Familia ya Diamond Yaikacha Sherehe ya Birthday ya Zari Iliyofanyika Zanzibar...Mabifu Yaibuka Upya

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

MWISHONI mwa wiki iliyopita (juzi Ijumaa usiku) ilifanyika pati ya kusherehekea kuzaliwa kwa mpenzi wa Mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari’ ambayo imeibua mabifu upya. Pati hiyo iliyohudhuriwa na mastaa wachache kutoka Bongo ambao ni pamoja na Moze Iyobo, Aunt Ezekiel na wengineo ilifanyika Zanzibar ambapo licha ya kufana, imeibua mtifuano upya kati ya Zari na wifi yake, Esma Abdulkadiri na Diamond na mume wa zamani wa Zari, Ivan Semwanga.
 
IVAN NA DIAMOND
Bifu la wawili hawa lilikuwa limezimika, lakini lilirudi upya baada ya juzikati Diamond kumzawadia Zari nyumba iliyopo Afrika Kusini kisha kumrushia Ivan dongo kwa kuandika mtandaoni: “Wanakazana kujisifu matajiri ilhali watoto wao wanaishi kwenye nyumba za kupanga… halafu leo yuleyule wanayemtukana kutwa kwenye mitandao kuwa maskini, kajawa na shida, kanunua nyumba kulekule kwao ili watoto wao waishi maisha bora kama wanayoyatamani… Heri ya siku ya kuzaliwa Mama tee wangu…. Nakupenda sana na unalifahamu hilo…natumai umeipenda nyumba yetu hii mpya South Africa.”

NI DONGO KWA IVAN
Ujumbe huo moja kwa moja u l i o n e k a n a kumhusu Ivan ambaye kipindi cha nyuma kwa kushirikiana na mshikaji wake aliyefahamika kwa jina la King Laurence, walikuwa wakimtusi wakimsema kuwa ni maskini ila wao wana pesa licha ya madai kuwa, nyumba wanayoishi watoto wa Zari kule Sauzi ni ya kupanga. Baada ya dongo hilo, hali ilichafuka huku Ivan akimrushia madongo Diamond sambamba kumtaka Zari amwambie bwana wake (Diamond) aondoe ujumbe huo mtandaoni kwani hata wanaye wakiuona wataumia. Inadaiwa kuwa, licha ya Ivan kuomba hivyo, Zari alimjibu kuwa Diamond amegoma kwa maelezo kwamba, wao (King Laurence na Ivan) ndiyo walioanza kumtusi.

 ESMA NA ZARI
Bifu lao lilihusishwa baada ya Esma kuulizwa sababu za kutomuwish wifi yake katika siku yake ya kuzaliwa, kuonesha ‘analo na limemfika hapa’ alifunguka: “Siwezi kumuwishi, mbona Taraj (mwanaye) hakumuwishi wakati ndiye aliyekuwa akicheza na mwanaye (Tiffah) nyumbani? Wee ukosane na mimi umkasirikie hadi mtoto, ujinga huo. Siwezi kumuwishi Mbona Bi. Snura (mama wa Diamond) alimuwishi akamfuta na mafumbo juu, akasababisha watu wakamchamba!….. (anataja jina la mwandishi) nimekaa tumboni kwa mama yangu miezi 9 ‘so’ mtu anavyomletea dharau siwezi kumpenda. Mbona wote tumekaa nao vizuri haijawahi tokea haya mambo, kwa nini yeye?” alihoji Esma.

FAMILIA YA DIAMOND YASUSA BETHIDEI
Katika kile kinachoonesha kuna kitu kizito nyuma ya pazia kati ya Zari na ndugu wa Diamond, inadaiwa hakuna hata mmoja aliyefika hali iliyoibua maswali mengi.

DIAMOND, ZARI VIPI?
Kufuatia kuibuka kwa mabifu hayo sambamba na figisu nyingine, gazeti hili lilifanya jitihada za kuwatafuta Diamond na Zari kupitia simu zao za mkononi ili waseme lolote, lakini simu zao hazikuweza kupatikana.

Global Publishers
________________

KISASI CHA USALITI PENZINI !!!,usipoipenda simulizi hii dai Mb na pesa zako,licha ya kuenjoy mahaba ndani yake kuna kitu cha kujifunza mwishoni Bofya Hapa kusoma Sehem ya 1 bure,sehem iliyobaki tsh 2000 kwa mtandao wowote.

Tembelea www.makapedia.com kwa stori mpya kila tarehe moja.


