Mmoja Auwawa kwa Kupiga Risasi Akipora Abiria kwa Kutumia Silaha

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mtu mmoja anayesadikiwa kuwa ni jambazi alijeruhiwa kwa kupigwa risasi na askari Polisi kisha kufariki dunia wakati akipelekwa katika hospitali ya Monduli kwaajili ya matibabu.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Naibu Kamishna Charles Mkumbo, alisema tukio hilo lilitokea usiku maeneo ya Makuyuni barabara ya Arusha-Makuyuni wilayani Monduli.

“Mara baada ya kulisimamisha gari hilo wakaanza kumpora abiria mmojawapo aliyejulikana kwa jina la Victor Pius (46) Mfanyabiashara, mkazi wa Majengo Moshi ambapo walichukua simu mbili aina ya Nokia na Samsung pamoja na fedha taslimu Tsh 50,000/=,” Alisema Kamanda Mkumbo.

“Wakati wanaendelea na tukio hilo askari Polisi waliokuwa high way patrol walipata taarifa za tukio hilo ambapo walikwenda kwa haraka na mara baada ya majambazi hao kuwaona walianza kufyatua risasi hovyo na polisi kuanza kujibu mapigo na kufanikiwa kumjeruhi mmoja wao na kuwakamata wengine kumi na mbili papo hapo wakiwa na mapanga sita na marungu manne huku wengine akiwemo na yule mwenye bunduki wakikimbia,” aliongeza.

Aidha Kamanda Mkumbo alisema jambazi huyo akiwa na wenzake wapatao 29 walikuwa na bunduki ambayo bado haijafahamika pamoja na silaha za jadi mapanga na marungu ambapo waliweka mawe barabarani na kulisimamisha gari aina ya Fusso lenye namba za usajili T. 871 BUZ ambalo lilikuwa lina mzigo likitokea Moshi kuelekea mkoani Singida.

Kamanda Mkumbo alitoa wito kwa wananchi wa mkoa huu kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za uhalifu ili zifanyiwe kazi kwa haraka, huku akitoa onyo kwa majambazi wanaopenda kujipatia kipato bila kuvuja jasho kwani Jeshi hilo limejiandaa vizuri.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mungu atawasimamia hawa vijana kwa kile kilichotokea

    ReplyDelete

Top Post Ad