Baada ya Kufunga Goli Kwenye Mchezo wa Europa League Samatta Afunguka

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mtanzania Mbwana Samatta aliweka rekodi ya kufunga katika michuano ya Europa League baada ya timu yake ya Genk kuibuka na ushindi wa magoli 2-0 mbele ya Budućnost ya Montenegro.

Clouds FM kupitia kipindi chake cha michezo cha Sports Extra kilifanya mahojiano maalu na Samatta kutaka kujua mambo mbalimbali. Mtandao huu ukaona haitakuwa vibaya kama utakuletea kile alichokisema nyota huyo hasa kama ulikosa kusikiliza show ya Sports Extra.

sportsextra: Mbwana Samatta unajisikiaje kuwa Mtanzania wa kwanza kufunga goli katika michuano ya Europa League?

Samatta: Nimejisikia vizuri kwasababu ndiyo kitu ambacho kila siku nakipigania kuweza kufanikiwa, mshambuliaji unaweza kufunga magoli, nimejisikia vizuri na inanipa morali zaidi ya kuendelea kujituma.

sportsextra: Ulianza katika kikosi cha kwanza mbele ya Nikola Karelis mshambuliaji wa kutumainiwa wa Genk, hii inamaanisha kuwa mwalimu Peter Maes anakuamini sana kuliko mshambuliaji huyo anayehusishwa na kujiunga na klabu ya Nottingham Forest ya nchini England?

Samatta: Nafikiri sasahivi mwalimu ananiamini na anapenda kunitumia, ni kitu ambacho kwakweli ni kizuri kwangu mwenyewe binafsi lakini pia nafikiri yeye kwake anaona namsaada mkubwa kwenye timu yake nikiwa naanza kwenye kikosi cha kwanza. Nafikiri ni jambo la kusubiri muda utakapofika kilakitu kitakuwa wazi lakini kwa sasahivi nafikiri mwalimu anapenda kunitumia zaidi.

sportsextra: Watu wengi walikuwa wanajaribu kujiuliza kuwa Mbwana yupo wapi wakati wa likizo yako baada ya kusimama kwa Ligi Kuu ya soka nchini Ubelgiji. Watu wanataka kujua ulikuwa wapi Mbwana wakati wa mapumziko?

Samatta: Likizo nilikuwa Tanzania japo likizo ilikuwa fupi lakini nilikuwa nyumbani nimepumzika ilikuwa ni kipindi cha mwezi wa Ramadhani kwahiyo nilikuwa kwenye mfungo. Ilikuwa haina sababu ya kuonekana kwasababu ilikuwa ni kipindi cha mapumziko.

Ukifata program ya mazoezi kutoka kwenye timu, ilikuwa ni muda wa kupumzika kwa wiki moja halafu wiki nyingine unatakiwa ufanye mazoezi wewe mwenyewe binafsi. Lakini kwa bahati mbaya mimi sikupata muda wa kupumzika kwasababu wakati likizo inaanza mimi nilitakiwa nijiunge na timu ya taifa kwa ajili ya mechi dhidi ya Misri na baada ya hapo niliendelea na program ambayo nilipewa mimi binafsi.

Mchezaji anapopewa likizo anatakiwa apumzike kabisa kwasababu ni kipindi ambacho mwili wake unatakiwa ujirudi na kutengeneza nguvu mpya. Haina maana kwamba ukipewa likizo basi ujifue na kujiweka nondo hapana, muda wa mapumziko ni kipindi ambacho anatakiwa apumzike kama amepewa program basi afanye lakini asijichoshe.

sportsextra: Mbwana nafasi ya timu yako ya Genk sasa unaionaje katika michuano ya Europa League baada ya jana kupata ushindi mbele ya klabu ya Budućnost?

Samatta: Nafikiri bado tunakibarua kwasababu ni mechi ya kwanza na tumeshinda kwa goli 2-0, mpinzani sasahivi kichwani kwake anajua kwamba amefungwa goli mbili na anahitaji kurudisha na kupata ushindi akiwa nyumbani, kwahiyo kibarua bado kipo siwezi kusema moja kwa moja kwamba tutakata tiketi ya kucheza kwenye makundi lakini nafikiri tuna timu nzuri na tunaweza kufika huko kwa hiyo kila kitu ni wakati.

sportsextra: Asante sana Mbwana Samatta.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad