MICHEZO Jose Mourinho kufukuzwa Chelsea? huu ndio msimamo wa Chelsea kwa sasa ….

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mmiliki wa klabu ya Chelsea ya Uingereza raia wa Urusi Roman Abramovich tumezoea kuona akifukuza makocha kwa haraka zaidi endapo tu mwenendo wa timu yake utakuwa sio mzuri kwa kipindi kifupi, tabia ya tajiri huyo wa Kirusi imekuwa ikihusishwa kwa kiasi kikubwa kutimuliwa kazi kwa Jose Mourinho kutokana na mfululizo wa matokeo mabaya.

Wakati wengi wakiwa wanahisi kuwa huenda Jose Mourinho atafukuzwa kazi muda wowote kutokana na kipigo alichokipata kutoka kwa Southampton, mchana wa October 5 tovuti ya Chelsea iliandika ujumbe ambao unatajwa kuwa utaongeza kujiamini kwa timu na kocha, kwani katika kipindi kigumu kama hiki, huwa ni kawaida kwa kocha na wachezaji kupoteza hali ya kujiamini.

“Klabu inaweka wazi kuwa Jose Mourinho ataendelea kuungwa mkono na klabu kama kawaida, licha ya kuwa Jose Mourinho alisema timu imekuwa haina matokeo mazuri na inahitaji kuimarika, hivyo tunaamini tuna kocha mzuri msimu huu na anaweza kuleta mafanikio”>>> Chelsea

Chelsea ina wakati mgumu katika msimu huu kwani imecheza mechi nane, imeshinda mbili, sare mbili na kufungwa michezo minne, kwa sasa Chelsea ipo nafasi ya 16 katika msimamo wa Ligi Kuu Uingereza. Jose Mourinho aliwahi kuwa kocha wa Chelsea katika kipindi cha mwaka 2004 hadi 2007 na kufukuzwa kazi na mmiliki wa klabu hiyo  Roman Abramovich, kabla ya kurejea kwa mara ya pili mwaka 2013.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad