Madai ya Diamond Kutoka na Kajala Kimapenzi Yapigiliwa Msumari Kwa Picha Hizi za Dada Yake Diamond na Kajala

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

HUKU kukiwa na madai kwamba mwigizaji Kajala Masanja ana uhusiano wa ‘kikubwa’ na Mbongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, mwigizaji huyo amezidi kuyachochea moto madai hayo kwa kutokana na kujiachia mara kwa mara na dada wa Diamond, Queen Darleen, Risasi Mchanganyiko linakujuza.

Kwa mujibu wa chanzo makini, Kajala na Queen Darleen wamekuwa ‘beneti’ kila kona ambapo pia kuna fununu kuwa hata familia ya Diamond imebariki uhusiano wake na Mbongo Fleva huyo na wanampa ushirikiano wa kutosha Kajala.

Mwishoni mwa wiki hii, paparazi wa GPL aliwanasa laivu Kajala na Queen Darleen katika fukwe za White Sands, Mbezi Beach jijini Dar es Salaam walipokuwa wameenda kupunga upepo na kuwapeleka watoto wao kuogelea.

Kuonekana kwa wawili hao kuliibua gumzo la aina yake ambapo wafuatiliaji wa ‘ubuyu’ walionekana kunong’onezana kuwa yale waliyokuwa wakiyasikia na kuyasoma kwenye mitandao kuwa Kajala ana uhusiano na Diamond, yana ukweli.


Itakuwa ni kweli Diamond anamiliki Kajala, juzikati niliona kwenye mitandao, nikajua ni uzushi lakini si kwa ubeneti huu wa leo na Queen Darleen. Si bure, Queen atakuwa anautendea haki ‘uwifi’ wake kwa kumpa kampani Kajala,” alisema mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo.

Ili kukamilisha ubuyu huo, mwanahabari wetu alimuibukia Kajala aliyekuwa ameambatana na mwanaye Paula pamoja na baunsa wake, ili aweze kuzungumzia ukaribu wake huo na Queen ambao umeleta tafsiri kuwa ni mtu na wifi yake. Kajala akafunguka:

Queen (Darleen) ni mtu pekee ninaye muamini, hana maneno ya kuhamisha hamisha, hivyo ametokea kuwa mtu wangu wa karibu na ndiyo maana utaona kwa sasa nipo naye kila sehemu hakuna uwifi hapa. Tumekuja kupunga upepo na kumleta mwanangu kuogelea,” alisema Kajala.

Kwa upande wake, Queen Darleen alisema mwenye macho haambiwi tazama!



Shinda Zawadi ya Gari Kama zawadi ya X-Mass 
Jiandikishe Kwa Kubonyeza Hapa>> Zawadi ya Gari
Washindi Wawili Kutangazwa Tarehe 24 Dec
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad