Breaking News:Rais Magufuli Atumbua Majipu NIDA....Amsimamisha Kazi Mkurugenzi Mkuu na Maofisa Wengine Wanne Kwa Tuhuma za Ubadhirifu wa Fedha

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

1.0           Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA)

1.1 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, ametengua uteuzi waBwana Dickson E. MAIMU, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa kuanzia leo, tarehe 25 Januari, 2016.

1.2 Aidha, baada ya utenguzi huo, Bwana Dickson E. MAIMU amesimamishwa kazi kupisha uchunguzi, pamoja na wafuatao:

1.2.1    Bwana Joseph MAKANI, Mkurugenzi wa TEHAMA

1.2.2.   Bi Rahel MAPANDE, Afisa Ugavi Mkuu

1.2.3    Bi Sabrina NYONI, Mkurugenzi wa Sheria

1.2.4    Bwana George NTALIMA, Afisa usafirishaji

1.3  Taarifa zilizomfikia Rais zinaonesha kuwa NIDA hadi sasa imetumia Sh.179.6 bilioni. Kiasi hiki ni kikubwa na Rais angependa ufanyike uchunguzi na ukaguzi jinsi fedha hizi zilivyotumika, maana Rais amekuwa akipokea malalamiko ya wananchi kuhusiana na kasi ndogo ya utoaji wa Vitambulisho vya Taifa.

1.4 Hivyo, Rais ameelekeza Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) wafanye ukaguzi maalum wa manunuzi yote yaliyofanywa na NIDA.

1.5 Rais pia ameelekeza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali afanye ukaguzi maalum wa hesabu za NIDA, ikiwemo ukaguzi wa “value for money” baada ya kuthibitisha idadi halisi ya vitambulisho vilivyotolewa hadi sasa.

1.6 Rais vile vile ameelekeza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ifanye uchunguzi kujiridhisha kama kulikuwa na vitendo vya rushwa au la.

2.0  Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki na Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa

2.1 Aliyekuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwenye Serikali ya Awamu ya Nne, Mhe. Mahadhi Juma MAALIM ameteuliwa kuwa Balozi wa kwanza wa Tanzania nchini Kuwait, kufuatia uamuzi wa Serikali kufungua Ofisi ya Ubalozi katika nchi hiyo rafiki.

2.2  Rais ameagiza Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki na Ushirikiano wa Kianda na Kimataifa kuwarejesha nyumbani mara moja Mabalozi wawili ambao mikataba yao imeisha. Leo hii Mabalozi hao wanatakiwa kukabidhi kazi kwa Afisa Mkuu au Mwandamizi aliye chini yao. Mabalozi hao ni:

2.2.1    Bi Batilda Salha BURIANI, aliyeko Tokyo, Japan

2. 2.2   Dkt. James Alex MSEKELA, aliyeko Rome, Italia.

2.3 Rais amemrejesha nyumbani Balozi wa Tanzania aliyeko London, Uingereza,Bwana Peter Allan KALLAGHE. Anarejea Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki na Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa atakapopangiwa kazi nyingine.

2.4  Kwa maana hiyo, vituo vya Ubalozi vifuatavyo viko wazi:

2.4.1  London, kufuatia kurejea nchini kwaBalozi Peter A. KALLAGHE

2.4.2    Brussels, kufuatia aliyekuwaBalozi, Dkt. Deodorous KAMALAkuchaguliwa kuwa Mbunge.

2.4.3    Rome, Italia, kufuatia kuisha kwa mkataba wa Dkt. James Alex MSEKELA.

2.4.4    Tokyo, Japan, kufuatia kuisha kwa mkataba wa Bibi Batilda BURIANI

2.4.5    Kuala Lumpar, Malaysia, kufuatia aliyekuwa Balozi, Dkt. Aziz PonrayMLIMA, kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Afrika Mashariki na Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa.

2.4.6    Brasilia, Brazil, kufuatia kustaafu kwa aliyekuwa Balozi, Bwana Francis MALAMBUGI.

3.0   Tawala za Mikoa

3.1 Rais ametengua uteuzi wa Eng. Madeni Juma KIPANDE kabla hajathibitishwa kwenye cheo cha Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi kutokana na utendaji kazi usioridhisha.

4.0       Utumishi wa Umma

3.2  Nachukua nafasi hii kuwahimiza viongozi wote katika Utumishi wa Umma, na watumishi wote wa umma, kubadilika kwa dhati kwenye utendaji wao na uadilifu wao.

