Hakuna Record Label Ninayoweza Kukubali Inisainishe, Watanipa nini Ambacho Sijafanya! – Diamond Platnumz

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Diamond Platnumz hana mpango wa kuwa chini na record label yoyote duniani. Infact hitmaker huyo amedai kuwa makampuni kibao yamewahi kummendea yakitaka awe chini yake lakini akayapiga kibuti.

“Mimi nimeshaapprochiwa na makampuni mengi sana kutaka kunisaini, mengi sana, mengi hata wanayoyasikia, mengine wanayasikia,” Diamond ameiambia 255 kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM.

“Lakini nafikiria kwamba unapotaka kunisaini mimi unataka kunifanyia nini? Una kitu gani cha kunioffer cha kuona mimi unisaini? Video? Mimi naweza kufanya video zangu hadi za wasanii wangu. Collabo? Collabo mimi naombwa napigiwa simu, msanii wa Marekani wa Tanzania, yeyote nikitaka kufanya chochote naweza kufanya naye,” ameongeza.

“At the end of the day is all about money, nina capital, nina network, ndio maana nikasema kwa nilipofikia sio nibaki mimi tu, niwe na record label yangu. So sifikirii kusainishwa, nafikiria kusaini watu ili kuweza kusaidiana wenyewe kwa wenyewe.”

“Kwa mfano unataka kunisaini, unataka kunifanyia nini? Nikaperform mbinguni? Tuzo zote ambazo mwaafrika anatakani kuziwin.. sijawahi kupata BET na Grammy tu, nataka nipige na Grammy nioneshe kabisa napiga na Grammy. Ukiniambia nasainiwa it doesn’t make sense. Naamini management yangu ni kubwa kuliko mtu yeyote akinisaini, akisema anifanyie promotion hatoweza kufanya promotion ninayoifanya mimi,” amesisitiza.

Diamond aliyeanzisha record label yake, WCB tayari amewasaini Harmonize na Raymond huku kukiwa na uwezekano kuwa amemshamsaini Rich Mavoko.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

15 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kwa hiyo unamkejeli Ali Kiba na wanamuziki wengeni wadogo wanaozitegemea hizo Label au sio. Sasa na wewe na Label yako feki ni kwa nini uwasainishe wanamuziki wengine???? Kwani label yako ina nini cha kuwapa ambacho wao hawana???? Acha madharau bwana mdogo wewe. Kichwa cha chini kimezidi akili kichwa cha juuu. Na madafu dafu yako hayo.

    ReplyDelete
  2. Hahahaaaa kweli wivu ni wivu, mke akibwagwa na mume et mimi njo nimemubwaga, mmume naye ni hivyo. Kwel inauma et hawez saini watamfanyia nini? heb jifunzen kuzungumz fikiria vizur kabl ya kuzungumz. Diamond una kitu gan chakujivunia? ni wasani gan maaruf ulio imba nao? Nigeria SA? kwanz sion muzik unaoimba haitosh wasan wakubw ambao wanasainishwa ten maaruf dunian hata kiat chao ni maarufu kukuzid wamesainishwa et wewe unakil kit gani?unapo sem hivy mbon mimi huk ulaya sijasikiag nyimb yak kweny radio? acha kujisifu wee kubal kam hun level ya kusainishw kwan hujui kuimb, kwawal wenye ujuz wakuimb humo kwan hujui kupang saut vocal hujui. Huwez fany cobcert live hapan hizo huwa munadangany wa Afrika. Nyimb zako ni zamda ila ukiisikia saut ya Kiba kila mtu anakubali nyimbo zak zot hazichuji zinabak pale pale hata kabla ya myaka nenda rudi. Mda si mrefu utapotea na hautasikika ten. Lady J, Kiba, Rosa M,ni wat ambao nyimb zao zitaendelea kusikik myak yote.

    ReplyDelete
  3. Huyu bado ni bwana mdogo ndio kwanza anaanza life hajajua kuwa maisha ni safari ndefu sana yeye anafikiri kuishi the whole life as a musician ni masihara acha kukufuru kwa kuwa sasa hivi hauishi tenda kule Manzese uwanja wa fisi life huwa inabadilika within a second ukashangaa what has hit you down halafu ukashindwa mahala pa kuificha sura yako yaani unaropoka hivyo baada ya kusikia huyo mshindani mwenzako ka-sign mkataba majuzi South Africa povu linakutoka bwana mdogo au na wewe una ile roho ya kwa nini?Mtoaji ni Mungu na sio vinginevyo kumbuka aliyekupa wewe huyo huyo kuna siku anaweza kuja kukupora ukabikia mtupu kama siku ulivyozaliwa na mama yako Snura so always think first before opening your mouth and talk something bwana mdogo

    ReplyDelete
  4. Sio dharma jamaa ajui nini anachikiongea,

    ReplyDelete
  5. mondi mbona povu linakutoka kama umemeza omo,umeulizwa swali ndio lakini ulivyojibu ni kwa jazba na maelezo luluki kama gazeti la uhuru,huu mchezo hautaji hasira mondi take some pill so u can relax,inaonekana kiba anakusumbua sana akili yako,mbona mwenzio amekuombea kura za BET damn!!!!!! mondi be easy.

