NISHA: Mimba Hii Ingekuwa ya Baraka The Prince Inge.........

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Nyota wa filamu nchini ambaye siku za karibuni amekuwa akihaha na ujauzito alionaonao bila kumuweka wazi muhusika, amekanusha kuwa ujauzito huo ni wa msanii Baraka The Prince.

Nisha Baby amefunguka kuhusiana na hilo akiwa katika kipindi cha FNL cha EATV, na kusema kuwa endapo ujauzito huo ungekuwa wa Baraka kama inavyosemwa na wengi basi ungetoka wenyewe mapema sana kwa kuwa Baraka ni miongoni mwa wanaume asiowapenda kabisa duniani.

"Kama hii mimba ingekuwa ya Baraka, ingetoka yenyewe, wala isingesubiri" Alisema Nisha.
Kuhusu muhusika wa ujauzito huo, Nisha ameendelea kufanya siri na kuapa kutomtaja kabisa hata siku moja licha ya watu kutaja baadhi ya majina ya watu maarufu ambao amekanusha kuwa siyo wahusika.

Katika hatua nyingine Nisha aliweka wazi kuwa anatarajia kujifungua mtoto wa kiume, licha ya kuwa bado hajamtafutia jina.

Kuhusu mazingira aliyopata ujauzito huo, Nisha ambaye alijikuta akimwaka chozi studio, alisema mwanaume aliyempa ujauzito alimlazimisha kufanya naye mapenzi, na kwamba ahaikuwa ridhaa yake na ndipo ikatokea hivyo.

Kuhusu hoja za baadhi ya mashabiki kuwa ni kwanini hakuitoa kama hakuwa tayari, Nisha alisema imani yake ya dini haimruhusu kutoa mimba.
"Ingawa kuzidi ni dhambi, lakini kutoa mimba pia ni dhambi na dini zote haziruhusu kutoa mimba"
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. huyo itakuwa kapewa mimba na Baraka, na kuna dini wanaruhusu kutoa mimba endapo mimba itakuwa imetokea kwa bahati mbaya au kubakwa kama wewe

    ReplyDelete
  2. mimba mimba,hata panya ana mimba!!!

    ReplyDelete
  3. Dah huyo demu na mimba mbona kazi ipo. Mpaka siku anajifungua kwa kweli tutakuwa tumeyasikia mengi sana. Lakini kwa sababu huo uja uzito aliupata kinyume cha matakwa yake basi alipeleke hilo suala Mahakamani na likashughulikiwe kisheria zaidi badala ya kukaa na kung'aka humu kwenye mitandao. Kwani Kisheria kufanya mapenzi na mtu tena bila ya matakwa yake ni ubakaji na ni kosa kisheria na tena ni kosa la Jinai. Kwa hiyo huyo Nisha inabidi tu amtaje huyo mtu ili ashughulikiwe Kisheria zaidi.

    ReplyDelete
  4. TUMEKUCHOKA TOA SHOBO ZAKO.

    ReplyDelete
  5. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete
  6. mtoto akizaliwa atakuwa na sura ya Baraka hapo tutajua kuwa ndiye yeye alikupa mimba ndiyo maana unamchukia sana sababu alichaguwa kuwa na Naj

    ReplyDelete

Top Post Ad