Wabunge wa Upinzani wametoka nje ya bunge kuonyesha kutokuwa na imani na Naibu Spika Tulia Ackson

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Wabunge wa vyama vya upinzani leo wametoka nje kwa mara nyingine kupinga Naibu Spika Dk. Tulia Acksonkuendesha vikao vya Bunge na kumwachia Bunge yeye na wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).


Taarifa kutoka Bungeni zinaeleza kuwa, wabunge wote wa upinzani wametoka nje kususia kikao cha Bunge ikiwa ni kutekeleza azimio lao la kutokuwa na imani na Dk Tulia.


Baada tu ya kusomwa dua ya kufungua Bunge asubuhi wabunge hao wametoka nje na kumwacha Dk. Tulia akiwa na wabunge wa CCM pekee.


Hata hivyo Dk. Tulia ameanza kupaniwa na wapinzani tangu jana. Ni kwa madai kuwa wapinzani hawamwamini tena.


Wameeleza kuwa, namna anavyoliongoza Bunge, kauli zake na kuyumba kwake katika kusimamia haki kwa wabunge wa Ukawa na wale wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kumechochea kuonekana kuwa, nafasi aliyonayo haimstahili.


Kutokana na hali hiyo, Freeman Mbowe ambaye ni Kiongozi Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni jana aliahidi kuanzisha mgomo dhidi ya Dk. Tulia.


Mbowe aliwaambia hayo wabunge wenzake mjini Dodoma kwenye kikao cha dharura alichoitisha na kushirikisha waandishi wa habari.


Alisema, Dk. Tulia ndio tatizo kuu la Bunge la Kumi na Moja na kwamba, kiongozi huyo wa Bunge kila anapokuwa kwenye kiti na kuongoza Bunge, mtafaruku hutokea.


“Nitapendekeza kuwa kila kikao cha Bunge kinachoongozwa na Tulia Ackson, sote tutoke nje ili kuonesha kwamba hatuna imani naye katika kuendesha shuguli za bunge,” Mbowe alisema jana.


Utekelezwaji wa kauli ya Mbowe umeanza leo ambapo sasa Dk. Tulia amebaki na wabunge wa CCM pekee.


----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Haya sasa anasemaje juu ya hili nalo!! wale wapambe wa matusi njooni mtukane... rasimu imerudi tena, kila kitu ndiyo mzeee....
    ha ha ha ha haaaaa uwiiiii

    ReplyDelete
  2. Mbowe... Nilikuwa nakuona kuwa wewe labda umewiva kisiasa na lakini kumbe siyo... Kama unavyo jiita kinogozi wa upinzani inaelekea kuwa hujali Uzalendo.. na unataka kuthibitisha na kuanzisha mambo ambayo hatima yake yatagawa kusini na kaskazini,, Ninacho kwambia ni undoa chuki katika moyo na ufikirie kidogo halafu jibu utalipata... wewe si mtoa posho kwa hao unaowashawishi ni sisi walipaji kodi.. sasa usiwatie wenzako njaa manake nje kumenuka... Kua kisiasa ukitaka kuwa mwanasiasa...Nadhani unanielewa toka enzi za kina choggy slai.. Usibahatishe wala usijidanganye na kudanganya...Lawama zako na chuki zako hazina mashiko na usiwapoteze wenzako kwa ushawishi usio na faida.. Kuwa mzalendo na mwenye kujikisia na mwelewa...

    ReplyDelete
  3. Mbowe... Nilikuwa nakuona kuwa wewe labda umewiva kisiasa na lakini kumbe siyo... Kama unavyo jiita kinogozi wa upinzani inaelekea kuwa hujali Uzalendo.. na unataka kuthibitisha na kuanzisha mambo ambayo hatima yake yatagawa kusini na kaskazini,, Ninacho kwambia ni undoa chuki katika moyo na ufikirie kidogo halafu jibu utalipata... wewe si mtoa posho kwa hao unaowashawishi ni sisi walipaji kodi.. sasa usiwatie wenzako njaa manake nje kumenuka... Kua kisiasa ukitaka kuwa mwanasiasa...Nadhani unanielewa toka enzi za kina choggy slai.. Usibahatishe wala usijidanganye na kudanganya...Lawama zako na chuki zako hazina mashiko na usiwapoteze wenzako kwa ushawishi usio na faida.. Kuwa mzalendo na mwenye kujikisia na mwelewa...

