Rais Kikwete, Mkapa na Makongoro Nyerere Waishambulia UKAWA kwa zamu......Magufuli Aahidi Kuwashughulikia Mafisadi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Rais Jakaya Kikwete, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa na Mtoto wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Makongoro Nyerere wameshambulia vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).

Wakizungumza kwa zamu katika Uwanja wa Jangwani jijini Dar es Salaam wakati wa kufungua kampeni za chama hicho wamesema, mgombea wa UKAWA hana sera za wapinzani.

Katika mkutano huo uliotawaliwa na vijembe kwa UKAWA Rais Kikwete bila kutaja jina amesema, katika umoja huo kuna mgombea anayesimama kama mgombea binafsi kwa kuwa, sera zake ni tofauti na chama anachosimama kugombea.

Alikwenda mbali na kuonesha kushangazwa kuwa, mmoja vyama viwili ambavyo sio msingi wa chadema ndio vimesimama katika ngazi ya urais na mgombea mwenza wake.

Rais Kikwete aliwalenga Mgombe Urais wa Chadema, Edward Lowassa aliyejiunga na chama hicho akitokea CCM pamoja na Juma Duni Haji aliyejiunga na Chadema akitokea Chama cha Wananchi (CUF).

“Wagombea sio wa Chadema. Mmoja ni CCM na mmoja ni CUF.., Pale kuna mgombea urais ambaye unaweza kusema kama mgombea binafsi maana ana sera zisizofanana na chama,” amesema Rais Kikwete na kuongeza “lakini wameyataka wenyewe.”

Hata hivyo Kikwete hakumwacha Waziri Mkuu Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Frederick Sumaye aliyejiunga na chama hichi siku moja iliyopita.

Kikwete amesema, pamoja na Sumaye kujieleza lakini hakumwelewa alichokuwa akikusudia “nimejaribu kusikiliza anasema nini lakini sikuelewa kabisa,” amesema.
.
Hata hivyo amesema, CCM haikubahatisha kumteua Dk John Magufuli kuwa mteule wa chama hicho katika urais na kwamba, “tumemweka kwa sifa zake, tunataka rais anayeipenda nchi na anayependa wananchi wa nchi hii.”

“Magufuli anayo sifa hiyo. Tumesema, hatutaki kuchukua mgombea mwenye makando kando mengi na tukatumia muda wetu mwingi kujitetea sisi na yeye kabla ya kuomba kura. Tunamtaka mgombea mwaminifu, mwadilifu. Safari hii Mungu kamchagua Magufuli.”

Kabla ya Rais Kikwete kuzungumza, alitanguliwa na Mkapa ambaye amesema, kuna vyama vinawadanganya Watanzania kuwa wanawatafutia ukombozi-wapumbavu.

“Kuna chama kimoja tu cha ukombozi hapa Tanzania, ni CCM iliyotokana nas ASP na TANU. Kuna vyama vinawadanganya Watanzania eti wanataka kuwakomboa wananchi-wapumbavu, nenda nchi zote za jirani uliza chama cha ukombizi Tanzania watakwambia CCM. Nina kila sababu ya kusema wapumbavu,” amesema.

Hata hivyo amesema, haitoshi kusema mtu anauchukia umasikini peke yake.

“Haitoshi kusema unauchukia umasiki, lazima useme unauchukiaje umasikini?” amesema Mkapa.

Lowassa katika hotuba zake mbele ya wananchi kwenye safari zake za kutafuta wadhamini alipokuwa CCM na hata baada ya kuhamia Chadema, amekuwa akisema anauchukia umasikini-haupendi.

Hata hivyo Mkapa amesema, timu ya CCM ni madhubuti kwa kuwa Magufuli anapenda kushirikiana na wenzake, yupo mstari wa mbele katika kutekeleza mambo yote ya umma na kwamba, wakati wote ni mfano wa tabia nzuri kwa vitendo vyake.

Makongoro ndio aliyefungua ukurasa wa mashambulizi kwa UKAWA kwa kumvaa Sumaye baada ya kujiengua CCM.

