PAUL Makonda Kuwashindanisha Christian Bella na Banana Zoro Kuimba Live....Bella Ajigamba Kuchukua Mil 50 za Zawadi

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Mkali wa masauti Christian Bella amejinadi kuwa atamshinda muimbaji mkongwe Banana Zorro katika pambano la kuimba live lililoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda.


RC Makonda wiki moja iliyopita aliwataka wasanii hao wawili kuandaa show ya pamoja ili washindane kuimba live na mshindi atampatia tsh milioni 50.

Akiongea na Bongo5 wiki hii Christian Bella, amedai hana shaka na pesa hizo kwani anajua atamshinda Banana na kuondoka na kitita kicho kikubwa cha pesa.

“Tunamshukuru Mh Paul Makonda ni wazo zuri sana kwa kutujali vijana, kwa kujali vipaji na kuvithamini,” alisema Bella. “Kwahiyo sisi tunaiandalia mazingira ili kuangalia itakuwaje kwa sababu tunatakiwa kuwa serious sana lakini tumeshapanga itakuwa mwezi wa pili au wiki ya mwisho ya mwezi Januari,”

Aliongeza, “Kwa upande wangu mimi sasa najiandaa, mimi sitaruka sarakasi bali nitaperform vizuri ngoma zangu zote kali, niimbe zaidi, nitafanya performance ya hasira ili nipate hiyo hela. Lakini mimi naamini hiyo hela niyakwangu hata kama Banana Zorro ni mkali na anaimba vizuri, mkongwe, kipaji lakini naamini mimi nitachukua hiyo hela,”
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Rc anawazo zuri bt anaowapambanisha sidhani wanastaili kupewa fursa ya mchongo kama huo coz hao wote wnapata hiyo fedha na wanamafanikio makubwa so ni sawa sawa na kujaza maji baharini so its better angetangaza underground wenye talent wagombee hzo dolla 20 ingekuwa fursa kweli kwa vijana

    ReplyDelete
  2. Rc anawazo zuri bt anaowapambanisha sidhani wanastaili kupewa fursa ya mchongo kama huo coz hao wote wnapata hiyo fedha na wanamafanikio makubwa so ni sawa sawa na kujaza maji baharini so its better angetangaza underground wenye talent wagombee hzo dolla 20 ingekuwa fursa kweli kwa vijana

    ReplyDelete

Top Post Ad