AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA
Gigy Money
Akizungumza na gazeti hili juzi, Gigy alisema kwamba amekuwa na uhusiano wa kimapenzi na mastaa mbalimbali wakubwa Bongo akiwemo Mbongo Fleva, Ali Kiba na kudai kuwa, kama kuambukizwa virusi angeanza yeye na wengine wangefuata.
“Unajua watu wanashangaza sana. Kama mtu ana virusi vya Ukimwi hawezi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mtu anayempenda, ningependa watu waache unyanyapaa. Ninachojua mimi sina Ukimwi kwa kuwa nilipima kwa shinikizo la mpenzi wangu wa sasa (Moulad Alpha ‘Moj’) na watu niliotembea nao wanaendelea vizuri tu, wengine wachumba zao wananyonyesha,” alisema Gigy.
Video queen huyo alikwenda mbele zaidi kwa kusema kuwa, kuvaa nusu utupu ni kitu anachopenda kufanya toka ndani ya moyo wake hivyo hakuna mtu wa kumwambia kitu au kumkataza hata siku moja na wala siyo mgonjwa wa akili bali anafanya kitu kujifurahisha nafsi yake si ya mtu mwingine.
“Mimi nasikilizaga moyo wangu unasema nini, si mtu anasema nini juu yangu hivyo kama kuvaa nusu uchi wana hofu na mimi waondoe hilo kwa maana kama ni Ukimwi wengi wangeondoka siku nyingi kwenye ramani ya dunia hii maana hakuna niliyemuacha kwa mastaa unaowajua,” alisema Gigy kwa kujiamini.
Gigy ameshatoka kwenye magazeti mbalimbali akidaiwa kutembea na mastaa kama Hemed Suleiman ‘PHD’, Richard Martin Lusinde ‘Rich Mavoko’, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, Seif Shaban ‘Matonya’ na Omar Nyembo ‘Ommy Dimpoz’.
Mwingine aliyewahi kutajwa ni Mtangazaji Gardner G. Habash ‘Captain’ na Mshindi wa Big Brother Africa 2014, Idris Sultan.
Chanzo:GPL
Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.
Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA
Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.
NAFASI ZA AJIRA
JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA
GOODLUCK
Gigy wape ukweli hao mimi mwenyewe nimetembea na wanaume zaidi yako wewe na sina ukimwi mara ya mwisho kupima ilikuwa mwaka jana, ukimwi si rahisi kuambukizwa kama kipindupindu watu wakae wakijua hivyo ukimwi ni rahisi kuambukizwa kama ukifanya mapenzi kinyume na maumbile lakini kwa njia ya kawaida si rahisi
ReplyDelete