    ReplyDelete
  6. Hahahaaaa Diamond acha wivu huna loloteee fala wewee!!!!wewe endelea kuhonga mipesa upate mituzo na roho yako mbayaaa umehonga mipesa kibao alikiba asipate tuzo na wala nyimbo zake zisipigwe lakini bado kakufunikaa!!!aibu yako hiyo unalo utajibebaa...huna sauti ya kumfikia alikiba na wala Dovido humfikii hata robo ya pesa aliyonayo na sauti piaa,,,eti sifikirii kusaini na label yeyote mjinga kweli wewe...wanasaini kina Rihanna,Nicki minaj,kina Puff daddy sembuse wewe!!???huna jipyaaa wewe endelea Kurogaa unafikiri Mungu ni wa peke yako poleeee😭😭😭😭😭

    ReplyDelete
  7. Ma super star karibia wote wa Marekani wanasaini Label ili kupata pesa zaidi,sasa wewe unakataa ya kweli hayo maneno usemayo Ama Longo longo tuu!!!????ama kweli waswahili wanasema limbukeni akipata matako hulia mbwataa...Labda waliokufata ni label za mitaani na sio Internationally...tunakucheka kwa dharau na kukuonea huruma maskini weeee....endelea kujitutumua kwa Neyo na kujipendekeza labda unaweza pata na wewe mkataba mnono😁😁😁 endelea kuhangaika na matuzo wenzio wanaangalia pesa tuu na sio kupenda sifa kama wewe tumeshakuchokaa kila siku Drama tuu..mxiuuu Pumbavu...

    ReplyDelete
  8. Usitukane mamba ungali haujavuka mto dharau mbaya kumbuka kuna kupanda na kushuka mbona tunasikia mastaa wakubwa wa muziki huko Marekani wako chini ya label,Acha mipasho hiyo....

    ReplyDelete
  9. kachanganyikiwa huyu na vipesa vyake vya madafu, masikini akipata bwana anajisahau kabisa!

    ReplyDelete
  10. Natamani nimtukane ila nimemuonea huruma badala ya kumtusi. Aisee huyu dogo ni mjinga sana anadhani yeyye dunia keshaimaliza anavyoweweseka yaani hana adabu domo kubwa hata chapati hakunji. MImi ni mzee ila we dogo mwalimu wako kipofu. Namsapoti aliyekuambia kichwa chako cha chini kimezidi cha juu yuko sahihi manake povu linakutoka kama umekula maharagwe mabichi. Unajikweza kwa kipi hasa pambafu mngese

    ReplyDelete
  11. Hahahhahaahahahhahah bwana mdogo kapanic na badooooo tunakutaarifu pia lipstick za wema zimeanza kuingia marekan mtaarifu bibiyo eeeh maana nyie kwa mashauzi na dharau kwa wenzenu mtadhan nyie ni miungu watu...hujui kuimba nani akusainishe sasa hayat maiko jackson alikuwa chin ya sony music na alikuwa legendary itakuwa ww..maiko alikuja kutoka sony siku chache kabla ya kifo chake bt alikuwa chini ya sony who ar yu useme huwezi kusainishwa una nn ww mfyuuuu....unamajibu ya dharau koz huna chochote unatembelea kiki tu na kiki zenyewe tushakuchoka nazo..kwa vokali za kiba utasubiri sanaa

    ReplyDelete
  12. na tomato sorce alisain ya nn. naanza kuamini shule ni muhimu sana.

    ReplyDelete
  13. Wewe Diamond jishughulishe na upandaji wa miti na ugawaji wa maji safi katika eneo lako. Hakikisha mabomba ya maji safi ya kunywa na kupikia yanaewafikia wananchi waliokuzunguka hapo Tegeta sijui Madale sijui wapi. Wewe si mdosi mwenyewe bwana. Sasa jitutumue ili jamii ikuone wa maana kwa kuwafanyia zile project za maana katika maisha yao.

    ReplyDelete
  14. ok diamond bin laden,inabidi uwe makini unapojibu hayo maswali haina haja ya kutengeneza uhasama usio na maana,sishangai wote waliotoa maoni hawajapendezwa na jibu lako,siyo kwamba hawakupendi la asha ni jibu uliotoa linaonyesha una gubu sana kwa mwenzio.

    ReplyDelete
  15. na hizo label zenu sijui za wasafi baby subirin magu aanze kuzilipisha kodi ya maana ndio mtakuwa na heshima hapo mjini na kujua sony ina umuhimu gani,sababu mmezoea kuingiza hela kiujanja ujanja na kuanza dharau kwa label za kimataifa.

    ReplyDelete

Top Post Ad