JE UNATAKA BIASHARA YAKO IWE YA UHAKIKA MIAKA YOTE YAJUE HAYA? usikose kitabu hiki Bofya Hapa kusoma sehem ya 1 bure sehem ya 2 tsh 2000 tu 

ndani ya www.makapedia.com

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

17 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
 1. Acheni mambo yenu bwana......sio kila kitu familia familia kwani nyie mna mamlaka gani kwenye maisha ya diamond na familia yake???!!!Familia haiwezi kupanga maisha jinsi ya kuishi na mkeo bwana kama wamesusa waende zao huko. Huyo esma jinga tu pia.....kuna mambo ya kuongea mkiwa kama familia sio kuropoka kwenye public

  ReplyDelete
  Replies
  1. Kweli kabisa, wasiingilie nyumba za wenzao wakati zakwao zimewashinda

   Delete
 2. Mkimaliza kutunga tunzeni familia zenu.

  ReplyDelete
 3. Ni kweli mke kwanza ila mke anaye mdharau mama yako mzazi aliyekubeba miezi 9 tumboni....I don't think kama ni mke mwema....wote tunajua mama mkwe na mawifi always wana visa ila you have to think twice.....wewe uliotoa comment hapo juu ...sijui kama una mke na una mama mzazi unaye mpenda kuwa uyaone.....

  ReplyDelete
  Replies
  1. kweli hata kama mama mkwe ni mkorofi lakini ndo mzaa chema huyo huna budi kumuheshimu maana hakuna mkamilifu

   Delete
 4. Domo
  Zari
  Ivan
  Udaku
  Wote pumbavu

  ReplyDelete
 5. Mwacheni diamond atulie na zari tatizo wanandugu hapo want to lead macho vijimali wanamuonahuyodada wakiganda anafaidi kumbe munguamewapangia maisha bora

  ReplyDelete
 6. NDIO KAZI ZA WASWAHILI, KAZI KWENU HEBU WAACHENI JAMANI DIAMOND NA ZARI WAFURAHIE MAISHA .

  ReplyDelete
 7. ni kweli kabisaaa zari kafanya vibaya mnooo,hawezi mzarau mama daimond na wakati mama huyo akikasirika daimond hawezi fika popotee!!! ukweli ndo huo zari anaroga sana ili awe na daimond lakini atashindwa tuu...yetu machooo!!!!huyo mama kahangaika sana na mwanae mpaka kufika hapo alipo sio fair at alll...yeye azae tuuu kama kuku lakini mapenzi yao hayana mwisho mwema ni bora zari aombe msamaha tuu...sio kitu kizuri alichokifanya ndo ubaya wa kutembea na makahaba.

  ReplyDelete
 8. wanawake kawaida sio watu wema % kubwa wakishapata mume basi tena inakuwa kama ndio kapewa sadaka wakati ulipo moata huyu bwana ulimkuta na mama na dada zake yaani ndungu kwa ujumla sasa kitu kina cho shangaza ni kuwa heshima inakuwa hakuna dgarau nyingi mke ana haki na mama na ndugu vile vile wana haki hasa mama badili yake hakuna vp daimondi ana kubali mama yake adharauliwe au akisema kapata mke mwema hapo kakosea kabisa zari hana tabia uzuri ni wa mawigi na makeup kitu muhimu heshima kwa mama mzaa chema amka wewe diamondi

  ReplyDelete
 9. True angaliye yenu

  ReplyDelete
 10. Hawa wazazi wetu wanaojifanya wanajua mitandao ni tatizo hasa wazazi wetu wa kiswahili toka Mama domo amempost wema na Ujumbe wake uzalendo kwanza.niliona tatizo tutoe ushabiki jiweke Kwa nafac ya zari wewe mwanamke Mama mkwe wako ampost aliyekuwa mpenzi wa mmeo utafurahi? Au ata anamsifia tu mbele yako utajickiaje. Na kwenu wanaume Baba mkwe wako amsifie mpenzi wa zamani wa mkeo utafurahi? Hiyo itaonyesha wazi kuwa familia ya mmeo hawakupendi lakini kama wao hawakupendi lakini mtoto wao kafa kaoza kwangu inabidi nikomae na mpenzi wangu hayo mengine baadae. Kwani kama familia inakupenda lakini mwanamme wako hakupendi uwezi kuolewa nafamilia.lakini kama mmewako anakupenda lakini familia aikupendi mnaweza ishi kwenye ndoa miaka yote tena Kwa furaha. Muacheni domo na zari.

  ReplyDelete
 11. Ame post wema kama star wa Tanzania ache unafki mama ni mama atakama ako naupere utanyonyatu

  ReplyDelete
 12. Ame post wema kama star wa Tanzania ache unafki mama ni mama atakama ako naupere utanyonyatu

  ReplyDelete
 13. yes mama ni mama hakuna kama mama wala badili ya mama na ukitaka dunia yako maisha yako na watt wako iwe na furaha mtii mama yako yeye ndie anaejui whats good for you ama wanawakw mbona wamejaa ni upende mwenyewe wapo tu kama samaki you choose what is good wake up Naseeb usije ukajuta baadae

  ReplyDelete

Top Post Ad