    ReplyDelete
  4. Mbowe... Nilikuwa nakuona kuwa wewe labda umewiva kisiasa na lakini kumbe siyo... Kama unavyo jiita kinogozi wa upinzani inaelekea kuwa hujali Uzalendo.. na unataka kuthibitisha na kuanzisha mambo ambayo hatima yake yatagawa kusini na kaskazini,, Ninacho kwambia ni undoa chuki katika moyo na ufikirie kidogo halafu jibu utalipata... wewe si mtoa posho kwa hao unaowashawishi ni sisi walipaji kodi.. sasa usiwatie wenzako njaa manake nje kumenuka... Kua kisiasa ukitaka kuwa mwanasiasa...Nadhani unanielewa toka enzi za kina choggy slai.. Usibahatishe wala usijidanganye na kudanganya...Lawama zako na chuki zako hazina mashiko na usiwapoteze wenzako kwa ushawishi usio na faida.. Kuwa mzalendo na mwenye kujikisia na mwelewa...ikiwa una utashi wenye Malengo ya uharibifu itabidi ungoje hiyo miaka ya baadae manake sisi tumeshawashitukia na mayaunyau yetu ya sera mbovu ( kwa hisia yangu) na kizuri hakijapata kuwa kizuri kwenu siku zote mnatafuta cha kuleta mabishano. Je wewe huoni kwamba ukishawishi hao uliotoka nao nje ni kwamba mnatulia wakati na posho bila kuwajibika... Naomba Bunge letu tukufu lipitishe Sheria ya asiye hudhuria na posho inakatwa hapo mtanyooka wana sokomoko na sikendo... MBOWE Hivyo Jina lako kamili ni nani? Umuri wako katika Game ni miaka mingapi?.. Na wazifa wako ni NINI?... naomba unieleweshe.NANGOJA MAJIBU... Na hao waliotoka ni lazima watafakari wao wako hapo kwa matakwa ya nini.. Mbowe au Wanachi ili kuleta maendeleo...Au wameitwa na Mbowe Dodoma kwenye pati ya NYAMA CHOMA CLUB 84???? WABUNGE MJIHESHIMU NA MUWAJIKE REGARLESS WHO IS CHAIRING WHAT... UZALENDO UWE MBELE NA MASILAHI YA NCHI NA SIYO KUSIKILIZA MBOWE WALA TOWEE!!!

    ReplyDelete
  5. Mbowe... Nilikuwa nakuona kuwa wewe labda umewiva kisiasa na lakini kumbe siyo... Kama unavyo jiita kinogozi wa upinzani inaelekea kuwa hujali Uzalendo.. na unataka kuthibitisha na kuanzisha mambo ambayo hatima yake yatagawa kusini na kaskazini,, Ninacho kwambia ni undoa chuki katika moyo na ufikirie kidogo halafu jibu utalipata... wewe si mtoa posho kwa hao unaowashawishi ni sisi walipaji kodi.. sasa usiwatie wenzako njaa manake nje kumenuka... Kua kisiasa ukitaka kuwa mwanasiasa...Nadhani unanielewa toka enzi za kina choggy slai.. Usibahatishe wala usijidanganye na kudanganya...Lawama zako na chuki zako hazina mashiko na usiwapoteze wenzako kwa ushawishi usio na faida.. Kuwa mzalendo na mwenye kujikisia na mwelewa...ikiwa una utashi wenye Malengo ya uharibifu itabidi ungoje hiyo miaka ya baadae manake sisi tumeshawashitukia na mayaunyau yetu ya sera mbovu ( kwa hisia yangu) na kizuri hakijapata kuwa kizuri kwenu siku zote mnatafuta cha kuleta mabishano. Je wewe huoni kwamba ukishawishi hao uliotoka nao nje ni kwamba mnatulia wakati na posho bila kuwajibika... Naomba Bunge letu tukufu lipitishe Sheria ya asiye hudhuria na posho inakatwa hapo mtanyooka wana sokomoko na sikendo... MBOWE Hivyo Jina lako kamili ni nani? Umuri wako katika Game ni miaka mingapi?.. Na wazifa wako ni NINI?... naomba unieleweshe.NANGOJA MAJIBU... Na hao waliotoka ni lazima watafakari wao wako hapo kwa matakwa ya nini.. Mbowe au Wanachi ili kuleta maendeleo...Au wameitwa na Mbowe Dodoma kwenye pati ya NYAMA CHOMA CLUB 84???? WABUNGE MJIHESHIMU NA MUWAJIKE REGARLESS WHO IS CHAIRING WHAT... UZALENDO UWE MBELE NA MASILAHI YA NCHI NA SIYO KUSIKILIZA MBOWE WALA TOWEE!!!

    ReplyDelete
  6. Huyu dada nilishaona tangu mwanzo naona anavyotumia uongozi wake, lakini kutokana na hali ilivyo siamini sana kama maamuzi yake kweli ni yake yeye binafsi, naamini ya kwamba maamuzi yake niyakichama zaidi kuliko uzalendo, kwani kuna mambo mengi yamefanyika na yanendelea kufanyika kukilinda chama zaidi kuliko huo uzalendo tunaouzungumzia. Kwa hiyo tunaweza kusumbuka na mtu mmoja lakini kumbe tatizo ni mfumo. Suala la mfumo ndio lakuangaliwa zaidi.

    ReplyDelete
  7. Kimsingi hawa wapinzani tumewachoka sana na tena sana. Hatuwataki, hatuwataki, hatuwataki. Wanatutia kichefuchefu sana. Hawana mambo yoyote ya maana katika vichwa vyao zaidi ya kutuletea fujo. Kwa kweli tumewachokaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

    ReplyDelete

Top Post Ad