Shindano la Serengeti Masta Lahitimishwa Kanda ya Ziwa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mshereheshaji Alifa Said akiwaonyesha wadau wa bia ya Serengeti mshindi wa jumla wa shindano la Serengeti Masta kwa mikoa ya kanda ya ziwa Bw. Said Kanolo ambaye alijishindia kiasi cha Tsh. 100,000/=kwenye shindano hilo linaloendeshwa na bia ya Serengeti Premium Lager lililofanyika katika baa ya Shooters jijini Mwanza. Kampeni hiyo imefikia kikomo kwenye kanda hiyo baada ya kuzunguka kwenye baa za mikoa mbalimbali ya kanda hiyo kuwatafuta washindi ambao walitambua ladha halisi ya bia ya Serengeti Premium Lager ambapo pia ilifanikiwa kuwafikia wahudumu zaidi ya mia tano wa baa tofauti ambao walifunzwa juu ya utoaji wa huduma kwa wateja kitu ambacho kilisaidia katika kupanda kwa mauzo ya bia ya Serengeti Premium Lager katika baa husika.

Mshindi wa jumla wa shindano la Serengeti Masta Said Kanolo (katikati) akifurahi na wadau wa bia ya Serengeti Premium Lager, wakati wa shindano la mwisho la Serengeti Masta kwa wateja wa kanda ya ziwa lililofanyika katika baa ya Shooters iliyopo barabara ya Airport jijini Mwanza. Kampeni hiyo ya Serengeti Masta imedumu katika kanda hiyo kwa takriban muda wa miezi (2) sasa ikiwakutanisha wateja na meneja wa bia hiyo katika kujifunza kwa undani kuhusiana na bia hiyo ambapo zawadi mbalimabli zilipatikana.

Mshindi wa jumla washindanola Serengeti Masta kwa wakazi wa kanda ya ziwa Said Kanolo (kushoto) akipokea fedha taslim Tsh. 100,000/= kutoka kwa Afisa mauzo wa Kampuni ya bia ya Serengeti Joan Semguruma, (kulia) wakati wa shindano la mwisho kwa kanda ya ziwa la bia hiyo lililofanyika katika baa ya Shooters iliyopo Barabara ya Airport jijini Mwanza. Ushindi wa jumla wa Bw. Kanolo kwa wateja wa kanda ya ziwa umekuja baada ya kuwashinda wateja wengi walioshiriki katika kutambua ladha halisi ya bia hiyo na kuielezea kwa undani ambapo mwanzo wa Kampeni alishinda Tsh. 50,000/= pamoja na zawadi nyingine kutoka bia ya Serengeti Premium Lager katika baa ya Cross parkjijini Mwanza nakufanikiwakutingafainali. Kampeni hii imezunguka katika baa mbalimbali za kanda ya ziwa ikiwaburudisha wateja wa bia hiyo na kuwafundisha wahudumu wa baa mbalimbali juu ya utoaji huduma kwa wateja.

Wadau wa bia ya Serengeti Premium lager wakigonga cheers, ndani ya baa ya Shooters iliyopo barabara ya Airport jijini Mwanza wakati wa shindano la mwisho la kumtafuta Serengeti Masta wa jumla kwa mikoa ya kanda ya ziwa katika baa hiyo. Kampeni ya “Serengeti Masta” imedumu katika kanda hiyo kwa takriban miezi miwili na imezunguka baa kwa baa kusaka washindi mbalimbali wanaotambua ladha halisi ya bia hiyo lakini pia imetoa elimu kwa wateja wake kuhusiana na chapa hiyo namba moja kutoka SBL.

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad