UKAWA Wamgomea Rais Magufuli, Wamtaka Aandae Magereza za Kutosha

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mwenyekiti wa Chadema na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe amesema hawatakubaliana na kauli ya Rais John Magufuli ya kukataza mikutano ya shughuli za siasa hadi mwaka 2020 na kama hivyo ndivyo, Serikali iandae magereza ya kutosha.

Mbowe ambaye pia ni mwenyekiti mwenza wa Ukawa, alisema jana kuwa kutokana na kauli hiyo kuwa nzito vyama vinavyounda umoja huo vitakutana na kujadiliana kabla ya kutoa msimamo wa pamoja.

Mbunge huyo wa Hai alisema wamepokea kwa mshtuko mkubwa kauli na maagizo ya Rais Magufuli kuhusiana na haki ya kufanya shughuli za kisiasa ikiwamo mikutano ya hadhara, makongamano na hata maandamano kwa vyama vya siasa.

“Aandae magereza ya kutosha kwa sababu hatutazibwa midomo... kama wananchi wananyimwa fursa ya kusema ni vibaya, watatumia vitendo mambo ambayo yalileta vita katika nchi za wenzetu. 

"Mbowe alisema Rais Magufuli anastahili kujua siasa siyo starehe, bali ni kazi kama zilivyo nyingine zozote. Alisema siasa siyo tukio la uchaguzi, bali ni maisha ya kila siku na ni mfumo unaogusa maisha ya kila siku.

 “Uhalali wa kazi za siasa unatolewa na Katiba aliyoapa kuilinda na kukaziwa na Sheria Namba 5 ya mwaka 1992 (Political Parties Act NO. 5 of 1992) pamoja na marekebisho yake,” alisema. 

Alisema uhalali huo ndiyo unaomfanya yeye kuwa Rais leo na ndiyo unaotoa uhalali wa chama chake kuwepo na kutekeleza kihalali na kisheria majukumu yake ya kila siku.

Alisema haki ya kufanya siasa haiwezi kuwa miliki ya Serikali, wabunge na madiwani pekee kama Rais anavyoagiza.

 “Akumbuke uchaguzi mkuu siyo tukio pekee la kisiasa. Kuna chaguzi za serikali za mitaa, chaguzi za marudio na mambo mengine mengi. Ni wajibu wa msingi wa vyama vya siasa kufuatilia utendaji kazi wa kila siku kwa wale wanaoongoza Serikali na hivyo siasa siyo uchaguzi pekee,” alisema Mbowe. 

Alisema elimu ya uraia na ile ya siasa ni wajibu mkuu wa vyama vya siasa na hustahili kutolewa wakati wote na siyo na wanasiasa wa kuchaguliwa au kuteuliwa pekee.

“(Rais Magufuli) anapaswa kubaini kuwa vyama vya siasa vina miundo ya viongozi na watendaji nchi nzima ambao majukumu yao ni ya muda wote na siyo ya msimu wa uchaguzi pekee,” alisema. 

Alisema makongamano yakiwamo ya siasa anayolalamikia Rais ni pamoja na Kigoda cha Mwalimu J.K. Nyerere ambalo lilionekana kuhoji mambo kadhaa yanayogusa mustakabali wa nchi.

“Makongamano katika vyuo na taasisi mbalimbali ni sehemu muhimu ya taaluma na huibua uelewa muhimu kwa jamii,” alisema. 

Alisema makongamano mengi huandaliwa na taasisi zisizo za kiserikali na taasisi za dini na kusema Rais anastahili kutambua kuwa siasa inamgusa kila mmoja kwani ni maisha ya watu.

Mbowe alisema; “walianza kwa kulithibiti Bunge na wabunge wa upinzani kwa kujaza askari bungeni kama vile ni uwanja wa vita. Leo ni vyama vya siasa vya upinzani kupewa likizo ya lazima ya Rais; kesho inaweza ikawa taasisi za dini, baadaye asasi zisizokuwa za kiserikali na hatimaye nchi hii itaweza kugeuka nchi ya utawala wa mabavu ya kutumia dola,” alisema na kuongeza:

“Ukawa hatutakubaliana na hali hii. Hili ni tamko la hatari kwa demokrasia, utawala wa sheria, haki za binadamu na linakinzana na kila aina ya uhuru ambao Katiba yetu aliyoapa kuilinda Rais, imetoa.” 

Aliwataka Watanzania wote wakatae utamaduni huu mpya ambao alisema utabomoa mshikamano wetu kama Taifa.

Mbowe alisema Rais kuwa mkali katika kusimamia uwajibikaji na utendaji wa Serikali ni jambo jema lakini linapoteza maana kama ukali huo unatumika kuvunja Katiba na sheria na kuziba watu midomo.

“Uhuru ni jambo la kupigania na kutetea kwa gharama yoyote ile na tuko tayari kwa wajibu huo. Wanaoweza kumshauri Rais na wafanye hivyo kwani athari za jambo hili likiachiwa likaota mizizi, hata hayo maendeleo anayoyapigania yanaweza kubaki kuwa ndoto na nchi kuingizwa kwenye machafuko yasiyo ya lazima,” alisema. 

James Mbatia 
Msimamo kama huo pia ulitolewa na Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa, James Mbatia aliyesema Rais ameweka kando Katiba.

Mbatia ambaye pia ni Mbunge wa Vunjo (NCCR- Mageuzi), alisema kauli nyingi ambazo zimekuwa zikitolewa na Rais zimekuwa hazizai matunda na kutoa mfano wa kuzuia sukari kutoka nje ya nchi kuingia nchini jambo ambalo muda mfupi baadaye, ilibainika kuwa sukari ya nchini haitoshelezi mahitaji.

“Hatuombi ruhusa kwa Rais kufanya mikutano ya kisiasa, bali ni haki yetu kikatiba,” alisema.

Mbunge wa Viti Maalumu (CUF), Riziki Ng’wale, alisema kauli ya Rais Magufuli si sahihi kwa sababu siasa ni kazi na hakuna namna anavyoweza kuweka wigo wa kuyafanya mambo hayo.

“Kwa sisi wakongwe wa siasa tunamwambia apanue magereza, hatutakubali hilo... Aache ubabe,” alisema. 

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanataaluma wa Vyuo Vikuu na Vyuo Vikuu Vishiriki vya Umma nchini, (ASA), Paul Louslie alisema agizo la Rais Magufuli ni gumu kutekelezeka hata ndani ya CCM.

 “Kukaa bila kukutana kwa vyama vya siasa hata ndani ya CCM labda kwa sababu yeye ni Mwenyekiti wa CCM na ni Amiri Jeshi Mkuu. Na hapo akiamua kutumia madaraka yake hatatenda haki kwa vyama vingine vya kisiasa,” alisema. 

Alisema kazi ya siasa ni kukutana na watu na haiwezekani kukaa ndani bila kukutana na watu kwa muda wote kwani huko ni kuua chama.

----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

13 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Baada ya Kuisoma na Kuitafakari hii makala hapo Juu.. Inadhihirisha na inabainisha Ufinyu wa Uelewa alicho kizungumza Mtukufu Raisi Dkt JPJM.. Maudhui na mwelekeo wa wazungumzaji ni utashi wa kutuonesha kuwa wao Hawakubali. Hawakubali nini Hawakujui baada wa kuchanganya Madaa zilizokuwepo na zisizo kuwepo... Na ni tofauti kabisa na Mazungumzo ya Raisi wetu.

    Hii inaonesha Mioyo yao na Fikra zao Na Akili zao na Mwelekeo wao. Ni kutaka Kupotosha Mantiki ya Mazungumzo/ Hotuba ili ilete mfarakano wa Uelewa na Kupotosha wananchi... Siasa Haijakatazwa na Wala haitakatazwa Cha msingi ni Wakati Gani wa Hiyo siasa na kwa mwelekeo upi??

    Wanadhihirisha Ufinyu wa Uelewa! Huu ni wakati wa kutekeleza kile kilicho kufanya Ukachaguliwa na Sio Lele mama za Siasa.. Wakati ukifika Milango ya kumwaga sera zenu utafunguliwa na Mtamwaga sera upya huku mkiwa mmziboresha na Wananchi watakufanyieni tathmini kama wawapeni au wawatolee njee baada ya kuona Vioja vyenu na Kutotoa ushirikiano wakati mlipo Hitajika kufanya hivyo huku mlikabidhiwa Dhamana na wapiga Kura wenu.
    Tanzania ni yetu sisi Watanzania na Itajengwa na sisi Watanzania. Chuki / Uovu / Tamaa na Majungu yasiyo na Mshiko vyote hivi ni Uvivu na Ucheleweshaji. Tunacho taka toka kwenu na kwetu sote ni tuwe wamoja Kuliletea Taifa hili Maendeleo.. Na cha kwanza kabisa Ni WEWE kujijia kwamba una Wajibu wa Kufanya Hivyo Bila Kujali una mwelekeo upi na umetoka wapi na unategemewa kufanya Nini leo na Kesho... Ukitenda zuri na lenye manufaa kwa nchi UTAKUMBUKWA na vinginevyo utatukanika...
    Inasikitisha na kuleta wasi wasi ikiwa nyinyi mne daiwa kuwa Waheshimiwa mnaweza kuzungumza hayo maneno mtawahamasisha vipi wanachi kuijenga hii nchi kwa hali tuliyoikuta na tunavyo enda mbele. Ningeomba Mfupishe hayo Majungu na Kuelekeza nguvu zenu na zetu tuliletee Taifa Maendeleo... Hapa Kazi tu.. Na tumuombee Mungu ampe umuri na afya Mchapa kazi wetu JPJM na timu yake na wote tumpe ushirikiano wetu ili azidi kututumikia na kumrahisishia Kazi ngumu tuliyompa. Na kama mnajiona mnahitaji mapumziko mlango uko wazi na wenzenu wako tayari kuendelea na kazi ikiwa nyinyi mmeona Kazi Kufanya Kazi. Na isiwe kazi kuwacha kazi ili Mtuache Tufanye KAZI... Hongera Wakuu wetu chini ya JPJM. MUNGU IBARIKI TANZANIA YA UMOJA AMANI NA UPENDO.

