Angalizo kwa Mbowe, Mnyika, Kubenea, Mdee, Tundu Lissu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Ni dhahiri kuwa sasa uchaguzi umekamilika mara baada ya tume kumtangaza mshindi wa urai ndgu yetu John Joseph Pombe Magufuli kuwa ndiye rais mteule kwa mjibu wa matokeo.

Ushauri wangu kwamba kwa upande wa wabunge wa viti maalum naomba watoke hata kule ambako CDM haikushinda lakini imefanya vizuri. Kuna kushinda lakini pia kuna kufanya vizuri sana japo hukushinda. Hii inaweza kuwa karata ya kukiimarisha chama kwa kuwa si kwamba baada ya kushindwa wanachama wa CHADEMA ndo wamehamia CCM, hapana, bado wapo kabisa na cha kushangaza hawana imani na CCM na mteule Magufuli wenyewe bado wanaamini mabadiliko hayatatoka CCM hata siku moja ila ni mpaka upinzani uingie madarakani.

Hivyo basi, kwa kuwapa nafasi ya mbunge viti maalumu bila shaka italeta nguvu mpya ya mshikamao na mbunge huyo kazi yake nyingine itakuwa ni kuendelea kufungua matawi mapya huku akiyaimarisha yale yaliyopo tayari.

Mungu bado anaipenda CHADEMA na wana CHADEMA wote popote walipo ndani na nje ya nchi na ndiyo maana tumeona kabisa kuwa safari hii Chadema kimepata nafasi ya kuunda na kuongoza halimashauri nyingi yakiwemo na majiji makubwa mfano Arusha, Mbeya na pengine Jiji kuu la Dar. Hii ni fursa kubwa mno kuliko wakati wowte w uwepo wake ktk siasa za Tanzania.

Ombi lakini pia angalizo: Hakikisheni kuwa kwa mara ya kwanza Jiji la Dar limekuwa chini ya upinzani, na mfanye juu chini na uzalendo kabisa kuwa mgombea wa CCM hapati nafasi ya kuwa Mayor kwakuwa madiwani wengi na wabunge wengi Dar Es Salaam wanatoka upinzani.

Hivyo siasa ni mahesabu yalichanganyikana na science bila kusahau technique na akili-maarifa. Kulichukua Jiji kuu kama Dar ni nafasi ya heshima sana kwa chama pinzani kwa kuwa jiji hilo ndiyo sura ya nchi nzima. Hivyo basi fanyeni kazi usiku na mchana ili kuwaletea kile wananchi walichokikosa toka CCM na ndo kaana wakawakataa kwa njia ya kura. kwa kutumia mapato ya Jiji, Boresheni miundo mbinu, elimu, afya na nafasi za biashara kwa watu wenye hali ya chini maana hawa ndo walioichoka CCM, matumaini yao ni kwenu.

Hivo hivo na kwenye halimashauri za wilayani mfano Ukerewe, Arumeru Tunduma na kwinginepo fanyeni kiume mkawe hodari kwa vitendo na mipango yenu yote ilete matokeo bora kwa watu husika. Jengeni shule za secondari za kisasa zenye maabara na mazingira safi, jengeni shule za msingi safi na zenye ubora kwa watoto huku mkijali maisha ya waalimu kwa kuwajengea nyumba kwa kuwa hela mnazo za halimashari.

Naamini kufikia 2020 mtakuwa mmeshapata mtaji mkubwa mno mtakao uhubiri kwa watanzania huku mkitoa mifano ya kazi zenu kwenye zile halimashauri mlizoongoza kwa miaka mitano ijayo.

Hii itakuwa karata nzuri isiyohitaji maneno mengi bali iliyojaa vitendo na utimilifu wa ahadi walizonadi wagombea. Watu washachoshwa na maneno matamu ya CCM yasiyo na vitendo, basi ninyi mtakuwa mfano bora endapo mkizifanyia hayo niliyoshauri hapo juu halimashauri zenu yakiwemo na mjii, naamini uchaguzi ujao mtakuwa na nafasi kubwa sana ya kuongoza halimashauri kam siyo zote basi thelui tatu ya wilaya zote nchi nzima. Na hapo ndipo CCM itapoteza nguvu kabisa kuanzia serikali za mitaa hadi ngazi za wilaya na majiji, na huu ndo utakuwa mwisho wa CCM.

Naomba kuwasilisha kwenu wadau na wapenda nchi yetu si kwa ushabiki usiyo na ufahamu wa hali halisi ya Taifa letu ilivyo, kwamba CCM imetumia hila hasa kwa wale walioishia elimu ya msingi wengi wao wanaishi vijiji kwa utafiti wa TWAWEZA ulivyoonyesha.

By Obsaver
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Waache kuweka wachaga wenzao na ma'girl friend zao, we unasema nini..........PIPOOOOOOOOOS PWAAAAAAAAAAA

    ReplyDelete
    Replies
    1. Poyoyo huna jipya..... ccm ni ile ile ile ileeeee chama cha walaji tanzania

      Delete
  2. Tumeshawazoea,kila chaguzi matamshi ya mwisho wa CCM hutamkwa sana lakini mwisho wa siku mnaangukia pua.CHADEMA,CUF msahau kushika dola,mnakurupuka mno,sijui mnadhani kuongea kwa kutoa mapovu ndio ushujaa?Haitatokea mtoe rais atuongoze,Ila kwa mbali naona ACT-wazalendo kuna rais atatuongoza napo endapo tu CCM wataboronga.

