Bondia Mashali Aliponzwa na Tsh.1000

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Rafiki wa karibu wa marehemu Thomas Mashali aliyejitambulisha kwa jina la Ally amesimulia mkasa mzima wa kifo cha rafiki yake huyo.

Tokeo la picha la thomas mashali

Ally alisimulia mkasa wa rafiki yake huyo akiwa msibani maeneo ya Tandale jijini Dar es salaam, ambapo amedai kuwa juzi usiku alipata taarifa za kushambuliwa kwa Mashali na watu wasifahamika maeneo ya Kimara jijini humo.

“Ilikuwa usiku nimekaa nyumbani Manzese Madizini akaja dereva bodaboda anaitwa Yusuf Kidevu akaniambia babaako wanampiga huko Kimara wanamuua kama vipi nenda.”

“Nikahisi ni uongo kwasababu wakati mwingine wanazusha tu, mara kidogo akaja mtu wa pili akasema babaako anakufa huko Kimara, kwasababu alikuwa ni mtu wa pili kuniambia nikaona bora niende.”

“Nikaenda hadi Kimara, kufika pale nikakuta wameshampiga wamemuumiza askari wanampakia kwenye gari. Nikalifata gari hadi Sinza, akapata kitanda akalazwa nikaenda kumsalimia lakini saui ilikuwa inatoka kwa mbali hadi usogeze sikio ndio unaweza kumsikia.”

“Nikamuuliza imekuwaje, akasema kuna dereva bodaboda alimkodi lakini walivyofika Kimara akampa hela kidogo wakaanza kuzozana ndio mkasa ulipoanzia.”

“Alimpa shilingi 2000 lakini dereva bodaboda alikuwa anataka shilingi 3000, akaanza kumtukana Mashali akaona anadharauliwa akampiga ngumi yule dereba bodaboda akaanguka chini, baada ya hapo akaanza kupiga kelele za mwizi wakaja watu wengine watatu wakataka kumpiga akapambana nao akawapiga.”

“Baada ya kuona wote hawamuwezi wote wakaanza kupiga kelele za kumuita mwizi, wakaongezeka watu wengine wakaanza kumshambulia.”

Mwili wa Thomas Mashali unatarajiwa kuzikwa Jumatano jijini Dar es salaam.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. " Alimpa 2000 na dereve alitaka 3000" Kumbe alikuwa ni mwizi. Msitake kutetea maovu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Acha ujinga wewe sasa ndio umeona sababu ya kutoa uhai wa mtu.Vyombo vya sheria vipo mob justice haifai.

      Delete
    2. Anoni wa kwanza inaelekea unaweza ua kwa 200 pole sana asee!!!!!

      Delete
  2. Nae huyo mashali ndo alitumia huo ubondia wake mana niashara ni kupatana tu sio kwavile ni bondia ujione naweza fanya lolote bila mtu kuniweza. Angepatana nae tu kabla hajapanda hio bajaji sijui bodaboda lakini nae huyo mashali alijua lolote mimi ni bondia akinifanyia nisilotaka nitampiga yeye dereva hana kosa kadai haki yake na ni uongo hakupatana nae mana angepatana nae tokea safari haijaanza kusingetokea mapigano yaliopelekea mauwaji hayo. Ubondia jamani ni ulingoni sio mitaani na ktk biashara za watu.

    ReplyDelete
  3. Vyombo vya sheria vipo wapi?? Rushwa, uonevu nk

    ReplyDelete
  4. kweli ni heri wangepatana kabla hajapanda sababu bongo ya leo kitu kidogo tu unaitiwa kuwa ni mwizi na kwa watu ambao mnaishi bongo hayo mtakuwa mnayafahamu sababu yanatokea kila kukicha hivyo ili kuepukana na hayo matatizo ni heri kuwa mwangalifu na makini na mkweli kama bondia angemwambia dereva boda boda kuwa mimi nina 2000 tu kabla hajapanda hapo dereva angeweza kuamua apande au asipande kuliko kunyamaza kimya hayo yote yasingetokea naona dereva boda boda kaona amepewa zarau kwenye kazi yake sababu hizo kazi hamna mtu anayependelea kufanya kazi ambayo ni hatari lakini pamoja na yote siyo mpaka wamtoe mtu uhai Wake au kuwatoa watu uhai sababu ya pesa, jamani serikali iko wapi na inafanya nini, kwa nini serikali inaangalia tu mambo haya yakitokea kila siku bila kufanya lolote kweli ni aibu kwa taifa maana mambo haya ya mauaji bongo yanazungumziwa sana Ulaya na Marekani mpaka watalii wanaogopa kuja bongo kuona vitu hivi vikitokea

    ReplyDelete
  5. rip bROTHER HAYA MAMBO YANASIKITISHA SANA

    ReplyDelete

Top Post Ad