Mkoa wa Dar es Salaam Sasa Kuwa na Wilaya Tano

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

RAIS Dk. John Magufuli ameidhinisha kuwepo kwa wilaya tano katika jiji la Dar es Salaam, badala ya tatu zilizokuwepo awali, ili kuleta maendeleo ya haraka hususan katika elimu. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki, alisema jana kuwa, waliwasilisha ombi la ugawaji wa wilaya za Kinondoni na Temeke kwa rais, ambapo ameshaliidhinisha.

“Hatua hii ya kuwepo kwa wilaya tano italiwezesha jiji la Dar es Salaam, kupata maendeleo ya haraka kwa kugawanywa kwa wilaya hizo, ambapo kutakuwa na usimamizi thabiti na hakutakuwa na kisingizio cha kuelemewa kwa majukumu kwa watendaji,”alisema.

Aliomba katika ugawaji wa wilaya hizo, rasilimali zilizopo na mipaka igawanywe kwa manufaa ya wananchi wa wilaya hizo. Aidha, alisema kinachosubiriwa ni ugawaji wa mipaka na kutangazwa rasmi kuongezeka wilaya mbili ya Kigamboni na Ubungo na kufikisha idadi ya wilaya tano katika jiji la Dar es Salaam.

Kutokana na kuongezeka kwa wilaya, Sadiki aliwataka watendaji wake kuwa waadilifu katika ugawaji wa mipaka na rasilimali zilizopo ili kuleta maendeleo yaliyokusudiwa.

Akizungumzia ombi la ugawaji wa wilaya za Kinondoni na Temeke, Sadiki alisema hadi kufi kia jana, ombi hilo lilishaidhinishwa na rais, hivyo Kinondoni itakuwa na wilaya mbili za Kinondoni na Ubongo huku wilaya ya Temeke ikiwa na wilaya za Temeke na Kigamboni.

Source:JPM ARIDHIA WILAYA ZA UBUNGO NA KIGAMBONI | Uhuru

Maswali Muhimu ya kujiuleza kwa yeyote anayeweza kutoa ufafanuzi:
1. Je ni kweli kuongeza wilaya kutaleta maendeleo ya haraka? Vipi kuhusu gharama za uendeshaji zitakazotokana na kuongeza watendaji na kujenga makao makuu ya wilaya?
2. Je ni kweli usimamizi thabiti hautakuwa na kisingizio?
3. Vipi kuhusu mipaka?
4. Vipi kuhusu mabaraza ya Madiwani?

Source;Uhuru
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wameshaanza kupeana ulaji. Njia tu za kulipa maswahiba fadhila, hakuna lolote.

    ReplyDelete

Top Post Ad