Prof. Mark James Mwandosya Kuhamia Upinzani?

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mark James Mwandosya
Tangu jana kumekuwa na taarifa za moja kati ya makada maarufu na wenye ushawishi ndani ya CCM Prof.Mark Mwandosya kuhamia upinzani, taarifa hizo zimekuwa zikienea kwa kasi sana na kuchagizwa vilivyo na vibaraka wa propaganda za CHADEMA na UKAWA bwana Yeriko Nyerere na wenzake.

Baada ya kuendelea kuzagaa kwa taarifa hizo nimeamua kufanya uchunguzi wangu binafsi dhidi ya madai hayo lakini nilichoambiwa na mmoja kati ya watu wa karibu sana wa Prof.Mwandosya na familia yake ameniambia kuwa PROFESA mara kadhaa amekuwa akihojiwa na watu mbalimbali wakiwemo waandishi wa habari pamoja na baadhi ya wanachama na makada waandamizi wa chama amekuwa akijibu na kusisitiza kuwa HANA MPANGO WA KUHAMA CCM.

Aidha duru za udadisi zinaeleza kuwa PROFESA kwa sasa yupo nchini MAREKANI katika shughuli zake binafsi.
Kwa kuwa wakati ni ukuta nadhani tusubiri tuone ataamua nini, kwenda kujivua nguo upinzani kama SUMAYE na mwenzie LOWASSA au ataendelea kulinda heshima na utu wake akiwa ndani ya CCM.

MUNGU IBARIKI TANZANIA
MUNGU BARIKI UCHAGUZI
MUNGU MUONGEZE PROFESA MWANDOSYA KATIKA KUTOA MAAMUZI YAKE
AMEN.

By Kawakama
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Aliyekuambia kwenda upinzani ni kujivua nguo ni nani? Tumia akili yako vema. Acha ushabiki

    ReplyDelete

Top Post Ad