Ridhiwani Asema Hana Chuki na Wasiompigia Kura

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

MBUNGE wa Jimbo la Chalinze wilayani Bagamoyo mkoani Pwani, Ridhiwani Kikwete amesema hana chuki kwa wale ambao hawakumpigia kura kwenye uchaguzi uliofanyika Jumapili kwani hizo ni changamoto za uchaguzi.

Aliyasema hayo jana kwenye Uwanja wa Miembe Saba mjini Chalinze wakati wa mkutano wa hadhara wa kuwashukuru Wanachalinze kwa kumchagua kuwa mbunge kwenye Uchaguzi Mkuu uliofanyika Jumapili.

Ridhiwani alisema licha ya baadhi ya maeneo kutompigia kura za kumchagua kuwa mbunge, lakini atawatumikia wananchi wote bila ya kujali kama walimpigia kura au la kwani kila mtu ana haki ya kumpigia kura mgombea yeyote anayempenda.

Nawashukuru wananchi wote walionipigia kura na hata wale ambao hawakunipigia kura kwani hiyo ndiyo demokrasia nitahakikisha nawahudumia wananchi wote bila ya kuwabagua nitahakikisha napeleka maendeleo kwa watu wote wa jimbo hili,” alisema Ridhiwani.

Alisema kutopigiwa kura kwa wingi siyo sababu ya kuwagawa wananchi kwani hizo ni changamoto za uchaguzi ambao unakuwa na mambo yake ambapo baadhi ya maeneo walipiga kura kwa kuzingatia ukabila.

Sitakuwa na chuki wala hasira kwa wale ambao hawakunipigia kura nitashirikiana nao katika suala la maendeleo ili kuhakikisha jimbo letu linakuwa na maendeleo na wananchi wanaboresha maisha yao ili yasonge mbele,” alisema Ridhiwani.

Aidha, alisema atahakikisha Mji wa Chalinze ambao umekuwa Halmashauri ya Mji Mdogo unajengwa kwa kuwekewa huduma muhimu ili wananchi waboreshe biashara zao hasa ikizingatiwa kuwa mji huo ni wa kibiashara.

Moja ya mambo nitakayoyafanya ni kufanya Chalinze kuwa makao makuu ya Halmashauri hiyo na baadaye kuwa wilaya kwani mchakato unaendelea na tunaamini baada ya muda tutapewa wilaya hivyo tutaweza kujitegemea na kujiimarisha kiuchumi,” alisema Ridhiwani.

Alibainisha kuwa wananchi wasiwe na wasiwasi kwani kukichagua Chama Cha Mapanduzi CCM ni kuchagua maendeleo hivyo wasubiri kuona jinsi serikali mpya itakavyofanya kazi kwani kwao ni kazi tu.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCM Chalinze, Nasa Karama alisema mbunge huyo ameonesha uwezo mkubwa kwani kwa kipindi alichochaguliwa cha mwaka mmoja na miezi mitatu amefanya mambo makubwa ambapo alitumia ziadi ya Sh bilioni moja na zaidi miradi ya maendeleo.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Jizi tuu, linandaliwa kuja kututawala mbeleni

    ReplyDelete
    Replies
    1. Piiiiiipoooooosssss Pwaaaaaaaaah!!!

      Delete
  2. Na wewe ndo mtambo wenyewe, Ooh PANONE ya Patrick kumbe mjinga wewe umejiweka wewe. Mnafikiri mtawadanganya wangapi na mara ngapi? Mtatafuna mali za watanzania mpaka lini? Za mwizi ni 40 siku zako zikifika utajuata kuwa mtoto wa KIKWETE. Zote mtakazotafuna zitakuja kuwatafuna watoto na wajukuu zetu nyambaf nyie.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Taratibu unatutemea mate.....haya baada ya yote hayo ulosema hebu tuma salamu kwa uwapendao kisha uchague na wimbo wakusindikiza salamu zako

      Delete
  3. Uso umejaa masundosundo mtoto mdogo
    Yana mwisho hayo

    ReplyDelete

Top Post Ad