Makongoro amesema, anamshangaa Sumaye aliyejiunga na vyama vinavyounda UKAWA na kwamba, alipaswa kukubali matokeo ya kushidwa

Makongoro alianza kwa kibwagizo “kuna mmoja-au niache?- kuna yule kaka yangu mmoja nasikia afya yake sio kweli. Kuna huyu mwingine wa jana (Sumaye)?

“Sumaye tumpige kanzu au tumuache hivihivi, kwani angetulia tungeshughulika naye, kajileta mwenyewe sasa mimi nifanyeje, nimpige tobo?” amesema na kuongeza;

“Sumaye akiwa Waziri Mkuu na kaka yangu Kikwete (Rais Kikwete) waliingia kwenye tano bora, Sumaye alikuwemo, kura zake hazikutosha zikatosha za Kikwete, kwa kuwa aliingia tano bora akasema, chama kizuri.

“Miaka 10 baadaye tano bora hakuingia- Sumaye akatuambia mkimpa Lowassa kugombea urais hiki chama mimi nitahama, sasa huyo ni mkweli ama muongo. Hii ndio shida ya kusema uongo, kusema rahisi kuukumbuka tabu,” amesema Makongoro.

Katika mkutano huo, mgombea mwenza wa CCM, Samia Suluhu Hassan amesema, atasimamia na kuwawezesha akina mama.

Pia ameahidi kusimamia pesa Sh. Mil 50 zinazotolewa na serikali kwa ajili ya kupelekwa vijijini.

“Nitasimamia kuwawezesha akina mama, pesa za vijijini Sh. Mil 50 zitatoka kwa ajili ya vijijini nitazisimamia. Mimba za utotoni nitasimamia kuhakikisha zinaondoka, pia nitahakikisha maji yanapatikana na kusaida akina mama wote,” amesema.

Akizungumzia uzowefu alioupata amesema, amekuwa karibu na Makamu wa Rais wa sasa, Dk. Mohammed Gharibu Bilal hivyo hakuna wasiwasi katika nafasi hiyo.

“Nilikuwa kwenye mikono mizuri ya Dk. Bilal, najua kazi zilivyo nawahakikishia Ofisi ya Makamu wa Rais itasiamama vyema kutekeleza ilani ya uchaguzi pamoja na muungano,” amesema.

Dk. Magufuli amewaahidi watanzania kujikita katika kutetea maendeleo ya wananchi kwenye Nyanja zote.

Dk. Magufuli amesema utawala wake utajikita katika masuala ya kilimo, afya, uchumi na amani ya nchi.

“Watanzania natambua mnapenda kuona mabadiliko, nitasimama vizuri katika miradi ya uchumi. Watanzania nawahakikishia shida na matarajio yenu nayajua, nayafahamu na natambua ninao uwezo wa kuyashughulikia.

"Mnataka suala la rushwa, wizi serikalini vikomeshwe haraka. Kwa kuwa palipo na rushwa ufisadi hakuna maendeleo, nitasimamia hilo,” amesema.

Amesema, kama atachaguliwa “nitahakikisha naunda mahakama maalumu ya kushughulikia mafisadi na majizi yafungwe haraka.”
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

30 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Yaani mkapa unawatukana watanzania unavaambia ni malofa na wapumbavu? Kisa? Pesa jeuri? Umepata wapi hiyo pesa? Si ulituibia? Kuwapatia akina Peter Maro nyumba za Posta wafanye zao za kuufanyia biashara ndio sio upumbavu...wewe ndie una nepotism, ni mpumbafu zaidi wewe. Badala ya kutoa haja unawatukana watanzania (hata kama sio wote), lakini umetutukana. Nani hujui wizi kwenyw meremeta, nani hujui wizi kwenye rada. Yaani wewe mwenyewe umemwambia Sumaye kuwa waziri mkuu kwenye serikali yako kwa miaka 10, leo unamwita mpumbavu? Kama ni mpumbavu, na wewe mkapa ulikuwa boss wake, basi na wewe ni mpumbavu na lofa SQUARED. Pennine wewe ni zaidi ya majina hayo. Tikutegemea katika level yako uweze kuheshimu utu wa mtu, lakini, kuanzia sasa nitakudharau sana, kama wenzao wLiotuita kwamba ni vibaya wenye njaa zetu ndio maana tunataka mabadiliko. Of course, tuna njaa ya miaka 50-60 ya uongozi wa ccm, of course ni CCM NDIO vibaka, ndio maana ndovu za tembo zikaweza kupiga AIRPORT. BWANA MKAPA UMETUUDHI SISI WATANZANIA

    ReplyDelete
    Replies
    1. kakuudhi wewe peke yako mimi naogezea ni wabumbafu

      Delete
    2. Usisemee watanzania kama wametukanwa wote sema ni wewe na aliyekutuma unazungumza kama na unajiti la jang'ombe matakoni maana linavyokusulubisha mpaka una kosa akili

      Delete
  2. Mbona hujaweza kusimamia ufisadi katika wizara yako ya UJENZI. TANROAD wizi mtupu. Barabara inajengwa asubuhi, jioni ina mashimo. Au nikuambie na wewe ulichukua chako mapema? Utasimamiaje system (au mfumo ambao wewe mwenyewe umekulia - MAGUFULI USITUDANGANYE). Miaka kumi umekaa kwa kikwete umeshindwa kuuliza PEMBE ZA NDOVU ZIMESHIKWAJE PALE USWISS, LEO UNASEMA UTASIMAMIA HAYO. KAHADAE WATOTO WADOGO. Umeshindwa Escrow (mbona ccm imewarudisha akina ANNA TIBAIJUKA mbona hujaongelea hilo; kina chenge mbona unaogopa hilo!! Lol, watanzania wakati huu, tutumie karatasi zetu na wino wetu - TUWAAMBIE WATU HAWA - BASI. Wanaona hii nchi ni ya KWAO. Wanafikiri hapa ni uholanzi au uingereza kwa MALKIA, NA KING...hakuna hilo. Hii ni saa ya UKOMBOZI! Hii ni saa ya UKOMBOZI mwananNGU!! MAMA YANGU. TANZANIA INAHITAJI UKOMBOZI TOKA KWA MAKABURU WEUSI WANAOTUTUKANA KWA SABABU TUMEWAPA VYEO!

    ReplyDelete
    Replies
    1. sasa huyo anaye tetemeka midomo mpk mkono ndo atakukomboa

      Delete
    2. Anageuka mzima mzima kama robbot......

      Delete
  3. ccm mbele kwa mbele

    ReplyDelete
    Replies
    1. Waacheni waandamanee, CCM mbele kwa mbele.........

      Delete
  4. Kwani upumbavu ni tusi?mbona hamjui kiswahili nyinyi waswahili!

    ReplyDelete
    Replies
    1. We ndio hujui kiswahili mpumbavu, mpumbavu ni mtu asiyejielewa kabisa!! na hata nyerere alilijua hilo akasema nawaita wajinga maana mjinga anaweza kujifunza lakini sio mpumbavuuuu....

      Delete
  5. Huwez jua kuwa ni tusi maana naww pia nimpumbavu

    ReplyDelete
  6. Huwez jua ni tusi maana naww ni mpumbavu...

    ReplyDelete
  7. kwahiyo mlisikia upumbavu tu au? kweli ukawa kazi mnayo, msubirini mheshimiwa fulani atatangaza kuhamia chadema soon ili aje awasaidie kufungua kampeni maana imeonekana nyie pekee hamuwawezi kabisa wazee wa dola, mwambieni mgombea wenu ajifunze kutetea sera zake mwenyewe kwanza, halafu apunguze swaga za ukaskazini maana kama sumaye ndio ameua kabisa ule mchakamchaka wenye nyimbo nzuri mlizokua mnaimba tangu januari, MAGUFULI yeye tu peke yake anauzika, mmeyataka wenyewe na mvimbe mpasuke........CCM MBELE KWA MBELEEE, labda mumbembeleze ZITO awasaidie kuichafua CCM ingawa mmechelewa tayari, tunataka sera imara sio kama kutafuta mchumba baa unamdanganya nitakufungulia glocery yako, huu ni URAIS jamani hatunadi ukabila HAPA KAZI TU

    ReplyDelete
    Replies
    1. Magufuli selema,CCM selema
      Selemaselema.

      Delete
    2. ACHANA NAO HAO MDAU,25/10/2015 WATAKAA TU.
      CCM MBELE KWA MBELE,MAGUFULI ANOGILE!

      Delete
    3. Wanataka yatukute yale ya Libya,
      mbona wanajuta sasa hivi,MUNGU IBARIKI TANZANIA.

      Delete
  8. Of couze ccm tutsiyondoa kwa damu na sio kwa bao.la kisigino kama alivyo sema nape nyie mnao itea ccm no wapumbavu sisi guano chukizwa na uhuni wao tumeshajitolea kuwanchinja ngedere wore mkiwemo na nyie mnayo itetea tumechoka kundamizwa na mikodi mikubwa na umasikini saws loawasa mtukaneni sana ila ndio chaguo la tulip funguka nyie tutawafungua kwa kuchinja at a watoto wenu wasrnge kabisa nyie mnao zidi kuigandamiza nchi kwa ulimbukeni wenu walisha wagawia shilingi ngapi mnatoa comment za kishenzi hapa uku ukitoka halo ujui ulenini nyoko nyie

    ReplyDelete
  9. Na ya Libya yatakuja ikiwa ccm itapita tupo tulip jitoa muhamga kwa faida ya watoto wetu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Unazungumzia CCM 'A' au "B"..........clarify!!

      Delete
  10. MAGUFURI NA SAMIA WAMESHANGAAA AWAMU ZOTE 4 KWAMBA HAZIKUWAJIBIKA KABISAAA,ILA NAJIULIZA 50 MILIONI KILA KIJIJI?MAHAKAMA YA MAFISADI? WAKATI ALIKUWA NAO WOTE PALE PALE KAMA SIO USANIII NI NI

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kweli juha hawezi kuwa mwerevu utalaumu mchezaji kakosa goli akiwa benchi lazima utathimini wakati huo alikuwa wapi na sasa atafanya nini akiwa ya ndani ya uwanja usiwe na fikira potofu kila wizara na usimamzi wake leo hii huwezi kumkusanyia yote majukumu na kumhukumia usitake kuchagua pumba ukamwaga mchele kisa umekinai utahitaji kujaza tumbo lako wakati umebakia na pumba mahakama ya mafisadi sasa inawezekana kwani mfano hai CCM Mafisadi nje na ndo una wataka wakuletee mabadiliko wajitayarishe October 25

      Delete
    2. SAWA MKUU UMENENA VEMA KAMA ANAUBAVI AANZA NA JK Escro,RIZ MOKO,MIRAJI KIKWETE NA, SIMBA TRUST,MKAPA NA MAKAA YA MAWE ALIO JIMILIKISHA,NA KUJIUZIA NYUMBA ZA SERIKARI KWA BEI CHEEEEEEE,KUMBUKA TIMU, KOCHA NA MFUMO NI ULE ULE USITEGEMEE MAGOLI HAPO DAWA KUUNDA KIKOSI KIMPYA NA KUBADILI MFUMO

      Delete
  11. sasa ww fikiria mtu mmoja anasaidiwa na referee (kikwete); malaizmen (mkapa, mwingyi, warioba), lakini watazamajo WOTE wanashangilia TEAM nyingine! Nyie hamuoni maajabu hayo? Gone are those days --now it is ccm chini chini zaidiI.. gone are.those days now it is fikira za mwenyekiti zzzzzzz!! ccm ina ukoma; ccm ina kipindupindu; ccm inakohoa kama makongoro nyerere!! Ccm sasa ni MWISHO. Someni alama za nyakati nyie!

    ReplyDelete
  12. POLE SANA NAKUSIKITIKIA SIJUI WAJUKUU ZAKO UTWAWAMBIA NINI SIKU UKIAMKA KUMEKUCHA

    ReplyDelete
  13. Alietuambia watz wapumbavu atuombe msamaha! maana Nyerere alitufafanulia kuwa wajinga ni neno zuri maana naweza kujifunza! lakini mpumbavu, Biblia inasema ni mtu asiyejielewa kabisa!!! na nyerere alisema nawaita wajinga siyo wapumbavu!! please msamaha unahitajikaaaa. UKAWA oyeeeee.

    ReplyDelete
  14. KWELI MKUU CCM IMECHOKA JANA SIJASIKIA HATA LA MAANA ZAIDA YA MATUSI NA MIPASHO YA PWANI KWELI CCM CHAMA CHA WASWAHILI TARAAABU MBELE KWA MBELE

    ReplyDelete
  15. Let us ASK them to give us something tangible - that we can weigh them on!! These two GUYS: Magufuli na Salima on the same OLD stuff BLA BLA BLA! Gone are those days of clapping our hands without knowing exactly what we were UP to! Gone are those days of Zidumu Fikira za Mwenyekiti! In the modern age, where can use the Internet to compare our own lives with those of Malaysia; Singapore and of all places - one of the poorest nation on earth (i dont have curent data on this though) - Banglandesh - one keeps on wondering - kwa nini tudanganyike na hawa wajamaa wanaotaka kuifanya hii nchi kama ya kimalkia au you wafalme (monarchy-yaani wao watawale tu.....pia na hata wake na watoto zao waendelee kututawala tuuuuu? Wamepata mali kutokana na vicent vyetu vichache tunavyolipia kodi au hivyo vicent wamaekani au watu wa nchi za scandnavia wanazotupa HALAFU WANATUONA SISI NI MALOFA, MAFALA, WAPUMBAVU.. Ww mkapa kwanza unatakiwa ushtakiwe kwa kutumia lugha ya namna kwa kiongozi uliyepata bahati ya kutembelea nchi za wenzetu wastaarabu. Umeshindwa kutoa HOJA zenye NIDHAMU. Unawafundisha nini wanao? Unawafundisha nini wajukuu zako! Nilifikir kiongzoi ni KIOO kumbe wewe ni sawa sawa na uchafu ULIOPO kwenye KIOO UNAOZUIA WATU KUIONA SURA YAO VEMA! Mkapa umeshindwa kwa hilo! Kikwete umeshindwa kwa kuwaambia watanzania - kufurahia utashi wa mkapa bila kuulaani! NEC mmehsindwa bila kutoa TAMKO kwa HILI jambo. Police wa Tanzania mmeshindwa bila kumchukulia hatua kali huyu BWANA! Eeh bwana uturehemu sisi malofa wa tanzania tutakaopiga kura yetu Octoba 25th!! Amen!

