Ticker

6/recent/ticker-posts

Zari Hawezi Kuhamia Tanzania Moja kwa Moja – Diamond Platnumz

Nafasi za Ajira Serikalini Zilizotangazwa Wiki Hii Bonyeza HAPA

Nafasi za Internship Zilizotangazwa Bonyeza HAPA

Matokeo ya Form Four 2022 Bonyeza HAPA

Diamond Platnumz na Zari The Boss Lady tayari wameziunganisha familia zao kwa kumpata mtoto wao wa kwanza Tiffah, lakini hakuna mpango wa mrembo huyo Mganda kuhamia moja kwa moja Tanzania ili kutengezeza familia moja.

Diamond a.k.a Baba Tiffah licha ya kuwa amekuwa akitoa ahadi ya kufunga ndoa na Zari bila kusema lini, amesema kuwa hakuna mpango wa Zari kuhamia Tanzania moja kwa moja kutokana na kuwa na biashara zake Uganda na Afrika Kusini.

“Kusema Zari atakaa moja kwa moja kubase Dar, Tanzania itakuwa ni ngumu lakini atakuwa muda atakaokaa kule na huku ni sawa kabisa atakuwa Tanzania, atakuwa pia South Africa, atakuwa Uganda kwasababu anabiashara zake tofauti tofauti anazozifanya.” alisema Diamond alipokuwa akijibu swali la shabiki siku ya 40 ya Tiffah, aliyeuliza kama Zari atahamia Tanzania.

Aliendelea kusema;
“Sasa ukimwambia mtu abase na biashara zake kuzihamisha sio rahisi kihivyo…na huwezi kujua kibiashara itatengeza nini, na mwanzo wa mapenzi kufanya vitu vya kumkwamisha mwenzako kimaisha haiwezi kuleta maana.”

Tiffah ni mtoto wa nne kwa Zari, watoto wake watatu wa kiume aliowapata na mume wake wa zamani Ivan wanaishi Afrika Kusini yaliko makazi ya Zari. Huenda hiyo ikawa ni sababu nyingine japokuwa Diamond hakuitaja.

Post a Comment

6 Comments

 1. Domo anajaribu kuficha ukweli, Zari hawezi kuishi tz si kwa biashara zake tuu, na watoto na ivan je?

  ReplyDelete
 2. atafanya ufuska saa ngapi akiishi bongo! amdanganye huyo dai

  ReplyDelete
 3. KWANI KAOLEWA HATA AKAE BONGO? KAONA MAMBO SIYO ALIVYOFIKIRIA

  ReplyDelete
 4. tobaaaaaaaaaaaa! Katunzi nae anataka mtoto apimwe DNA.

  ReplyDelete
 5. Katunzi kashindwa kuvumilia nae katoa la moyoni, anataka DNA ya Tifaa, ijulikane kunyoa au kusuka.

  ReplyDelete
 6. Aishi popote si mapenzi yao jamani
  Si tatujalishi

  ReplyDelete
Emoji
(y)
:)
:(
hihi
:-)
:D
=D
:-d
;(
;-(
@-)
:P
:o
:>)
(o)
:p
(p)
:-s
(m)
8-)
:-t
:-b
b-(
:-#
=p~
x-)
(k)