Diamond Aombwa Kufanya Kazi na Mume wa Alicia Keyz, Swizz Beatz, Kwenda Marekani Kushoot Video ya Collabo na Ne-Yo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mwaka jana (2015) tulishuhudia producer na rapper Swizz Beatz wa Marekani ambaye ni mume wa muimbaji wa RnB, Alicia Keyz walidhihirisha hadharani kuwa wao ni mashabiki wa kazi za Diamond Platnumz kwa kupost video wakiwa wanasikiliza nyimbo zake (Ingia hapa).

Hiyo ilikuwa ni dalili kwamba kuna siku Swizz Beatz na Diamond wanaweza kuja kufanya kazi endapo itatokea wamekutana. Lakini kabla hata hawajakutana tayari mtayarishaji huyo ameonesha nia ya kutaka kufanya kazi na Simba.

Diamond amesema kuwa Swizz alimtafuta hivi karibuni na kumwambia inabidi wafanye kazi,

“Kuna Collabo na watu wengi sana Kwa mfano kama juzi kati nafikiri, kama siku tatu nyuma hivi Swizz alinicheki akaniambia itabidi tufanye kazi, nikamwambia sawa, na tuko tunaplan,” alisema Diamond kupitia Ayo TV.

Katika maelezo yake Diamond pia ameweka wazi kuwa anampango wa kwenda Marekani kushoot video ya collabo yake na Ne-Yo mwezi wa tatu, na alimwambia Swizz kuwa atakapokwenda kwaajili ya video hiyo ndio anafikiria wafanye kazi pia.

“Nikamwambia mimi nakuja Marekani nafikiri mwezi wa tatu kama sijakosea, au before mwezi wa tatu, kwasababu kushoot video yangu niliyofanya na Neyo, ndio tunaenda kushoot video, nikamwambia nikija ndio itakuwa time nzuri tunafanya hapo hapo”.

Katika collabo hiyo Platnumz amesema pia ana mpango wa kumuomba Alicia Keyz aimbe kiitikio kwenye collabo hiyo na Swizz.

Katika hatua nyingine, Diamond amesema kuwa ana collabo nyingine na msanii wa Marekani ambaye hata hivyo hakupenda kumtaja kwa sasa.

Source;Bongo5

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Pamoja sana Simba dume 100 100

    ReplyDelete
  2. Saafi hakuna kulala hapa kz tuu

    ReplyDelete
  3. Fantastic siyo km wengine kuchekacheka tuu kwenye media

    ReplyDelete
  4. lazima wa nune mwaka huu
    domo wauwee

    ReplyDelete
  5. Awauwe kweli mn mungu anamsubiri,hk kuimb hk kuzini,cc sote njia ni moja mungu atuongoe kwasote

    ReplyDelete
  6. Kaza buti baba Tifa achana na maneno ya kukatishana tamaa, kama wimbo wako wa utanipenda unavyosema kujibu wewe hakuna.Mwenyenzi mungu akulinde sanaaa.

    ReplyDelete

Top Post Ad