Wolper Afungukia Penzi Lake na Harmonize, Adai Hakujua kama ‘Mkongo’ Ana Mke

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mwigizaji Jackline Wolper jana amefanya mahojiano na Zamaradi Mketema kwenye kipindi cha TakeOne na kuzungumzia mambo mengi kuhusu yeye na aliyekuwa mpenzi wake Putin ‘Mkongo’ aliyemvisha pete, na uhusiano wake na msanii Harmonize.


‘Ni kweli Raj (Harmonize) ni mpenzi wangu,ukweli nilimjua siku nyingi nilikuwa nikimchukulia kama mwanamuziki tu, tuna mwezi mmoja na wiki mbili sasa’’ alisema Jack.

’Nisingependa kumuongelea mwanaume niliyekuwa naye ‘Putin’, nikiona picha zake,nikisikia jina lake yaani kuna vitu nikiviona kuhusu yeye naumia sana , na mimi nikimpenda mwanaume nampenda kutoka moyoni, nilijuana naye mwaka 2012 nilikuwa namzungusha kwasababu watu walikuwa wakiniambia kabila lao ni waongo, sasa kipindi alivyorudi hapa nchini alinikuta nipo singo, nilikuwa sipo sawa’’

‘’Katika maisha yangu sijawahi kumpeleka mwanaume kwa wazazi wangu nilimuamini nikampeleka kwetu na unajua mwanaume yeyote unayempeleka kwenu hutokubali kuachana naye kwasababu utakuwa unawaangusha wazazi wako na familia yako na ikiwa wamempokea vizuri lakini kwanini nimekubali kumuacha’’(analia)

‘’Ni kweli alikuwa mume wa mtu, baadhi ya watu walikuwa wakiniambia na kunitumia picha siku ambayo alinivisha pete, n asiku ambayo alinivisha pete nilikuwa sijui ilikuwa ni sehemu ambayo tulikuwa tunapenda kukaa na kunywa kila siku ananivisha pete nikakubali baada ya kunivalisha watu wakawa wananiambia kwanini nimevishwa pete na mume wa mtu sikutaka kumuamini mtu kwa sababu mahusiano yangu mengi yamekuwa yakiharibika kwa sababu kuwasikiliza watu, niliziona picha za harusi lakini nilihisi ni harusi tu, sikuelewa kwa sababu nilikuwa kwenye mapenzi’’

‘’Putin alikuwa akinidanganya kuhusiana na mke wake na niliamini ndoa nyingi watu wanaoana na kuachana na aliniambia ni kweli alikua na mwanamke lakini waliachana, lakini mwanamke aliyekuwa naye ni tofauti na watu walivyokuwa wakiambia yeye aliniambia kuwa hawajaoana na mwanamke huyo ila walitaka kufunga ndoa, kiukweli ni mtu ambaye anaweza sana kujielezea alinidanganya sana, nilimuamini sana kuliko wale watu zaidi ya kumi waliokuwa wakinieleza ukweli kuhusu yeye sikuwaamini, na wale waliokuwa wananiambia ukweli hawakuwa wabaya lakini sikuwaelewa kwa sababu nilikuwa kwenye mapenzi tayari’’ (analia).

‘’Nilitoka naye hapa tukaenda South Afrika(analia) tulienda kwa ajili ya kusoma nakumbuka ilikuwa mwezi wa 12 mwaka jana akaniambia ameshalipa kila kitu na ameninulia gari ya kuendea shule,nikakaa miezi mitatu sikusoma lakini wazazi wangu walikuwa wanajua nasoma ilikuwa ni lazima nimsitiri mchumba wangu kwa wazazi wangu nikawadanganya kuwa nasoma, mama yangu alikuwa anampenda sana mchumba wangu lakini baba yangu hakukubaliana na naye, alikuwa akisema kuwa kama atanichukua kunipeleka South Afrika basi akamilishe ishu ya kunivisha pete na kunioa kabisa, akanivisha pete mbele ya wazazi wangu wakakubaliana baada ya mwezi wangeleta mahali ’’ alisema  Jack.

‘’Tulivyofika South Afrika nilikuwa namfanyia kila kitu kama mke wa mtu, nilikuwa namdanganya mama nasoma lakini baada ya hapo nikaona mambo hayaendi kwa sababu kuna siku nilienda salun nikasikia kuwa mke wake naye yupo kule Sauz na alikuwa ananiaga sana anasafiri anaweza akakaa siku mbili au tatu nikamuuliza akaniambia sio kweli yupo Kongo’’ alisema Jack.