3.3 Napenda kusisitiza kuwa Rais na sisi tunaomsaidia hatuoni raha kuchukua hatua dhidi ya viongozi na watumishi wengine. Tungependa kila mtu mwenyewe ajirekebishe na kutomfikisha Rais mahali ambapo inabidi amchukulie hatua. Mambo yafuatayo ni muhimu:

4.2.1 Kila kiongozi na kila mamlaka ya nidhamu isipate kigugumizi kusimamia utendaji na maadili ya kazi.

4.2.2 Kila kiongozi na kila mamlaka ya nidhamu asipate kigugumizi kuchukua hatua za nidhamu, lakini afanye hivyo kwa kuzingatia kwa ukamilifu sheria, kanuni na taratibu katika Utumishi wa Umma.

4.2.3   Lazima uongozi na watumishi wa umma wawahudumie wananchi kwa haki, weledi, uadilifu na heshima. Kwa sababu hiyo:

a)  Kila ofisi ya Serikali iwe na dawati la kusikiliza shida za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.

b) Kwenye kila Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya wajenge uwezo wa kushughulikia shida za wananchi kwa ukamilifu na kwa wakati. Kwa muundo wa Serikali yetu hakuna sababu kwa mwananchi kufunga safari mpaka Ikulu Dar es Salaam kwa kuamini kuwa ni Rais tu anayeweza kumaliza matatizo yake, maana wawakilishi wa Rais wako kila pembe ya nchi yetu. Ikibidi wananchi wafike Ikulu ina maana hao wawakilishi wa Rais hawakutimiza wajibu wao.

c)  Kuanzia sasa watumishi wote wa umma wavae majina yao ili iwe rahisi kwa mwananchi kumtambua anayemhudumia na hivyo kumsifu mtumishi wa umma anayewahudumia kwa weledi, uaminifu na kwa wakati, na kumtolea taarifa yule anayefanya mambo ya hovyo.

d) Kila ofisi ya Serikali iwe na utaratibu wa kupokea maoni ya wananchi kuhusu huduma inayotolewa kwenye ofisi hizo, na kushughulikia haraka maeneo yote ambayo wananchi wataonesha kutoridhika na huduma.

                                                            

Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

Arusha

25 Januari, 2016

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Uyu ndo rais tuliokuwa tunamuitaji miaka yote TZ..sababu serikali ilikuwa inanuka na kuelekea kuoza kwajiri ya baadhi ya mafisadi kwa manufaa yao. Ongera Mh.Dr.Magufuli kura yangu unayo tena mpaka mwisho utakapoamua kuacha siasa sababu ww ni Honestly,unajari na mchapa kazi.

    ReplyDelete
  2. Mh.Magufuli anaonyesha kweli kwamba serikali ilajaa mafisadi na wazembe na kila kitu kinawezekana..Marais awamu ya 1 mpaka 4 lakini muhimbili miaka yote iyo wagonjwa wanalala chini lakini amepata Uraisi ndani ya siku mbili muhimbili vitanda vya wagonjwa vyakutosha kama si uzembe ni nini..Mungu mbariki Dr.magufuli,Mungu ibariki Tanzania ata Vizazi vyetu vije kuwa Proud na nchi yao miaka ya mbele.

    ReplyDelete
  3. hapa kazi hakuna kusinzia hakuna kuchelewa saafi

    ReplyDelete
  4. Safi sana baba na hakika watanaomchukia JPJM ni wale mafisadi na matajiri wenye kuendesha biashara zao bila kufata haki na sheria.Nina imani miaka 5 ijayo TZ itakuwa na ahueni kimaisha.MUNGU IBARIKI TANZANIA,MUNGU MBARIKI RAISI WETU NA MAWAZIRI WAKE.

    ReplyDelete
  5. Fukuza wote na huyu ujerumani

    ReplyDelete
  6. China
    Wote mabalozi wa kisiasa fukuza fukuza
    Tunataka mabalozi wafanya kazi
    Si mabalozi tu hata maafisa WA ubalozini wengi ni migizo tu
    Kuna watanzania kibao ughaibuni ambao wanazijuwa nchi hizo waajirini hawa
    Kwa mikataba

    ReplyDelete
  7. Nenda na benki kuu fukuza wote watoto WA vigogo
    Au wote waingie mikataba mipya wafanye kazi kwa mikataba wote wafanyao kwenye ulaji
    Kwani wengi wao ni watoto , vimada, marafiki wa viongozi wakuu tangu awamu ya kwanza

    ReplyDelete
  8. Wakuu wa wilaya na mikoa wengi migizo
    Bana matumizi
    Kwanini tuwe
    Mkuu WA wilaya
    Katibu tawala
    Mkurugeni wa wilaya
    Msululu WA watu hawa wanini
    Bora meya awe na cheo kama mkuu WA mkoa au wilaya ni Chaguo. La wanainchi

    ReplyDelete

Top Post Ad