziba midomo kama ambavyo ilitokea pale kwa wana habari wenzangu au ni nini hasa?

Kama hii haitoshi bado najiuliza, Je na ile hoja ya Dr.Slaa kwamba ushahidi wa jambo hili anao na yupo tayari kwenda kuthibitisha mahakamani leo hii sisi watanzania tunaibebaje hii statement kuwa naye alikuwa anabwabwaja tu au namna gani?

Lakini nathubutu kwenda mbali zaidi kwa kujiuliza Dr.Slaa na wenzake wanasimama vipi Jukwaani kumnadi kwa kumtakasa mtu huyu ambaye wao walikuwa wanachangia kumchafua?

Mambo haya yananipa shida kuyapatia majibu basi nabaki kujiuliza bila mafanikio naombeni wadau mnisaidie kung'amua.
"Majibu ya hasira kwa swali la Msingi"
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

11 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. weeee ne umekuja na yako madogo ya kawaida yasiyokuwa na msingi wakati umeacha makubwa hukuyaona!!!!

    unatafuta kuonekena na wewe umechambua kauli za LOWASA lakini KICHWA CHA HABARI NA YALIYOPO NDANI HUNA LOLOTE

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kweli watadanyika tutakuwa wajinga mpaka lini kwa siasa za kipuuzi eti mtu kukatwa jina akatafute safari ya matumaini kwingine na anapenda matajiri kwa sababu ya kuuchukia umasikini tutabaki masikini kwa kudanganyika na siasa za kifisida

      Delete
  2. Mwanishi elimu yako ulivuka chekechea kweli?

    ReplyDelete
  3. Yaani ni kuchagua CCM,na kuchagua Magufuli basiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii.

    ReplyDelete
  4. huyo ni CCM Alafu katumwa basi loooh,mwandishi na uchambuzi feki. ufisadi umeendelea ndani ya CCM hata baada ya LOWASA kujiuzulu why so. majibu yake yana busara sana kwani inaonyesha wazi kuna nguvu ya juu inayo support ufisadi huyo mwandishi ana akili mgando.mbulllaaaah

    ReplyDelete
  5. Wewe unamawazo mgando. Upo negative. Ukome na ushindwe tunataka mageuzi kila kitu kwa serikali iliyopo ni matatizo. Serikali haina hela kila kitu kimesimama. Tunataka mageuzi.

    ReplyDelete
  6. majibu gani ya hasira??? ambacho haujaelewa nn kazi kumchafua lowassa wa watu. kama ww n team ccm kaa kimya movement for changes ndo habari kwa xxa

    ReplyDelete
  7. Hili swala halikuanza leo wala jana kuhusu richmond ni kweli his sick and tired go to court if you want to sue him, ok, if not shut up. Kuhusu kadi kaichukue uichane wewe, na Dr. Slaha na Mnyika achana nao hawakuhusu!
    Mwisho, kama amri ilitoka juu wewe ulitaka yeye afanyeje juu ya hilo!? Maana kuna wakati hata waziri mkuu wa sasa mtoto wa mkulima, alishindwa kutoa majibu bungeni akaishia kusema kama ningekua rais ningetolea uamuzi jambo hili ila sasa tumsubiri rais arudi kutoka safarini ataamua jambo hili! na hapo wewe unasemaje? Kwa hiyo ina maanisha maamuzi yake yalikomea pale basi. "Take a chill pill and drink, so will make you come down mr".

    ReplyDelete
  8. pumbavu tu,sema wewe ni CCM yaishe

    ReplyDelete
  9. Tatizo watu wapuuzi sana sisi Watanzania, muandishi ameongea vitu vya msingi sana, alafu tunaleta propaganda hapa. CDM tumevuna wengi kwa issue ya ufisadi, na ufisadi ulizungumzwa sana kupitia EL kuliko yyte Tanzania, kwa kumsafisha Leo tunataka kuwaaminisha kuwa sisi ni mafisadi kuliko CCM kwa sababu wao wanaonyesha kubadilika+ sisi tunakwenda-

    ReplyDelete

Top Post Ad