Maigizo Yanaendelea..Moshi Napo Jeshi la Polisi Laonyesha Mkwala wa Kudhibiti Maandamano

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Moshi. Mazoezi ya Polisi mkoani Kilimajaro yaliyodumu kwa takriban saa nne yaliyofanywa na vikosi vya askari wa kutuliza ghasia na magari ya washawasha, yametikisa mji wa Moshi na kuzua hofu kwa  wananchi.

Baadhi ya wananchi walishangazwa na kitendo hicho cha polisi  kuzunguka wakiwa na mabomu ya machozi na gari la maji ya washawasha.

Mkazi mmoja, Peter Lyimo alisema ameshtushwa kuona magari ya polisi yakizunguka, huku milio ya milipuko ya mabomu ikisikika.

Naye Mary Kavishe alisema: “Tumezoea kuona polisi wakifanya mazoezi kambini kwao, siyo kuzunguka katikati ya mji.”

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbrod Mutafungwa  alisema wanafanya mazoezi ya kawaida ya kujihami na wahalifu  na kulinda wananchi na mali zao.

“Ni mazoezi ya kawaida na yanafanyika mkoa mzima kwa ajili ya kuimarisha askari wetu,  ili kujihami na matukio mbalimbali ya kihalifu,” alisema.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Toba
    Tuyazoeya kuwayaona kwa wenzetu
    Na kwenye sinema
    Sasa live Tanzania
    Mungu tuepushe na hayo

    ReplyDelete
  2. Mbona siku hizi tuu baada ya kusikia ukuta ndio wanachukua mazoezi mitaani kweli polisi wanatumika kutisha watu.

    ReplyDelete
  3. NA WAFANYE HIVI KWA MAJAMBAZI SIO KUONEA RAIA WASIO NA HATIA

    ReplyDelete
  4. NYIE ACHENI TU TUZIDI KUMUOMBA MUNGU ATUSHUSHIE AMANI IZIDI KUTAWALA MAANA HATUJAZOEA FUJO HIYO SIKU SIJUI ITAKUAJE KILA MTU ATAFAKARI

    ReplyDelete
  5. Ni matumizi mabovu ya muda, silaha, ba matumizi mabuvu ya polisi ambao wanalipwa kwa pesa za kodi za wananchi.
    Wanatumia muda mwingi kuwasaka, kuwanyayasa raia badala ya kufanya upelelezi na kuwadhibiti majambazi, wanaopora na kutumia bodaboda kama walivyofanya Dar jana. Kiongozi wapolisi na majeshi wameshindwa kujua mienendo ya bodaboda sita zilizobeba majambazi na kwenda benki sababu polisi wako buze kuwasaka ukawa hii haileti picha. Na mnafanya mJaribio mijini je mtakaopokusanyika nyinyi wote mijini kutupa mabomu ndivyo hivyo majambazi wTafanya kuwaigeni na magaidi sababu mnafanya kama mchezo.hali kama hii magaidi watafanya na wananchi watakufa wengi sababu wamezoea kusikia milio yenu ya bunduki. Je mmeifikiria hii . Na jemedari anayelindwa je anawasahau watanzania wasio na ulinzi kama wake twenty four hours. Kwa nini watanzania wasipatiwe ulinzi wa nguvu na uhakika masaa yote ishirini na nne.ni wao ndio wanawalipa polisi.ni kodi zao. Watanzania wote wanapaswa na ni haki yao kumkatalia raisi matumizi ya jeshi , polisi, vifaa vya jeshi na muda wa wanajeshi kwa hasara na kwa vitisho.ni haki ya watanzania wote. Serikali imeshindwa kutoa elimu yenye faida kwa watoto watanzania bure, madawati bure, mishahara ya juu kwa wafanyakazi na polisi pia, inatumia pesa kuonyesha na kuogopesha wananchi na kuwatisha na kunyanyasa wasomi. Pesa ngapi inatumika ya watanzania vibaya. Na kwa nini raisi aseme nendeni mjiandae kwa lolote, na wakuu wa mikoa, wilaya watangaze vita dhidi ya wananchi.wamepewa kibali na sheria gani ya nchi.huwezi kuwaogopesha watu, inabidi uwape uhuru watu, elimisha watu, wasadie kiuchumi kuumuza uchumi wa nchi badala ya kuwaomba wamarekani, wafaransa wenye interest binafsi nchini na wachina wanaosomba jila kitu wakichukulia faida ya kwamba Watanzania wananyanyaswa na utawala wao na kuwazibia mafanikuo nchini kwao. Ni hawa ndio mnawatetea kwa pesa za watanzania. Mnawapa umiliki wa gesi, madini, mbuga, na ni hao wanaleta haya mabomu mnayoyatumia kukandamiza raia.wanaleta vyombo vya vita kuchochea na kukoroga nchi na watu wa amani kwa maslahi yao.mnawatajirisha bila kupitia wananchi.mnawapa mali bila kumhusisha mtanzania mwenye mali zake.huu ni ubadhilifu, ubepari, na unyonge wa Mwafrika na ukandamizaji wa Africa nzima na kuwaachia uchumi wautawale.watawala wengi hawaoni muwa haya yameingiliana.Ukawa wameona hii CCM imetumia madaraka vibaya miaka hMsini lakini hasa miaka ya awamu ya utawala wa miaka ya maraisi watatu waliopita.sasa mnatumbua watu wa chini wahusika mnawaogopa mtasafishaje nchi. Hii ndiyo inayotunyanyasa Watanzania. MtaNzania atajikomboa kivipi, anaposema mapepari na serikali wanatuibia, na kutunyanyasa.
    Hapa tulipofikia inAbidi hata polisi wanaoti amri na majeshi wajiulize ndio hivi waliapishwa munyanyasa na kuwatisha walipakodi wanaokatwa kila mwezi ili waishi? Wanayemnyanyasa ni baba zO, mama zao, shangazi zao, watoto wao, dada zao, kaka zao ambao wanadai uhuru, ajira, katiba, uwazi, na maendeleo ya kweli.

    ReplyDelete
  6. Ujinga mtupu mnaacha kwenda kupambana na majambazi mnaangaika na watu ambao hawana silaha.

    ReplyDelete

Top Post Ad