Semina Na Makongamano Yote Ya Serikali Kufanyika Online Kwa Tele-conferencing......... Hakuna Tena Posho Za Vikao Wala Viburudishaji

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

SERIKALI kupitia Menejimenti ya Utumishi wa Umma Ofisi ya Rais imesema haitagharamia gharama zozote za kuendesha vikao kazi na watendaji wake kuanzia sasa, badala yake vikao hivyo vitaendeshwa kwa kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHEMA).

Wahusika wakuu wa vikao kazi hivyo ni pamoja na Wakurugenzi, Makatibu Tawala wa Mikoa na Maafisa Utumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Florence Temba, Mkuu wa Kitengo cho Mawasiliano Serikalini na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, amesema kuwa, kupitia utaratibu huo washiriki wa vikao hivyo watabaki katika maeneo ya kazi ambapo wataunganishwa na mtandao wa pamoja kwa mfumo wa kuonana na kuongea uso kwa uso.

“Tulianzisha mfumo huo ili kupunguza gharama zisizo na ulazima ambapo awali ilitakiwa kila kunapokuwa na kikao lazma watumishi wasafili kuja Dar es Salaam kwaajili ya mkutano lakini kwa sasa tutatumia Video Conference iliyounganishwa kwenye mikoa yote nchini. Tumeokoa gharama za nauli, mafuta, chakula na malazi,” amesema Temba.

Temba ameeleza kuwa, hatua za utekelezaji wa teknolojia hiyo ulianza kufanyika tangu mwishoni mwa mwaka 2013 hadi sasa ambapo umekamilika na kufanyiwa majaribio yaliyofauli kwa kufanya mikutano kumi ambayo iliunganisha mikoa yote kasoro mitatu ambayo ni mipya ambayo ni, Njombe, Geita na Simiyu.

Kuhusu miondombinu ya mawasiliano amewatoa hofu watumishi kwa kusema: “Mfumo huo ni salama hakuna haja ya kuhofia kuhusu kukatika kwa umeme au hali ya hewa kwani mpango huo unaratibiwa na serikali hivyo ikitokea hali kama hiyo kutakuwepo na umeme wa ziada au kwa kutumia mkongo wa Taifa wa mawasiliano.”
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. NAUNGA MKONO MPANGO HUU MPYA WA SERIKALI YA AWAMU YA TANO.NIWAAMBIE,WAKURUGENZI,MAKATIBU TAWALA WA MIKOA WALISHA IFANYA SERIKALI SHAMBA LA BIBI.WANAPOISHI PERMANENTLY NI DAR-ES-SALAAM.WAMEJIJENGA IWE KIJICHI,TUANGOMA,KISOTA,KAWE,MBEZI,BOKO,BUNJU,KIMARA,UKONGA,CHANIKA,UBUNGO,MWENGE NA KWINGINEKO.VITUO VYAO MIKOANI NI MIRADI YA KUPANUA AU KUKAMILISHA MAHEKALU NA MIRADI YAO.HAWAKAI VITUONI SAFARI "ZA KURUDI NYUMBANI -YAANI DAR" NI ZA KILA SIKU WATAFANYA KIILA AINA YA HILA KUTENGENEZA SEMINA NA WAKONGAMANO.WAKE ZAO,WAUME ZAO,WATOTO WAO,NDUGU ZAO WANATANUA DAR.FUATILIA NAKWAMBIA KWA MFANO HAI. KATIBU TAWALA WA MKOA WA DODOMA MWAKA 2014 KWA MWAKA WA SIKU 365 AMEFANYA KAZI OFISINI [KUWEPO DODOMA MJINI] SIKU NGAPI?ANGALIE ATTENDANCE REGISTER YA MKOA..UKIPATA KAKAA SIKU 100 TUU FANYA SHEREHE.NCHI HII TUMEIBIWA SANA. IMEFILISIWA NA UTAWALA WA AWAMU YA NNE,NI SHIDA,NI SHIDA.TUNAKUOMBA MHE.MAGUFULI HAWA WEZI WOTE WAKUMBANE NA MKONO WA SHERIA.UNDA HARAKA ILE MAHAKAMA.

    ReplyDelete
  2. nakwambia mwaka huu, malafi yatakoma, matumbo yooote yatarudi ndani, safi sana Magufuli.

    ReplyDelete
  3. Hii sasa sifa......... mtatuua njaa jamani.....................
    hahahahahaha amakweli HAPA KAZI TUU.................

    ReplyDelete

Top Post Ad