Mgombea Ubunge ‘Aliyetekwa’ Mtwara Apatikana.......Ndugu Wasimulia Tukio Zima, Polisi Wasema Wanachunguza Kama Ni Kweli Au Lilipangwa

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mgombea  ubunge  jimbo  la  Mtwara  Mjini  kupitia  CHADEMA,  Joel Nanauka alipotea  katika  mazingira  ya  kutatanisha  tangu  juzi  na  kukutwa  ametupwa  nje  ya  mlangoni wa jengo la Kliniki/kituo cha afya  hapo  Mtwara.

Ndugu  wa  mbunge  huyo  wameusimulia  mkasa  huo  kama  ifuatavyo:

"Ndugu yetu Joel Nanauka ambaye anagombea Ubunge Jimbo la Mtwara Mjini kupitia CHADEMA, alipotea katika mazingira ya kutatanisha siku ya Jumatatu Tarehe 5/10/2015. Siku hiyo alitoka kwenye shughuli za kampeni akiwa na wenzake na walirudi nyumbani akiwa amechoka.
 
"Majira ya saa kumi na mbili na nusu, alimtumia mwenzake ujumbe mfupi wa mkononi (SMS) akimjulisha kwamba kuna mtu amekua akimtafuta tangu wiki iliyopita waonena na mchana wa siku hiyo alimfuata ofisi ya CHADEMA lakini hakumkuta, hivyo anakwenda kuonana naye mara moja eneo linaloitwa Mnarani hapa mjini Mtwara. Eneo hilo sio mbali na nyumbani kwao.

"Muda mrefu ulipita bila kurudi nyumbani huku giza likiwa limeshaingia. Tulizana kupata mashaka na ndipo tukaanza kumtafuta kwa simu na ilitushtua zaidi baada ya kuona simu yake haipatikani (imezimwa).
 
"Jitihada za kuwasiliana na kila ambaye tulidhani angeweza kuwa anajua alipo au kua na habari zake zilifanyika bila mafanikio.
 
"Tuliwasiliana na viongozi wa CHADEMA jimbo la Mtwara Mjini lakini nao hawakua na habari. Tulipoona muda unazidi kwenda tulitoa taarifa polisi na kwa kushirikiana nao tulimtafuta Joel usiku mzima bila kuonekana.
 
"Siku ya jana (terehe 6/10/2015) ilipita bila kua na habari zozote za wapi alipo jambo lilitupa hofu ya uwezekano wa kuwa ametekwa. Polisi waliendelea na jukumu lao a upelelezi.

"Asubuhi ya leo (Jumatano tarehe 07/10/2015) majira ya saa kumi na mbili asubuhi, Ndugu Joel alikutwa ametumwa mlangoni mwa jengo la Kliniki/kituo cha afya hapa Mjini Mtwara akiwa hajitambui, amechoka, amechafuka na shati lake limechanika.
 
"Alipewa huduma ya kwanza na alipoanza kupata fahamu amekua akilalamika kuwa ana maumivu makali ya shingo na mbavu ikionesha huenda alipigwa.

"Hadi sasa hatujui nini kimetokea na Polisi bado hawajatoa taarifa zozote na ndugu Joel yuko chini ya unagalizi wa madaktari katika hospital ya Mkoa wa Mtwara.
 
"Ikumbukwe jimbo la Mtwara Mjini ni kati ya majimbo ambayo umoja wa wananchi UKAWA hawajafikiana kuteua ugombea mmoja wa Ubunge na hivyo bado kuna wagombea wa vyama vya CUF, NCCR na CDM.
 
"Siku kama tano zilizopita, Ndugu Joel alitoa kauli kupitia radio mojawapo hapa Mtwara akieleza nia ya kujitoa kugombea Ubunge  kwa maelezo kwamba umoja wao umeshindwa kuafikiana juu ya nani agombee.
 
"Pia alisema kwamba amekua akifanyia siasa chafu na wenzake na huku yeye mwenyewe na familia yake wakititishiwa maisha.

