Magufuli Awataja LIVE WanaCCM Wanaomsaliti Huku Wakimsanifu Kuwa Wanamuunga Mkono

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli, jana aligeuka mbogo baada ya kuamua kuwataja hadharani watu wanaohujumu kampeni zake kwa kujifanya mchana wako pamoja na usiku wakigeukia upande wa upinzani.

Akiwahutubia wananchi wa mkoani Shinyanga jana katika mkutano wake wa kampeni uliofanyika katika Uwanja wa CCM Kambarage, Dk. Magufuli, alisema kuna mamluki wanaokihujumu chama hicho katika kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25, mwaka huu.

Dk. Magufuli aliwataja hadharani baadhi ya makada hao ambao wamekuwa wakiipigia kampeni CCM mchana na usiku wakiwapigia wapinzani.

 “Kuna baadhi ya wana-CCM wanatujuhumu sana, wengine nawajua hata majina yao bahati nzuri huwa sisemi uongo bali ukweli, kuna huyu Gasper mchana tunakuwa naye CCM lakini usiku anaungana na wapinzani,” alisema.

Hata hivyo, kauli hiyo ya Dk. Magufuli ilipokelewa kwa mshangao na  baadhi ya wananchi na wanachama waliokusanyika uwanjani hapo, kwa kuwa baadhi ya makada hao walikuwa wameketi jukwaa kuu wakifuatila hotuba yake.

Mwandishi wa habari hizi alimshuhudia meneja kampeni wa mgombea huyo, Abdallah Bulembo, akimfuata Magufuli na kumnong’oneza ghafla Magufuli alibadilisha na kudai msaliti ni Gasper Anthony wala si Gasper Kileo aliyetajwa awali.

Hata hivyo, Magufuli  baada ya kumaliza hotuba yake alimfuata kada huyo na kumkumbatia huku akimtuliza na kuendelea na msafara wake.

Kada huyo aliyetajwa kuwa msaliti anadaiwa awali kuwa mpambe wa mgombea wa urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa, anayeungwa mkono na vyama vinavyunda Umoja wa Katiba (Ukawa).

Akizungumza katika mkutano huo wa kampeni, Kileo alisema alimuunga mkono Lowassa akiwa CCM, lakini kwa sasa anamuunga mkono mgombea urais wa chama hicho, Dk. Magufuli na wala kwa kilichotokea hatarajii kukihama chama.

Akiwahutubia mkoani Shinyanga, Magufuli amesema hashangai wananchi kuanza kumwita rais kwasababu hata yeye anajua kuwa ndiye atakayeibuka na ushindi mnono kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu.

Alisema wagombea wengine wa nafasi ya urais ni wasindikizaji tu kama walivyo wapambe wa kwenye harusi.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

14 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. UNAYO KAZI BULEMBO .NA IMEKUWA BAHATI MBAYA KWELI KWELI KWA SABABU NA WEWE BULEMBO KICHWANI FYATU,BOSI WAKO KICHWANI FYATU ,HAPO SIMUONI WA KUMUOMBA MWENZIE MAJI.MAGUFULI AMEUFANYA UDHALILISHAJI WA DARAJA LA JUU KWA BWANA GASPER AKIMTAJA KUWA NDIYE MSALITI WAKE ALIYEMO KWENYE MSAFARA WAKE,AJABU YA MUNGU .YEYE ANGEWEZA KUMKATAA KWA KUAGIZA TUU WASAIDIZI WAKE WAMUONDOE,LAKINI KITENDO CHA KUMSHAMBULIA KWA MANENO MAKALI HADHARANI KIMEMVUNJIA HESHIMA SIYO GASPER BALI YEYE MAGUFULI,NA UKICHANGANYA NA HUKU KUWEWESEKA KWAKE MARA KWA MARA KWA,VITUKO VYA KUTISHA NI WAZI AMETUONYESHA HAFAI URAIS,TENA HAFAI KWA ASILIMIA MIA MOJA 100% RAIS GANI MWEHU!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Angalia uiano wa CCM na UKAWA inayoundwa na vyama vingi,bado hukubali Magufuli ndio Rais?Hahahahahaha!Tatizo akili za bamia ndio zinawaongoza.

      Delete
    2. SURE.
      Raisi wa nchi anatakiwa awe mtu mwenye hekima na uwezo wa kupokea mambo kuchuja na kujua lipi la kusema na lipi la kuacha huku ni kukurupuka ambako hakufai kwa kiongozi wa nchi.

      Delete
  2. Wapo wengi Subirini
    Watazuka last minute
    Ndo atalia kilio cha Mende na push up zake

    ReplyDelete
  3. Unawatakia nini wewe hata akiwataja haikuhusu wacheni ushabiki MAGUFULI OYEEEEEEEEEEEEEEEEEEE mtachimba mpaka mchoke na maswali yenu ya kitoto kutafuta kiki

    ReplyDelete
  4. tunataka ukweli na uwazi ili watu wakome kufanya usaliti kwani wajue wataumbuliwa hadharani.
    wakiwambiwa nyumanyuma ndiyo wanazidi kufanya makosa kozi wanajua watafichwa.

    tajaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

    ReplyDelete
  5. mwehu wewe unayeropoka ujinga, naona hujitambui, unafikiri wt wote wana akili km zakwako

    ReplyDelete
  6. kama wanauhakika wa kushinda ccm kwa nini wanatumia pesa nyingi katika kampeni kuzurura na wasanii chungumzima na mibango kila kona

    ReplyDelete
  7. ukisikia die-hards wa ccm ndio hawa,wanaelezwa,tena kwa kisayansi lakini bado hawasikii,hawaelewi.yaani wapo wapo tuu,wanasubiria vichinjio vyetu viwakate vibaya jumapili tarehe 25 octoba 2015

    ReplyDelete
  8. CCM hawana jipya hawana dira hawana maono juu ya taifa ni genge la watu waliojaa matusi mipasho hujuma na kejeli. Watu hawaongei ya msingi wanamuandama mtu mmoja kama yeye ndiyo tatizo la nchi au ndiye aliyeharibu nchi .Huu ndiyo ule ujinga alioupiga vita Nyerere. Haishangazi kuona wakitumia wanamuziki kuwahadaa wajinga ambao wamewatengeneza kwa miaka yote hamsini. Huo ndiyo mtaji wao na silaha pekee.

    ReplyDelete
  9. DAAAH MZEEE POLE KUMBE NDIO UMEJUA LEO, POLE SANA MBONA WAPO WENGI TUUUU ILA WAKUCHORA TU HUYO ULIEMTAJA NI SISIMIZI UKITAJIWA NA WENGINE UTAJITOA KATIKA KAMPENI NA KUJIUNGA NA UKAWA SIKU HIYO HIYO,AU KUZIMIA KABISA NA PUSH UP ZAKO.

    ReplyDelete
  10. Wewew ulio andika Lowasa Ikulu unaonekana ni mjinga kama Lowasa

    ReplyDelete
  11. CCM OYEEEE MAGUFULI HAPA KAZI TU

    ReplyDelete

Top Post Ad