Mh. Magufuli, Nchi inaongozwa Kwa Katiba na Sio Ilani ya CCM....

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kwa heshima na Taadhima napenda kumkumbusha Rais Magufuli kuwa, nchi yoyote duniani inaongozwa kwa Katiba ya nchi husika, na sio Ilani ya Chama. Ilani ya Chama hutumika tu kuomba ridhaa ya wananchi (kura), ili Chama husika kipate kupewa Mamlaka ya kuongoza nchi, chini ya Katiba.

Kuzuia vyama vya Siasa hasa vya Upinzani kuendesha shughuli zake za kisiasa, kwa kisingizio cha kukwamisha ahadi za Ilani ya Chama Chako CCM, ni hatua hatari sana ya kutokufuata Katiba ya nchi, ambayo ndio sheria mama inayoongoza nchi.

Kumbuka Ilani ya CCM haiwezi kuwa mbadala wa Katiba ya Nchi. Na madikteta wote duniani hupuuza Katiba.

Nakuomba na Kukusihi kwa jina la Mwenyezi Mungu, uongeze nchi kwa mujibu wa Katiba, ili usije ukaingia kwenye kumbukumbu za madikteta wa Dunia.

Nawasilisha.
By Tajirijasiri/JF
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kweli shule Na elimu Ni vitu vya maana . Wewe mdau uliekosa uelewa Na masikii ya kusikia..mtukufi Raisi aliyoyasema yanaeleweka Na usitie dosari yako ya upoteshaji kwa kuchanganya mada ya katiba na ilani..katiba Ni katiba Na ilani Ni sera za kuombea Kura..sasa wewe hata sijui nikuitaje jina unalostahiki..sema nakupa pole

    ReplyDelete
  2. mwandishi wa mada hujamwelewa kabisa mheshimiwa Rais, rudia kwa makini kusikiliza alichosema usichanganye habari kwa kujisingizia. pole.

    ReplyDelete
  3. Mi Nimeelewa, Rais si alisema uchaguzi umeisha tungoje 2020?? Anawaona wanaofanya mikutano ya kisiasa ni maadui na pia wanamkwamisha kutekeleza majukumu yake japo sielewi wanamkwamisha kwa njia zipi!

    Afanye kazi yake kwa mujibu wa katiba na aache vyama vifanye siasa. yeye ndio atafanya tena siasa 2020 maana kwa sasa anawajibika kuleta maendeleo (kutekeleza ahadi zake)

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nyumbu hata ukimkataza kuruka ndiyo kwanza ataruka.. yaani siku zote anakuwa ni kunyume na uealewa... Sasa sijui nikufananishe au???

      Delete
    2. Wewe Unaejisema umeelewa uko hivi... je hao waliondika wakoje??
      Jamani ndugu zangu shule zilikupigeni Chenga? ikiwa mtu mmemuona na kumsikia na bado mnashindwa kumuelewa na ukajiita Umemwelewa nahpo itabidi tukupe nasiha ya kwenda kumuona Dakitari ili aweze kuchunguza afya yako... si kitu kibaya kujijua... Hapa Kazi Tu

      Delete
    3. Wewe Unaejisema umeelewa uko hivi... je hao waliondika wakoje??
      Jamani ndugu zangu shule zilikupigeni Chenga? ikiwa mtu mmemuona na kumsikia na bado mnashindwa kumuelewa na ukajiita Umemwelewa nahpo itabidi tukupe nasiha ya kwenda kumuona Dakitari ili aweze kuchunguza afya yako... si kitu kibaya kujijua... Hapa Kazi Tu

      Delete
  4. Wanajitahidi sana UKAWA na bora wafanye ziara ya kuzunguka Dunia kuieleza kama serikali ya Tanzania inawaonea, ni ya kidikteta, inavunja haki za binadamu, wakaseme lolote na chochote watakachojisikia kushitaki ukweli hata huko nje hakuna mpuuzi kama wao atakayewaunga mkono
    Na mbona wanasahau kwenda ICC huko wangefanikiwa labda kwa kupata BUNGE LIVE maana huu upuuzi wao wote ulianza na madai ya BUNGE LIVE
    CCM kaza buti na 2020 watalia kilio cha,,,,

    ReplyDelete
  5. We cjui mwandishi ukapimwe akili. Usiandike mambo ya kupotosha umma Haya ndo mambo yakukemewa uhuru wa kuropoka usiokuwa na mipaka. Jitu linakurupuka kwenye usingizi anaandika aliyokuwa anadanganyana na hawara yake.tumechoka mwacheni mtukufu rais afanye kazi yake. Subirini kampeni 2020. Waambie na hao wanaokupa vijisent vya kujikimu na familia yako. Awe anaendesha nchi kwa ilani ya ccm au ukawa ni sawa tu cc tumeridhika. Waliokuwa wanaendesha nchi Kwa Hiyo katiba imetufikisha Wapi? Ufisadi mpaka kwenye kujisaidia. Usinitake nikatunana nikafungwa bure. Anayemsema rais wetu vibaya ni fisadi au mtoto wa fisadi. Nakuombea rais magufuli maisha marefu yenye baraka yani usiugue ata cku moja ili mifisadi isipate nafasi. Mungu mlinde Magufuli wetu.

    ReplyDelete

Top Post Ad