Baba Lowassa, Sumaye na Babu Kingunge Sheria ni Msumeno

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Sheria zetu za nchi haziruhusu kujadili matokeo ya urais mahakamani, so to say, huwezi kuyaquestion kokote isipokuwa kwa wananchi. Na ukishitaki kwa wananchi utasababisha uvunjifu wa amani, na hakuna mtanzania hata mmoja atakayekubali ujinga huo wa kuvunja Amani.

Twende mbele, turudi nyuma. Wakati sheria hizi zinatungwa, au zinafanyiwa marekebisho, Lowassa, Kingunge na Sumaye walikuwa CCM wakiyapinga mapendekezo ya wapinzani kutaka matokeo ya urais yajadiliwe mahakamani; wakaisimamia katiba mbovu iliyopinga uwepo wa tume huru ya uchaguzi.

Leo sheria zile walizozisimamiawakiwa CCM ndiyo zimewatafuna. Wameonja joto ya jiwe walilolirusha wenyewe. Hawana tena uwezo wa kushitaki kuhusu matokeo waliyoyapata, na sisi hatupo tayari kuandamana.

Hapa wanalazimika kukubali kukubaliana na wasiyokubaliananayo, maana wakati yanatengenezwa waliyatetea. "Walitega mtego mtego ambao umewanasa wenyewe".

Nampongeza sana Mbowe kwa kuwakaribisha hawa wanaCCM ndani CDM. Angalau wale waliobaki CCM watajifunza kutetea maslahi ya nchi badala ya kutetea maslahi ya chama na maslahi binafsi.

By COARTEM/JF
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. mbowe kawaponza wenzake ......polen wazee wetu

    ReplyDelete
  2. Kwa kweli nafurahi Sana kuona vijana wenzangu tunatambua kuwa uchaguzi umeisha Na japo tunaumia lkn sheria zetu Ni mbovu. Hivyo sasa Ni wakati WA kukishughulikia kimoporo kilichobaki nacho Ni katiba pendekezwa. Yaliyotokea yamesababishwa Na katiba mbovu tuliyonayo. Uchaguzi huu liwe somo kwetu kuhusu umuhimu WA katiba katika mustakaali WA taifa. Kumbuka katiba hairuhusu vyama kuungana, kupinga matokeo ya raisi mahakamani, madaraka makubwa ya raisi, uwajibikaji WA viongozi, nk. Ambayo yote yametuonyesha ktk uchaguzi huu. Nao wajibu WA kuijenga nchi kupitia katiba bora. Vinginevyo akina chenge watapeta akina kafulila watalia Tu.

    ReplyDelete

Top Post Ad