Wema Sepetu na Aunty Ezekiel Beef Upya...Chanzo Nimekuwekea Hapa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


URAFIKI wa mashaka! Mastaa wawili wa filamu Bongo, ambao walikuwa mashosti  kwa muda mrefu kabla ya kidudumtu kuingilia kati hivi karibuni na kusuluhishwa, hivi sasa bifu kati yao limeanza upya, Risasi Mchanganyiko linakujuza.

Chanzo chetu ambacho hakipepesi macho kinasema tangu Aunt ajifungue mtoto, Wema hakuwahi kukanyaga nyumbani kwake kwa ajili ya kumuona, kutoa hongera au hata pole kwa rafiki yake huyo, isipokuwa wamekuwa wakichati kupitia simu za mikononi, kitu ambacho si sahihi.

Lakini kali zaidi, ni kitendo cha Wema kushindwa kuhudhuria sherehe ya kutimiza siku 40 tangu azaliwe mtoto huyo, Cookie, kitu kilichomfanya mwenzake kumuondoa kabisa katika orodha ya marafiki zake.

“Yaani Aunt kipindi chote alimvumilia akijua huenda yuko ‘bize’, lakini kwa kutofika kwenye siku hiyo muhimu, amemtoa kabisa akilini mwake,” kilisema.

Baada ya kupata habari hizo, gazeti hili lilimtafuta kwa njia ya simu Aunt ili kuthibitisha ubuyu huo, lakini akakubali tu juu ya kutohudhuria kwenye tukio hilo muhimu la mtoto wake, licha ya kuwa alimpa taarifa.

“Hakuja, lakini siwezi mlaumu sana, labda alikuwa na majukumu mengi, ukizingatia hivi sasa ana mambo ya ubunge,” alisema.

Wema hakuweza kupatikana baada ya simu yake kutopokelewa kwa muda wote alipopigiwa.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Bifu liko wapi hapo udaku ni nomaaaa😈

    ReplyDelete
  2. Bifu liko wapi hapo udaku ni nomaaaa😈

    ReplyDelete
  3. Udaku mnachefua na hamna utu. Kwa nini mnatumia picha alipokuwa akiomboleza kifo cha baba yake? Kwa kweli acheni haya mnachuma mno dhambi.

    ReplyDelete
  4. wachochezi nyiee.
    i wish umgechochea vita za madawa ya kulevya.
    mxxxxx

    ReplyDelete
  5. udaku manna zenu sasa beef apo limeonekana wapi jifunzeni kuandika heading inayoendana na kitu husika NK

    ReplyDelete
    Replies
    1. Na mshangaaa sana tu huyu alieandika kichwa cha habari!!!!! Mbona unamchukia bila saabu? Umetumwaa? Wewe ukifiwa na mzazi wako miaka iliyota ,utajisikia vipi leo hii mtu akuzushie hishu chafi alafu aambatishe na picha ya uliokuwa ukimlilia mzazi wako? Kamuombe WEMA samahani.

      Delete

Top Post Ad