    ReplyDelete
  16. Na wewe anon wa Aug 25 saa 8:42 pm: Na nyerere alisema PIA kwamba mpumbavu ni sawa na kulinganisha mtu mfupi na mtu mrefu! Labda watu wafupi ndio wapumbafu! Asante Mwalimu. MUNGU AKUREHEM Huko Uliko. Hata ungerudi leo, ukakuta pale msasani ulippoacha palivyojengwa bila kuangalia mkondo wa maji; ukiangalia maghorofa yaliyojengwa mjini dar es salaam bila kuangalia ramani ya jiji, au kupitishwa na idara husika za jiji na kusababisha maafa; na pia ungeona jinsi pembe za ndovu zinavyopita uwanja wa ndege na siku hizi tuna X-ray machine (wakati wako ulipokuwa hai tulikuwa hatuna hizo machine lakini ndovu hazikupita kijinga hivyo). Ukiamka leo ukakuta jinsi madawa ya kulevya yalivyozagaa huko mitaani (na wauzaji wa "unga" ni vigogo wa ccm uliyoiacha; na ukija tena leo ukakuta watu hawana maji; DENI letu mwalimu limeongezeka hadi TRILLIONI ZA DOLLARS ZA MAREKANI; NA mwalimu nigkuambie nini - ukiamka leo utakuta shillingi yetu ya tanzania imekuwa sawa na madafu tu - kwa sababu wasanii wa bongo hasa walioko ccm hawataki kuitumia tena BASI wanataka kutumia dolla kununulia mboga huko kariakoo; wanawahonga wanenguaji kwenye majukwaa. Mwalimu nikuambie tena, jaribu uamke leo utakuta watoto wetu wanakaa chini - karibia shule zote; hawajui kusoma na kuandika mara wamalizapo shule ya msingi; ni vigumu kwao kwenda chuo kikuu; na wakienda au kubahatika kwenda vyuo vikuu vilivyopo, basi usiombe akimaliza hawezi kujilinganisha na mtoto aliemaliza chuo kikuu cha level hiyo hapa duniani! Eeh, Mungu akurehemu mwalimu kwa sababu ukiweza kuamka leo utakuta wadau wa tanesco wanakata umeme bila hata taarifa. Mwalimu ukiamka leo utakuta lile neno ulilokataa kuwaita watanzania "mpumbavu" ndilo analotumia Mkapa ambae alichukua urais baada ya mwinyi. Unakumbuka ulimsaidia kwenye kampeni? Mwalimu ukiamka leo - naaamini utaenda UKAWA - outright! Bila kuchelewa! Mwalimu ukirudi wewe na kenyatta mtakuta hata vile vyama mlivyofikiria ni vya kuwakomboa watu wa africa mashariki, leo vinatumika kama mahala pa kuwatukana watanzania - viongozi wa chama ulichokiasis yaani, ccm wamewatukana watanzania na kuwaita majina mengi: oil chafu; makapi; moto wa mabua. Mwalimu si unakumbuka ulikataa kujengewa nyumba kubwa? Basi mkapa kajichotea kila kitu halafu akajenga lijumba huko Lushoto utafikiri yeye nI tembo!! Basi amejuchukulia vile viwanda ulivyojenga kafanya ni vyake yeye na mkewe. Mwalimu, unakumbuka zile nyumba za oysterbay? Basi Mkapa; Kikwete na Magufuli wazijiuzia kwa bei chee. Mwalimu kazi uliyofanya kwa miaka 24 imeharibiwa kwa kipindi cha chini ya miaka 10-15!! Mwalimu natamani ungeamka leo umsikilize mwanao Makongoro anavyotumia majukwaa kuwatukana watanzania wanaojaribu kuikomboa Tanzania mara ya pili. Unajua mwalimu? Eti Kikwete alishikwa na BUSHA tu hapa akapanda ndege kwenda MAREKANI ili kupata consultation!! Mwalimu, ukienda hospitali ya mwananyamala, hakuna hata DAWA!! Mwalimu mimi ni mtanzania wa kawaida.................sijiwezi..tena ninaililia tanzania mwalimu. Je wewe ungerudi leo, ukaiona tanzania ambayo nimekusimulia hapo juu (na hiyo ni asilimia moja tu, yaani 1/100). Mwalimu natamani urudi, lakini, hapana utawapiga makofi hawa watu wa ccm uliyoiacha! Mungu akurehemu, Mwalimu wetu, baba wa Taifa letu la TANZANIA!

    ReplyDelete
  17. Wewe tobo fungua semina watu wakuelewe sio kutujazia ushuzi na kutupozea muda kusoma hilo libarua lako refu kupita maelezo unamwandikia nani mkalishe somo hilo mkeo nyumbani

    ReplyDelete
  18. Mdau 3:20 AM Wewe tobo fungua semina watu wakuelewe sio kutujazia ushuzi na kutupozea muda kusoma hilo libarua lako refu kupita maelezo unamwandikia nani mkalishe somo hilo mkeo nyumbani

    ReplyDelete

Top Post Ad