UKAWA Wadai Rais Magufuli Ndo Chanzo cha Sukari Kuadimika Nchini

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kambi  Rasmi ya Upinzani Bungeni, imesema tatizo la sukari nchini limetokana na uamuzi usio sahihi wa Rais Dk. John Magufuli, kwa kupiga marufuku uingizwaji wa bidhaa hiyo kutoka nje ya nchi bila kufanya tathmini.

Akizungumza jana na waandishi wa habari, Waziri Kivuli wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Anthony Komu, alisema agizo hilo lilitolewa kwa kukurupuka na ndilo lililosababisha sukari kuadimika.

Komu ambaye pia ni Mbunge wa Moshi Vijijini, alisema kama malengo ni kulinda viwanda vya ndani, basi lisifanyike kwa sukari pekee kwa sababu viwanda vipo vingi na bado bidhaa zinaingia kutoka nje nchi.

Alisema kuna harufu ya upendeleo kutokana na Rais kuwa swahiba wa Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, ambaye ni mmiliki wa mashamba ya Mtibwa, hivyo amefanya hivyo kwa kupewa ushauri mbaya huku nchi ikiingia kwenye upungufu mkubwa wa sukari.

Alihoji kwa nini apige marufuku kwenye sukari tu wakati kuna viwanda vya nondo, saruji na vinginevyo na vinaleta bidhaa kutoka nje.

Alisema kilichofanywa na Rais ni kukurupuka na ni kuvunja sheria.

Komu alisema kitendo cha Rais kutoa amri ya walioficha sukari wany’ang’anywe, ni kupora haki za watu na kuua mitaji yao kibiashara.

“Hakuna sheria ambayo inaruhusu kwenda kukagua maghala ya wafanyabiashara na kugawa bidhaa bure, hii hali hata wawekezaji wataogopa kuja kuwekeza nchini kwa sababu wataona mazingira ya hapa nchini ni hatarishi," alisema Komu.

Alisema serikali iandae njia mbadala ya kuwafidia watu walionyang’anywa maana wengine wamekopa kwenye taasisi za kifedha.

“Agizo la Rais lina walakini, kwani ni nani katika biashara za watu...tunakokwenda ni kubaya kwani upungufu wa sukari ulijulikana tangu Februari, lakini akapiga marufuku sukari kutoka nje,” alisema Komu.

Alisema katika tafiti mbalimbali ikiwamo ripoti iliyotolewa na Shirika la BBC, mahitaji ya sukari nchini kwa mwaka ni tani 590,000, lakini uwezo uliopo ni tani 300,000, hivyo serikali ilikuwa ni busara iruhusu kuingizwa kwa sukari kwa sababu viwanda vya ndani vimekosa uwezo.

Alisema Rais anatakiwa kukemewa na kuambiwa kwamba anakwenda kinyume na kwamba wao kambi ya upinzani hawatetei wanaoficha sukari, lakini serikali itafute namna ya kukabili hali hiyo.

Naye Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea, alisema taifa lina viwanda vinne vikubwa vya sukari, lakini bado havina uwezo wa kuzalisha sukari ya kutosha.

Alisema serikali imefanya sukari ionekane kama dawa za kulevya kutokana na kuadimika huko.

Alisema sukari hadi iletwe nchini, ni takriban wiki tano na wanaoingia kwenye Mwezi Mtukufu wa Ramadhani watahitaji sukari kushinda vitu vingine.

“Sisi hatutetei walioficha, lakini wamenunua ili kuuza kwa taratibu kulingana na bei ya soko wasibughudhiwe maana kuna hatari ya benki kushindwa kurejeshewa fedha zilizokopwa,” alisema Kubenea.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hawa Ukawa wangeachiwa nchi ingekula kwao hivi sukari imeadimika au imefichwa kwa makusudi kama sukari hakuna na hayo matani yanayokamatwa yametoka mbinguni Ukawa achane kuwahadaa watu Mungu Bariki msisishike nchi mtatuua na nja miaka 54 ya dhiki yatosha wacheni Ngosha ajenge nchi mlizoea vibaya

    ReplyDelete
  2. kitendo cha u dictator kabisa kuwanyanganya sukari wafanyabiashara tunaenda pabaya baadae ndio mtajua nchi inapelekwa kwa mabavu hakuna sheria ya kutaifisha sukari, kila mtu anafanya biashara kutegemea faida km ilihifadhiwa kwa maslahi yao hakuna shida

    ReplyDelete
  3. Mkapa alokuwa Ni mfanyakazi WA Umma aliweza vipi kumiliki Ardhi ikiwa aliyetutoa kwa mkoloni hakuwe kumiliki na Mwinyi miogopa mingu PIA Hana ma JPJM sidjani kama atachukua au bata kufikieia..Mkapa itanidi tumuangalie trtesi zipo Lushoyo na ikibainika hatua viille vile tutamchukulia hatutomdhulumu laki iadilifu na haki itapita..heshima alipewa alipohitajika...na sasa Ni mwananchi kama mwi gine yeyote..ana viwanfa au amewekeza...Hii Ni Tanzania mpya..kulimfana ndikp kulipo tupoteza...

    ReplyDelete

Top Post Ad