Zari Amvua Tiffah Hiziri iliyowekwa Mkononi Mwake na Bibi yake Mama Diamond

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

DIAMOND upoo! Zarinah Hassan a.k.a Mama Tiffah amechukua uamuzi mgumu wa kumvua mwanaye Tiffah ile dawa aliyokuwa amefungwa mkononi ‘hirizi’, hali iliyowafanya watu wengi wabaki na vingi viulizo.

Awali, Tiffah alivishwa hirizi hiyo siku chache baada ya kuzaliwa na Diamond akaizungumzia kuwa, ni utamaduni wa kawaida ambao kwa mila za Kibongo siyo tatizo.

Hata hivyo, wakati Diamond akitoa ufafanuzi huo baada ya watu kuibua maneno kuwa ‘hirizi’ hiyo inahusiana na mambo ya kishirikina, Zari alidaiwa kutokubaliana na uamuzi huo na ikadaiwa kuwa, alishindwa kugoma ili kutomkwaza mama Diamond ambaye ndiye aliyefanya zoezi hilo.

Baada ya Tiffah kudumu na ‘dawa’ hiyo kwa miezi michache (kitu ambacho si cha kawaida), Zari alipokwenda Sauzi alifanya maamuzi magumu ya kwenda kinyume na utamaduni na mzazi mwenzake na kuamua kuivua ‘hirizi’ hiyo.


Ushahidi wa Zari kufanya hivyo unaonekana kwenye picha za hivi karibuni alizoposti kwenye ukurasa wake wa Instagram ambapo moja inamuonesha Tiffah akiwa kavaa ‘hirizi’ hiyo na nyingine hana.

Kufuatia uamuzi huo, baadhi ya Wabongo walionesha kumshangaa Zari huku wakimponda kuwa alichokifanya siyo sawa.

Unajua ule ni utamaduni wa bwana wake, alitakiwa auheshimu hata kama kwao mambo hayo hayapo. Kitendo cha yeye kwenda Sauzi na kumvua Tiffah ile dawa ni kuonesha dharau, amemdharau Diamond na mama yake pia, siyo sawa,” alisema shabiki wa Diamond aliyejitambulisha kwa jina la Mariam.

Diamond hakuweza kupatikana mara moja kuzungumzia uamuzi wa mzazi mwenzake huyo.

Source:Global Publishers
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ss angekaa nayo mpaka lini?

    ReplyDelete
  2. zari umefanya vizuri kumvua, ukiwachekea hao waswazi watamrithisha mikoba yao.

    ReplyDelete
  3. Jamani kwakweli waTZ hatueleweki. Kipindi kile alipovalishwa huo 'mvuje' kuna walioponda kishenzi, leo kavuliwa tena limekuwa baya....mbona hamsomeki...NGACHOKA

    ReplyDelete
  4. Hongera zari
    Acha kutembea na vilema WA akili

    ReplyDelete

Top Post Ad