"Hata hivyo, siku moja baadaye, chama chake kilitoa kauli kwamba hakijamkubalia kujitoa kwenye kinyang'anyiro na hivyo analazimika kuendelea na kampeni.

"Kwa mazingira haya tunaamini kwamba tukio la kutekwa na kuumizwa kwake lina uhusiano na siasa za uchaguzi mkuu na matisho aliyokua ameyapataka kabla ya tukio hili."

Kauli  ya  Jeshi  la  Polisi
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Henry Mwaibambe  amesema  kuwa  jeshi lake linachunguza kwa kina taarifa za kutekwa kwa mgombea ubunge jimbo la Mtwara mjini (Chadema) Joel Nanauka na endapo litabaini kuna udanganyifu ameufanya dhidi ya tukio hilo hatua za kisheria zitachukuliuwa dhidi yake.

Akizungumza jana, Mwaibambe alisema wanalichunguza tukio hilo ili kubaini kama kuna ukweli, kutokana kuwapo kwa tetesi zinazoonyesha huenda tukio hilo lilipangwa kutokana na mazingira ya kutoweka kwake hadi kupatikana.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kazi ndogo sana hiyo kwa jeshi letu la polisi,tutajua tu mbivu na mbichi.

    ReplyDelete
  2. Naona Polisi wanaamua kufanya upotoshaji wa makusudi juu ya hili swala,na unaweza kuona kauli zao zikionyesha kabisa kuna kitu kinafichwa.
    Kwanini waibuke na statement ya kwamba ni staged mwanzoni kabisa mwa maelezo?
    Kwanini waanze kuchange direction ya upelelezi tangu mwanzo?
    "Wameshindwa kumpata" kwa makusudi baada ya kupewa taarifa then wanakuja mwishoni wanataka kutoa kauli ambazo hata mtoto mdogo anajua kuwa anadanganywa.
    Katika hili mkajipange vizuri.
    Ukweli utawaumbua muda si mrefu.
    Msisahau,anayekutumikisha kupindisha haki dhidi ya mwingine leo,akimaliza na wewe anaweza kutumia mwingine kupindisha haki kinyume/dhidi yako.
    Mnakubali kutumika kama big G mbele ya haki za msingi za raia?
    Polisi mlienda kufanya nini sasa?

    ReplyDelete
  3. Kwa kauli zile zinazotolewa na polisi.....
    Ni dhahiri kwamba hata uchunguzi hautakuwa wazi na kwa ajili ya kuchunguza utekwaji.....
    Kwa kifupi:
    Mwenendo wa polisi hauleti matumaini ya haki kutendeka.

    ReplyDelete
  4. Ni dhahiri ni hao hao ukawa wenyewe kwa wenyewe ndio 'wame-mafiana' wakigombea hiyo nafasi moja ya ubunge. Wananchi wa Mtwara mjini, dawa yao ni 'kuwapiga chini' hao wote wanaogombana, jimbo apewe mgombea wa CCM

    ReplyDelete
  5. Hamna issue ya Ukawa hapo,
    Hamna vyama vinavyounda ukawa kwenye hili.
    Vyama vianvyounda ukawa Tangu lini vikatumia polisi kufanya mambo kama hayo?
    kwa nguvu ya Propaganda inayofanywa n polisi pamoja na watu wengine unaweza kujua ni nini kinaendelea.....
    Sisi watu wa Mtwara tunajua msimamo wa Joel juu ya issue ya Gesi.
    ..na wote mnajua muhusika wa mikataba na aliyelazimisha kuwapa gesi wachina ni nani....
    Hii ni zaidi ya uchaguzi,situation ya uchaguzi imetumika ili kufunika msingi wa nini kinalengwa na kupata mwanya wa kupindisha ukweli.

    Wanasahau kuwa madaraka yana muda,na siku ikigundulika ukweli,na tukiwa na Luongo anayejali maswali ya macho kweli,kuna uovu mwingi sana wa wakubwa utawekwa wazi.

    Na wengi sana hawatapenda maovu yao yawekwe wazi.

    ReplyDelete

Top Post Ad