    ReplyDelete
  3. Hao wote ulowataja hapo juu wamrudishiea 'Edo' pesa yake alowahonga ili kuwaziba midomo, sio vizuri jamani, msimfanyie hivyo 'babu wa watu'.................hayo sio mahaba, ila ni DEKO KWELIKWELI

    ReplyDelete
  4. Mtoa mada anaota ndoto za saa saba mchana kwani hajuhi kuwa mbowe ni mcheza dili?Hivyo lazima atawateua mabinti wa kichagga wacheza dili wenzake na sio nyie kutoka kwa wala dagaa huko!

    ReplyDelete
  5. Ccm iliwacheza bila kujua walimtuma Lowassa huko nyinyi mkazani eti mmepata mgombea ahahaaa alikua mgombea wa ccm kubali isikubali ukweli njo huwo. Na mwaka 2020 tutatuma mwingine tena kama vile tulifanya kwa Lowassa. Eti upinzani mnachezwa bila kujitambua.

    ReplyDelete
  6. 🔓🔒🔏🔐Yan, tuwe wakweli, upinzani kwa hapa tz bado hauna ngvu, kumbuka lowasa amepewa support na vyama vinne vya ukawa lakin bado kashindwa, kashindwa na 🔓🔒🔐🔏🔑 magufuli ambaye kasimamishwa na chama kimoja tu.

    ReplyDelete
  7. angalizo ni zuri sana,naongezea kwa ENL huu usiwe mwisho wako baba umeleta hamsha hamsha ya nguvu kura hazikutosha cha msingi tuliza akili tengeneza afya yako 2020 urudi ukiwa ngangari na kama jpm ataboronga tia tim upya jpm akifanya vizuri sababu nia yako ni maendeleo pumzika mwache amalize 10yrs zake 2225 kuwa mshauri damu mpya wape mawazo yako uliozani yataleta maendeleo ;pongezi nyingi kwa amsha amsha ulioileta ENL na pongezi nyingi kwa JPM kwa ushindi kama ulivoona 58%sio ushindi mkubwa sababu tunataka mabadiliko maisha bora kwa kila mtanzania sio kwa mawaziri na familia zao na marafiki zao tu leta mabadiliko ya kweli 2020 upate zaidi ya 70%umeona mijinini ulivopoteza sababu mijini ndio tupo up to date tumechoka kila kizuri cha waziri au mtoto wa rais tunataka pia watoto wa mkulima wapiga kazi nao waneemeke tuone magorofa yao marefu mijini(maisha bora kwa kila mtanzania)siasa isiwe ndiosehemu ya kutajirka viongozi waadilifu na sio wafanya biashara cake ya taifa iwe kama birthday cake kila mmoja aionje

    ReplyDelete
  8. Hivi wewe ni Observer au ni kada? ninachokiona kwa upinzani huu amuwezi kufika kwa sababu hamna think Tankers wazuri na hawana strategy. Basi watu hao mnaowaamini kama profs katika nyanja nyingi uenda sasa wamechoka.Umoja wenu umeanza kupiga deal watu kutafuta urais as if ni ujumbe wa nyumba kumi,hapohapo watu wanapiga deal na kutajirika kwa watu kushindwa kufuatilia na kuhoji matokeo yake mnaanza kudai mmeibiwa kura. Mzee Slaa aliwuliza akina Mbowe hivi Lowasa ni Asset au Liability? na akauliza tena na CHIZI je? wakajibu ni hodari wa kuiba kura.Hivi kwa staili hii mtafika?Kilichofanyika wakati huu upinzani hasa Chadema kuchukuwa mjini na majiji ni hali ya matajiri waliopo miji hiyo kutoka kaskazini na limejulikana tayari, sasa dawa ni kulipa kodi inayotakiwa na utawala wa sheria halafu tuone 2020. Wengi wa matajiri hao ni receiver wazuri wa mali za wizi hasa Bandarini,Godouwns na wakwepaji wakubwa wa kodi.Nchi hii haiwezi kuongozwa kwa ukanda, ukabila na udini. Nina imani kuwa tabia hiyo ikiendelea uenda hali ya kila mtu kwao itajitokeza na hulo ardhi hakuna. Acheni mchezo mchafu wa ukabila na mfano wenu mmeona huko Mwanza na Morogoro na Dodoma. Mnachokifanya kitawaghalimu na sasa wananchi wameanza kawafahamu vizuri kuwa mwisho wa yote nyinyi mtawagawa kwa kigezo cha mabadiliko. Ngoja Maghufuli aapishwe kwani kila kitu anakijuwa na ataungwa mkono na waliompa ridhaa ya kuliongoza taifa hili. ALUTA CONTINUA.

    ReplyDelete

Top Post Ad