    ReplyDelete

  2. KUKOSA UELEWA NA MASIKITIKO YA KUTOELEWA HOTUBA YA MTUKUFU RAISI JPJM.

    HIYO TUNAKWENDA WATU MBATIA -MBOWE NA WASHABIKI WENU MLIOKOSA MWELEKEO!!!!!!

    Baada ya Kuisoma na Kuitafakari hii makala hapo Juu.. Inadhihirisha na inabainisha Ufinyu wa Uelewa alicho kizungumza Mtukufu Raisi Dkt JPJM.. Maudhui na mwelekeo wa wazungumzaji ni utashi wa kutuonesha kuwa wao Hawakubali. Hawakubali nini Hawakujui baada wa kuchanganya Madaa zilizokuwepo na zisizo kuwepo... Na ni tofauti kabisa na Mazungumzo ya Raisi wetu.

  3. KUKOSA UELEWA NA MASIKITIKO YA KUTOELEWA HOTUBA YA MTUKUFU RAISI JPJM.

  4. mageleza Tunayo... Kwani wahalifu wamezidi???

    ReplyDelete
  5. Hapa ndugu zetu inaonesha Kasi ya Magu hawaiwe na Hawataki Kuielewa!! Hapa kazi tu.

    ReplyDelete
  6. Mhhhh... Mwacheni Magu afanye yake!! Kaamua Kujituma na Anatumika Ipasavyu.
    Fyuuuu... Mtamuona hivi hivi nchi inakenda mbele wavivu wakubwa.. Hapunguzi Spidi.

    ReplyDelete
  7. Hawa UKAWA Wamechanganyikiwa Hawajijui.

    ReplyDelete
  8. Ahhhhhhhhhhhh.... Si Utumbo Mtupu wa hawa Nyumbu!! Sasa Ndiyo wamezungumza Nini... Siasa Siasa Tumeshazichoka wangoje wakati wake... Utakuja tu si sasa.

    ReplyDelete
  9. nIMEONA WAZUNGUMZAJI WATATU WAWILI KINA KAKA NA MDADA MMOJA... LAKINI SIKUWAELEWA. JAMANI NISAIDIENI WANASEMA NINI????

    ReplyDelete
  10. Hawa hawana jipya. Ndio zile zile zao. Hatu huko mbungeni wanaingia mitini. Posho la laivi inawasumbua.. Walizoweshwa vibaya . hapa ni kazi tu.

    ReplyDelete
  11. Wanachi wa Vujo na Hai mnawaona mliowapa kula hao.. Hawastahili Kula mara ijayo. ajili wamekosa Ulaji kama mlivyo wapa Kula na inakula kwenu. Si mnaona wenyewe.
    hata ule mwelekeo wa ulaji na posho inakwenda mlama. Inatisha hiyo.
    JINA KAMILI NA STATUS ZENU NI LAZIMA TUJUE. MNAMTUMIKIA NANI? MANAKE MKISEMA WANANCHI NI ITAKUWA SIYO KWELI.. TUJULISHENI PLIZI SANA

    ReplyDelete
  12. Dkt Tulia .. Hongera sana Mama.. Nchi inarudi kwenye mstari ndiyo kubwabwajika kote huku. Hii spedi ni balaa... Endeleeni Chini ya baba JPJM. Pamoja sana.

    ReplyDelete
  13. Mhhhh walakini hapa..comments hazijachapishwa ..mpaka sasa vp?

    ReplyDelete

Top Post Ad