Jerry Muro Atoa Mpya ''Simba si Washindani Wetu Tena...Watabaki Kuwa Watani Wetu Kama Wagogo na Wasukuma"

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Klabu ya soka ya Yanga imetangaza rasmi kuwa kuanzia leo wekundu wa Msimbazi Simba si washindani wao tena bali ni watani wa jadi kama walivyo wasukuma na wagogo.

Tamko hilo limetolewa hii leo na mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa wanajangwani hao Jerry Muro wakati akitoa salam za pongezi kwa wachezaji, benchi zima la ufundi na wanachama kwa kufanikisha kile walichokifanya Jumamosi iliyopita kwenye mtanange wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara walipoinyuka 2-0 Simba.

Aidha Muro ameongeza kuwa kwa sasa wanachotazama ni shughuli tatu zilizo mbele yao mechi ya kombe la shirikisho dhidi ya JKT Mlale, mchezo wa klabu bingwa barani Afrika dhidi ya Cercke de Joachim ya Mauritius na mechi dhidi ya Azam ikiwa ni ya ligi kuu Tanzania bara.

Aidha amesema kuwa kikosi cha Yanga kimeanza mazoezi katika uwanja wa chuo cha polisi Kurasini kwa ajili ya mchezo wa kombe la shirikisho dhidi ya JKT Mlale Jumatano na mara baada ya mchezo huo kitaendelea na maandalizi ya mechi ya marudiano dhidi ya Cercle de Joachim.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Jery wee kiboko ya wao,
    Kimya kabla ya mchezo ila ukishinda unatukomeshaje wenzio/
    Haya bwanaaaaaaaaaaaaa!

    ReplyDelete
  2. Wee jery mtoto mdogo tu wacha kuongea pumba waulize wazee simba na yanga ni wapinzani hadi kesho na ni zaidi ya watani na upinzani wacha jeuri

    ReplyDelete
  3. Huyo ndio msema-hovyo wa yeboyebo

    ReplyDelete

Top Post Ad