Kwa Mara ya Kwanza Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli Kutembelea Nchini Kenya....

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kwa mara ya kwanza Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli, atazuru taifa jirani la Kenya hapo kesho Jumatatu.

Ziara ya Magufuli nchini humo, inatukia wakati ambapo uhusiano wa mataifa hayo mawili umekuwa ukilegea.

Kwenye ajenda ya ziara hiyo rasmi ya kiserikali, kati yake na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta, ni kuimarisha biashara kati ya mataifa hayo mawili, kwani Rais magufuli amekosa kuhudhuria mikitano mikuu miwili jijini Nairobi, iliyowaleta pamoja marais wengi wa Afrika.

Tangu aingie mamlakani mwezi Oktoba mwaka jana, Rais Magufuli ambaye ameamua kukabiliana na ufisadi nchini mwake amezuru tu Rwanda na Uganda.


Pia ziara ya Dkt Magufuli inahusia na hatua ya Rais Uhuru Kenyatta kumpendekeza waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Kenya Amina Mohammed kwa kinyanganyiro cha wadhifa wa mwenyekiti wa muungano wa afrika-AU.

Tofauti na Tanzania, kashfa za mamilioni ya dola inafichuliwa mara kwa mara nchini Kenya, huku pesa za umma zikinyakuliwa na baadhi ya watu mashuhuri serikalini na walio na uhusiano wa karibu na watawala wa nchi hiyo.

Rais Uhuru Kenyatta atamkaribisha mgeni wake jijini Nairobi, baada ya Kenyatta kukamilisha ziara ya siku mbili huko Khartoum, alipokutana na Rais wa Sudan- Omar Al- Bashir.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ujirani mwema tutaudumusha na Marafiki wapya wenye Nia njema na Taifa letu na wawekezaji wente kupenda masilahi ya nchi mbili husika Tutaendelea kuwatafuta kama wafalme WA nchi mbili waliokuja karibuni hawa wanamuogopa mungu na si matapeli Tutaendeleza uhusiano WA karibu zaidi kuzidisha ajira kwa vijana wetu. Na Kula tuliyopakana nao undugu wetu tutauimarisha zaidi na ushirikiano. Bila Tamaa na kwa uadilifu WA hali ya juu. Mungu Skype umuri na afya njema Baba..Tuko begs kwa begs. Hapa Kazi Tu

    ReplyDelete

Top Post Ad