BASATA: Diamond Amestahili Kukabidhiwa Bendera ya Taifa Kwajili ya Show yake ya Ufunguzi wa AFCON 2017

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Kumekuwa na sitofamu katika mitandao ya kijamii kuhusu ni nani anastahili kukabidhiwa bendera ya Taifa ili kuwakilisha nchi, baada ya Diamond Platnumz kukabidhiwa bendera ya Taifa jana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Moses Nnauye kwajili ya show yake ya kutumbuiza ufunguzi wa michuano ya Afcon 2017 inayofanyikia nchini Gabon weekend hii.

Diamond akikabidhiwa bendera ya Taifa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Moses Nnauye

Mashabiki wengi katika mitandao hiyo wamekuwa wakizozana bila kupata jibu kwamba ni kwanini Daimond alikabidhiwa bendera hiyo kwa ajili ya kuwakilisha Tanzania wakati anaenda kufanya show yake binafsi.

Akiongea na Bongo5 Alhamisi hii kuhusu suala hilo Katibu mkuu wa na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) Godfrey Mngereza amesema bendera ya Taifa anaweza kupewa mtu yeyote ambaye anaenda nje ya nchi, na safari yake ina manufaa kwa taifa lake.

“Suala wa Waziri Nape ambaye ndiye Waziri mwenye dhamana ndani ya Wazira wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kumkabidhi Diamond bendera ya Taifa ni jambo zuri kwa sababu ingawa Diamond anakwenda kufanya show yake lakini tukumbuke yule ni mtanzania pekee pale ambaye anakwenda kuliwakilisha Taifa lake kwa show yake mbele ya maelfu ya watu Afrika nzima, jina lake linatambulika pale lakini wao wanamtambua yule kama mtanzania na hata akifanya vizuri sifa zinaenda kwa yeye pamoja na Taifa lake,” alisema Nngereza.

Pia Nngereza alidai mtanzania yeyote anaweza kukabidhiwa bendera ya katifa kama anaenda kufanya tukio lolote ambalo linaweza kuipatia sifa nchi yake kwa namna yoyote.

“Mtu yoyote ambaye anaenda nje ya nchi kwa ajili ya matamasha makubwa au kama kuna namna ambavyo anaenda kufanya kitu ambacho kimpatia yeye faida pamoja na Taifa lake anaweza kukabidhiwa bendera, awe mtanzania tu. Kwa hiyo hata ukiwa mtangazaji, mchezaji, vikundi vya ngoma na sanaa mbalimbali wanaweza kukabidhiwa bendera kama wakihiitaji kwa sababu kuna wengine hawatoi taarifa kuhusu matukio yao lakini kama ukitoa taarifa na mamlaka ikaona kuna umuhimu wa kufanya tunafanya hivyo kwa sababu ni kwa ajili ya taifa letu,”
Sikiliza Hapa:
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. ni kweli kabisa!!! diamond amesitahili kupewa bendera. bravo nape

    ReplyDelete
  2. Tunajipendekeza wakati mpira wetu uko ugokoni, WATANZANIA wangapi washapewa bendear kuwakilisha nchi?, hakuna, bali wapo WATANZANIA wengi ambao wanafanya vizuri nje ya nchi lakini hata bendera hawapewi, Mpira wetu utaishia ugokoni...

    ReplyDelete

Top Post Ad