Sasa Tunakwenda Kushuhudia Tofauti ya UKAWA Kushika Dola na CCM Kurudi Madarakani

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Tutakachoshuhudia katika awamu hii ni kuibuliwa kwa madudu makubwa huku wakuu wa mashirika ya umma wakiwajibishwa kama mbuzi wa kafara lakini vigogo walioko kwenye system wakipeta au wakikamatwa wale dagaa tu.

Inawezekana kabisa,hawa wakuu wa mashirika haya ya umma walikuwa wanafanya kazi tu ya kulinda maslahi ya wakubwa na huenda wao wakawajibishwa huku vigogo hawa wakiachwa jambo ambalo serikali ya UKAWA isingelifanya.

Kumekuwepo na madai/tuhuma za vigogo kutumia majina ya baadhi ya wafanyabiashara wakubwa kuendesha biashara zao kitu ambacho sidhani kama serikali ya Magufuli itathubutu kukufanyia uchunguzi-UKAWA wangethubutu.

Hivi biashara ya madawa ya kulevya, magogo,meno ya tembo na hata hii ya kupitisha makontena kiholela bandarini haina baraka za wakubwa?Magufuli ataweza kuwawajibishi vigogo hawa pindi wakibainika?

Fukuafukua hii ya serikali ya Magufuli huenda ikawa "counter-productive" kwa CCM na serikali yake na jambo hili likiwa handled vibaya, huenda likafanya watu waichukie zaidi CCM badala ya kuipenda kama wengi wanavyodhani.

Anachokifanya hivi sasa Magufuli ni sawa kuwadhihirishia watanzani,tena kwa ushahidi, ni kwanini CCM haikupaswa kuchaguliwa kurudi madarakani na akishindwa kuwawajibisha vigogo watakaobainika atakuwa anajimaliza mwenyewe.


Hivi sasa UKAWA wamerahisishiwa kazi kwani karibu kila kitu kinaibuliwa na serikali yenyewe na wao kama wapinzani watakuwa na kazi ya kushinikiza hatua zichukuliwe jambo ambalo nina mashaka kama litatekelezwa kwa uaminifu hata kama itaundwa hiyo Mahakama ya Mafisadi.

Bungeni ndio kutakwenda kuchafuka na hapa ndio mtihani wa Magufuli na serikali yake kuchukua hatua utakuwa mgumu zaidi maana ndani ya bunge huenda yakaibuliwa mengi ambayo hatukuyatarajia.

Kwa mfano, yanayosemwa na watu na kuandikwa mitandaoni kuhusu kampuni ya Home Shopping Center huenda yakaibukia Bungeni na wabunge wa UKAWA wakadai uchunguzi ufanyike kuhusu kampuni hii.

Kufichua tuhuma na watuhumiwa ni jambo moja, na kushughulikia tuhuma na watuhumiwa ni jambo lingine.

Kwenye orodha hakuna wafadhili?

Tusubiri.

Source: By Salary Slip/Jamii Forums
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hao ukawa wanasubiri vigogo mafisadi watimuliwe na CCM wao wawape uongozi, kazi ya ukawa hasa chadema ni maneno matupu, MAFISADI PAPA wameyakumbatia.....HAPA KAZI TU

    ReplyDelete
  2. Chadema ya sasa hivi haija 'jeuri' ya kufichua wala kushughulikia mafisadi kama enzi zile za Dr. Slaa, chadema ya sasa ukiwa fisadi na unahela 'chafu' ndio utapewa uongozi. Kwa unafiki huu wa ukawa, CCM itaendelea kushika dola mpaka mwisho wa dunia...........CCM MBELE KWA MBELE

    ReplyDelete
  3. Hakuna mtu hata mmoja ambae yupo ukawa au ukawa wenyewe wanaweza kufikia maamuzi ya serikali ya Magufuli anayofanya sasa hivi kwa sababu wafanya biashara wakubwa wengi wapo ukawa,mtoa mada naona bado unaushabiki wa vyama naomba uondokane na hali hiyo ili tusonge mbele anachofanya Magufuli ni Unexpected hata ukawa hawakutarajia

    ReplyDelete
  4. ndg yangu acha uchamaaaaa. sasa tunajenga nchi, je nani mwenye mamlaka kukamata na kupeleka mahamani je ni chadema au ccm yenye dola? uchama hautakiwi tunapozungumzia mambo muhimu kama haya. zungumzia utendaji wa kazi na sio siasa. nitajie mtu wa ukawa aliyeshika dola akafanya vibaya. magufuli mwenyewe kwenye kampeni zake alitaja ccm mara chache zaidi kuliko kusema serikali ya magufuli, mafisadi yapo ndani ya ccm subiri siku zaja utasikia hata wale ambao hukudhani

    ReplyDelete
  5. MTOA MADA SIJAKUAELEWA KWA HIYO UNATAKA KUSEMA NINI KAZI INAYOFANYWA SASA IACHWE AU UNAMAANISHA NINI, NINA MASHAKA KAMA SIO WEWE MMOJAWAO BASI

    ReplyDelete
  6. We mtoa mada ni msenge sana hauna jpya hata angepewa nchi huyo babu yenu unafikiri angefanya maamuzi magumu kama ya JPM HAPA KAZI na ukome kuleta mada za kisenge zipeleke UKAWA

    ReplyDelete
  7. Makala pumba kabisa tena ya kifisadi kutoka kwa kibaraka wa mafisadi. Nani kama maghufuli kutoka ukawa? Wakati mwengine msituwekee makala hovyo kama haya yanatia kichefuchefu. Nchi hii kama si kuchaguliwa kwa magufuli ingekuwa imekwisha finished. Eti anachokifanya magufuli ni sawa kwadhihirishia watanzania kwamba CCM haikupaswa kuchaguliwa? Huo ni muweweseko wa hali ya juu wa kuchanganyikiwa wa ukawa lol. Kuna tofauti gani kati ya CCM fisadi anayoiangamiza Mr Magufuli na ukawa ile inayoongozwa na Lowasa na sumaye?Mr magufuli is just doing exactly what he promised in his campaigns, to bring a new accountability oreder to the Government and its employees and making Tanzania as one of the best place to live in Africa and trust me he wont back off until he finish the business. Watanzania mnatakiwa kuwapuuza wale wote watakao jaribu kukurejsheni nyuma maana hujuma yoyote zidi ya raisi hata ikiwa ya maneno zidi ya vita ya kilikomboa taifa hili kutoka katika hali ya umasikini mjue kabisa hiyo ni hujuma zidi yenu nyinyi wananchi mlio wanyonge kwa hivyo mtu yeyote mwenye kujaribu kumrejesha nyuma raisi katika vita hii hata ikiwa kwa maneno mtu huyo ni wa kumlani kwa nguvu zote.

    ReplyDelete

Top Post Ad