‘’Siku iliyofuata alikuja nyumbani akiwa amechelewa, nilikuwa chumbani yeye alikuwa sebuleni ana’preview’ picha nikataka kumpora simu nikamwambia nimeona picha ukiwa na mke wako, na mtoto wako, akaniambia alimkuta mwanamke wake kwa kaka yake akataka kupiga picha naye ndo akapiga, halafu alikuwa anavaa pete ya ndoa nikamwambia siitaki hiyo pete akaiuza, lakini kuna siku alirudi akiwa ameivaa ile pete nikakasirika nikamwambia naondoka akanitupia ile pete kitandani akaniambia nikaitupe chooni’’ alisema Jack.

‘’Kuna kipindi nilikuwa nalewa sana kutokana na stress, kuna siku nilikuwa ‘location’ nilikuwa nimelewa hadi nikazima akapigiwa simu akanifuata akanipeleka nyumbani akanivua nguo zote akaanza kunirekodi na kunipiga picha, lakini nilifanikiwa kuzifuta, lakini baada ya wiki mbili alinitumia meseji na kunitisha kuwa kitu atakachonifanya watanzania watafunga macho na sitoamini’’ Alimalizia Jack

Cloudsfm
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. so wewe wolipa kutembea na bosi haikutosha umeamua kutembea na hause boy wa bosi wako,. halafu ujui kuchagua huyo ni mdogo na hakufai unajichelewesha kuolewa wewe,,, umempendea nini naye huyo musukule tu huyo!mnaboa sana!

    ReplyDelete
  2. Sasa hilo lijimwanamke lizeee likubwa lizima lijibibi halina hata aibu kwenda kutembea na hako katoto duh kwa kweli kama ni mapenzi basi ngoja mimi nikalale salaaleeee duh aiseee!!!

    ReplyDelete
  3. Na nyie wabongo, au mnaojita mastaa, mkiona wageni kazi kupapatikia, kwanza wacongo si dhani kama watu wazuri asilimia kubwa, angalau si wote labda,pengine hata sisi watanzania tuko afadhali zaidi kuliko wacongo, kwanza mnaaibisha. Watanzania wote, manaake huko kwao sifa watakazotoa, matoto ya Tanzania ni malaya sana, makahaba, hawafai hata kuwa wake wa kuoa, zaidi zaidi ni kupiga chini na kutmka, kama kuoa ni nyumbani kwetu congo, hivyo ndivyo watakavyojisifu na kuwatumia vibaya wanawake wa Tanzania kama hamjieshimu, sio kila mwanaume anaekutamkia anakupenda anakupenda nawe wamini, mmmh wengine wataka onja hiyo mitumbua ya wanawake wa kibongo basi

    ReplyDelete
  4. Ukupaswa pia kuwa na haraka cha kutafuta bwana mpya ungetuli kidogo ungemuomba mungu kwanza hasira ikiisha uwenda ungefanikiwa kupata yule uliyekua unamuhitaji Mara haraka uwa aisaidiii kitu

    ReplyDelete
  5. KAMA NI HIVYO HARAKA YA NINI? NA HUYO MTOTO HAMUENDANI HATA KIDOGO DADA!!!KHA!!

    ReplyDelete
  6. Ndio kuruka mkojo kukanyaga mavi?Pole wee.

    ReplyDelete
  7. Wolper nahisi ulifanya kukurupuka kuwa na Harmonize hata kama Putin alikuumiza kipindi mlichoachana na wewe kuanza mahusiano mapya tena kwa fujo zote kwenye mitandao ya jamii huoni kuwa unawaaibisha hata wazazi wako waliokushuhudia ukivalishwa pete hata miezi sita haijaisha leo baba yako anakuona unaliwa denda na mwanaume mwingine tena live kabisa hadharani.

    Hukatazwi kuwa kwenye mahusiano but best way kama mtu umebreak relationship na mtu basi jipe muda ujitathmini na hasira na uchungu vipoe then ndio uanzishe uhusiano mpya. Huyo Harmonize anaweza kuwa anakutumia tu na sio real love na nikwasababu anajua uko kwenye maumivu ya kutendwa so atajidai anakupenda lakini anachikihitaji kwako akishakipata atakuumiza zaidi ya Putin. Pole sana dada but next time mahusiano yakiaribika keep low profile jipe muda wa kujitibu vidonda na maumivu kabla ya kuanzisha mahusiano mapya.

    ReplyDelete
  8. Mmh! Kwa jinsi huyo jamaa alivyokudanganya na wewe ukadanganyika, nina wasiwasi na afya yake....... hivi mliwahi hata kupima??

    ReplyDelete

Top Post Ad