Kama ni Rahisi Kununua Tuzo, Wanaosema Hivyo na Wao Wakanunue – Babutale

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Babutale amezijibu shutuma za baadhi ya mashabiki nchini kuwa wasanii wa WCB wamekuwa wakinunua tuzo.

Akiongea na Prince Ramalove wa Kings FM, Tale alikuwa na maneno mafupi tu kuwajibu. “Kama ni rahisi na wao wakanunue,” alisema meneja huyo.

Jumamosi iliyopita Diamond na Harmonize walishinda tuzo za Afrimma zilizofanyika jijini Dallas, Marekani.

Alidai kuwa tuzo hizo ni za Tanzania nzima na imeonesha jinsi gani mashabiki wako nao pamoja. Amesisitiza kwa kuwaomba waendelee kuwapigia kura wasanii wote waliotajwa kwenye tuzo za MTV MAMA wakiwemo wasanii wake wa WCB, Diamond na Raymond.

Wengine ni Alikiba, Navy Kenzo, Yamoto Band na Vanessa Mdee.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. WCB WANATUMIA USHIRIKINA na hata kama kununua pia wanaweza na unapo sema hao wanao sema tumenunua tuzo na wao wakanunuwe (kama kweli mumefanya hivo basi huo sio ungwana) shindeni ki halali hata nafsi zenu hazewezi kuwasuta

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mbona wabongo mna roho za korosho hampendi mtu akafanikiwa inakuwaje na povu linawatoka na ni kweli WCB walivyosema kama wemenunua hizo tuzo na wengine wakanunue ina maana wamezipata kihalali ingekuwa zinauzwa wengi wangezinunua na kama ushirikina ndo unaleta mafanikio duniani ingekuwa njia ya mkato watu kupata mafanikio bila kujituma na hakuna mtu angekufa njaa mmoja wapo ni wewe

      Delete
    2. Inaonyesha jinsi gani akili yako ilivyo mgando na nina wasi wasi na elimu yako pia...acha chuki kijana.....diamond alichaguliwa kwenye category zaidi ya nne angekua ananunua au anatumia uchawi si angechukua zote?? lakini kapata moja....hivi juhudi anazozifanya inamaana huzioni ukampongezaq hata kwa hilo...acha chuki aliepewa kapewa dogo...huwezi kuendelea katika maisha yako kwa fikra hizo badilika life is not a rehersal is a perfomance

      Delete
    3. hahaha hakuna cha ushirikina wa wala nini jamaa wanapiga kazi kwa saana tu. wazungu wanahongwa??? sh ngapi?? wanalogeka??? wasafi classic baby kazeni buti. Pigeni kazi kwa kwenda mbele!!!

      Delete
  2. Mimi nakubalian nahao wanaosem kawa wcb wananunua tuzo ni kweli kwani nimeshangaa nikapigw na butwaa eti Harmoniz kashind tuzo ahahaaaa inachekesh. Harmoniz nae alish kuwa msanii? toka lini? acheni bana. Mtu kuitw msani ni pal anapoimb bila kushirikish ao kushirikishw na aonesh uwez wake. Ila kwa sasa utaon hao eti ni WCB hawafany hayo. Utasikia nao eti ni lable kubwa ahahaaaaaa TZ bhana ingali nyuma. Diamond mwenyew amekwish ni jina tuu limebaki kwan mzik anao fany ni wakushirikishw ao ashirikish so hapo ndo utaon kam amekwish.

    ReplyDelete
    Replies
    1. wewe mwenye jina ambalo halijaisha mbona hatukusikii??? acha ujinga jitume kama WCB utafanikiwa pia acha wivu wa kijinga na kipumbavu mnasema sana lakini vitendi kudigo mfyuuuuuuuu

      Delete
  3. Chizi huyo haujielewi maneno ya mkosaji hayo ha ha ha haaaaah duh

    ReplyDelete
  4. Ni biahsra tu kama hamjui. Hizo ni tuzo za kura za mtandao tu, kama una wafuasi wengi instagram basi unaweka link wakupigie hata kama wimbo wako hauiskiki redioni bado ukipata kura nyingi kutoka instagram unapata tuzo. Kama Daimondi ana wafuasi milioni tatu kule instagram na anwalipia baadhi yao mtandao basi akiweka linki tu, kura zinajaa. Ndiyo maana tuzo za maana huwa hazipigiwi kura za mtandao, na hakuna mtanzania aliyewahi kupata ktuzo isiyotokana na mtandao.

    ReplyDelete

Top Post Ad