Watu 50 Wauawa Baada ya mtu Mmoja Kushambulia klabu ya Mashoga Marekani

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Raia wa Marekani, Omar Mateen, 29, ameishambulia kwa bunduki klabu ya mashoga iliyopo Orlando nchini Marekani.

Mateen, anayetokea Port St. Lucie Florida, ameua takriban watu 50 na kujeruhi wengine 53 na kushikilia mateka.


Polisi walitumia mabomu kumchanganya mtu huyo na kuwaokoa watu karibu 30 waliokuwa wameshikiliwa mateka. Mateen alipigwa risasi na polisi saa kumi na moja alfajiri baada ya tukio hilo kudumu kwa masaa matatu.

Hilo ni tukio baya zaidi la aina hiyo kuwahi kutokea Marekani. Maofisa kwenye hospitali ya Orlando wamedai vifo vinaweza kuongeza.  Muda mfupi kabla ya shambulio hilo, Mateen alipiga simu 911 kuelezea utii kwa kundi la ISIS.

Baba yake Mateen, Mir Seddique, aliiambia NBC News kuwa mwanae alichukia baada ya kuwaona wanaume wawili wakipigana busu huko Miami miezi kadhaa iliyopita.

Kulikuwa na takriban watu 320 ndani ya klabu hiyo na karibu 100 walishikiliwa mateka.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. na hao watu walioshangilia hilo tukio na kumpongeza huyo jamaa aliyefanya mauaji katika blog ua bongo5, all i can say shame on you! wale watu waliouliwa hata kama ni mashoga na wenyewe pia ni binadamu kama nyie utawezaje kumjaji mtu ambaye humjui hamna mtu yeyote anastahili kuuwa namna hiyo kisa ni shoga kwanza hao waarabu kwa ushoga ndiyo wenyewe ila wanaficha na ni siri sana sababu ya dini yao, utakuta mtu anaye mke lakini anaenda kulala na wanaume, hata huko Marekani ambako tukio limetokea kule hamna mtu alyepongeza kutokea kwa tukio hilo, pia hata hapa Ulaya hamna mtu aliyepongeza kutokea kwa tulio hilo ni Tanzania tu ndiyo mnapongeza hiyo yoote inaonyesha ninyi Tanzania elimu ni duni sana na mko nyuma sana kimaendeleo pia inajulikana duniani kote kuwa Tanzania inawaua watu wenye ulemavu wa ngozi kuzani kuwa hao watu si binaadamu, pia inajulikana Tanzania inawanyanyasa watu wenye maambukizi ya ukimwi na ndiyo maana watu wenye maambukizi ya ukimwi wanajificha, mambo kama hayo hayatokei Marekani na hapa Ulaya, halafu mnampongeza huyo mwarabu aliyofanya mauaji hamjui kama hao watu wana ndugu na marafiki ambao wanawapenda, kama nyie hamna moyo na hao watu na akili yenu finyu lakini mjue hao watu waliouliwa wana wazazi, ndugu na marafiki ambao wanawapenda hata wangekuwa namna gani, hata mkiamua kunitukana nitukaneni lakini mimi nawatetea hao mashoga, na ndiyo maana pia Mungu ametaka na huyo aliyefanya mauwaji waende njia moja na hao watu aliyewatendea ukatili huo na ndiyo maana polisi wema wakalishoot hilo jamaa, na polisi wamefanya kazi nzuri wanastahili tuzo ya mwaka.

    ReplyDelete
  2. naona km naww bwabwa

    ReplyDelete

Top Post Ad