Sipo na Shilole Hivi Sasa - Nuhu Mziwanda

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Msaniii Nuhu Mziwanda ambaye kwa sasa anafanya poa na wimbo wake mpya 'Bilima' amefunguka na kusema kuwa kwa sasa hayupo na Shilole, Nuhu amesema hayo leo alipokuwa Kikaangoni akichat na mashabiki kupitia ukurasa wa facebook wa EATV.
Tweet

Toka ulipoaanza mwezi wa ramadhan kulikuwa na tetesi kuwa msanii Nuhu amehama kutoka kwa Shilole na sasa anaishi kwake mwenywe hilo limethibitishwa Nuhu alipokuwa akijibu swali la kwanini mpaka sasa anaendelea kuishi na Shilole kwenye nyumba ambayo Shilole amepanga.
"Hapana sipo na Shilole kwa sasa mimi nipo kwangu"
Lakini kauli ya Nuhu haina maana kuwa mapenzi yao yamekufa lahasha bali amempisha mwenzake katika kipindi cha mfungo wa ramadhan kutokana na misingi ya imani ya mpenzi wake na kudai kuwa licha ya hilo hivi sasa yeye mwenyewe anakwake na anamaisha yake mwenyewe.
Maswali mengi ambayo mashabiki wa ukurasa wa EATV walikuwa wakiyauliza yalikuwa ni kuhusu maisha ya mapenzi kati yake na Shilole hivyo walikuwa wakihitaji kufahamu mambo mbalimbali ambayo huenda wanaona kama yanazushwa na jamii hivyo ilikuwa ni sehemu ya wao kupata ukweli, mashabiki wengi walikuwa wakiiuliza inakuaje anakubali kupigwa pigwa na mwanamke kama mtoto na hapo ndio Nuhu Mziwanda alipoweka wazi suala hilo la yeye kupewa kichapo na Shilole.
"Hamna mapenz bila kugombana na siku zote ukitaka kudumu na mwanamke usimuonyeshe ubabe sababu mwanaume wa kweli hapigi na hata kama ukipigwa kibao na mwanamke hauwezi kufa hivyo ni vema kua kama mwanaume na kusamehe"
Mbali ni hilo Hit maker huyo wa Bilima alikana suala la yeye kulelewa na Shilole na kusema kuwa yeye ana maisha yake na mpenzi wake huyo ana maisha yake pia hivyo halelewi kama ambavyo baadhi ya watu wanavyosema mitaani kuwa analelewa na kutunzwa na Shilole.
"si kweli mimi silelewi maana nina maisha yangu na shishi ana maisha yake so tumekutana tu kimapenzi ila watu wanajudge tofauti ila wanapaswa kutambua kuwa mimi na maisha yangu na Shishi pia ana maisha yake binafsi,ni mapenzi tu yanafanya kuwa kitu kimoja"

MATUMIZI YA LUGHA
Msanii huyo amekiri wazi kuwa yeye lugha ya kiingereza si lugha yake hivyo makosa ambayo anakuwa anayafanya katika matumizi ya lugha hiyo ni ya kawaida sababu tu si lugha yake ila anazidi kujifunza zaidi ili aje kuwa na matokeo mazuri katika kutumia lugha hiyo ya kiingereza, hivyo anakubali wazi kuwa kile alichokuwa amepost katika mitandao yake ya jamii haikuwa makusudi bali ni bahati mbaya na yote ni sababu ya kutofahamu lugha hiyo kwa undani zaidi
"kingereza si lugha yangu nilikosea kweli ila bahati mbaya ila nazidi kujifunza, hivyo tegemeeni matokea mazuri kwenye hiyo lugha toka kwangu"

IMANI ZA KISHIRIKINA
Baadhi ya mashabiki wamekuwa wakisema kuwa msanii huyo anajihusisha na imani za kishetani kwa kutumia alama ya 666 katika mitandoa yake ya kijamii,lakini yeye amekuja kuweka wasa na kusema kuwa yeye anamuamini Mungu hivyo hana imani hizo lakini pia amesisitiza kuwa haamini kama namba hizo zinatumika na watu wanao amani ushetani,
"Sina imani hizo na siamini kama hiyo namba ni illuminat na kingine ukiamini hiyo namba ni illuminat basi itakudhuru ila mimi na muamini Mungu tu"
Katika safari yake ya Maisha Nuhu Mziwanda anasema hataweza kusahau kamwe siku aliyosafiri na kwenda nje ya nchi halafu akaachwa kwenye treni na wenyeji wake anadai hiyo siku katika maisha yake haitakuja kusaulika kirahisi,na kwa kumalizia aliweza kuweka wazi kuwa anatarajia kuja kufunga ndoa na Shilole na kuoana naye kama Mume na Mke kwa sababu anamiini kuwa wanapenda na ndiyo maana bado wapo pamoja sasa kwa mwaka wa pili katika mahusiano yake.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. HONGERA SANA!!!!

    ReplyDelete
  2. MM nasema hauna ndoa baina ya muisilamu na mkristo kwahiyo miezi mengine hamna mungu hata wakikaa nyumba moja hawapati zambi ila mwezi wa ramadhani unapata zambi

    ReplyDelete

Top Post Ad