Hii ni zaidi ya Laana,Diamond na Ali Kiba Wakimbia Mwaliko wa Kuhudhuria Maulidi ya Kuzaliwa Mtume Muhammad(S.A.W),Shehe Mkuu Dar Atoa Kauli Hii..!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Ama kweli imeshangaza wengi! Kitendo cha nyota wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ na Ally Saleh Kiba  kushindwa kutokeza kwenye sherehe za kumbukumbu ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W), yaani Maulidi iliyofanyika wilayani Temeke jijini hapa ambapo walialikwa na Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum na kumuahidi kuwa wangefika.

Katika Maulidi hiyo ambayo ilifanyika Mtaa wa Liganga wilayani hapo na mwenyeji wa shughuli hiyo kuwa Shehe Alhad, ilihudhuriwa na waheshimiwa mbalimbali wakiwemo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd, Makamu wa Rais Mstaafu wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, Mufti wa Tanzania, Shehe Abubakar Zubeir na wengineo.

KAULI YA SHEHE MKUU JUKWANI

Wakati Maulidi hiyo ikiendelea, Shehe Alhad aliutangazia umati uliojaa kuwa, katika hafla hiyo aliwaalika wasanii mbalimbali na kuwataka watu kuwachukulia wasanii hao kama wenzao. Akiendelea kuweka mambo sawa, alisema mpaka muda huo msanii ambaye alishafika ni Ahmed Olotu ‘Mzee Chilo’ na pia akaongeza kuwa, msanii wa nyimbo za kughani, Mrisho Mpoto ‘Mjomba’ alikuwa njiani kufika eneo la tukio ingawa mpaka wageni waalikwa wanaondoka, Mpoto alikuwa hajafika.

Baadhi ya watu walifurika kwenye eneo hilo na kujua kuwa, Diamond na Kiba wangekuwepo, walishangaa kuona muda unakwenda bila wapendwa hao kuonekana licha ya kusubiriwa kwa hamu kubwa.

KAMA WANGEFIKA

Baadhi yao walisema kuwa, kama Diamond na Kiba wangejitokeza kwenye Maulidi hiyo, wanaamini Shehe Alhad angewaunganisha na kuwashikanisha mikono ya wengine wakiwa hawezi hata kuongea.

WAGENI WAALIKWA WAONDOKA

Baada ya Shehe Alhad kuwasindikiza wageni waalikwa, Wikienda lilimuweka chemba na kuanza kumuhoji kuhusiana na kutofika kwa Diamond na Kiba ambao ilisemekana aliwaalika. “Aaah! Ni kweli Diamond na Kiba niliwaalika na wote waliniahidi kufika lakini nashangaa mpaka muda huu hawajatokea, sijui ni kwa nini lakini hilo siwezi kulizungumzia zaidi isipokuwa hata mimi nashangaa,” alisema Alhad na kuomba aachwe aendelee na majukumu yaliyombana, ikiwemo

kuagana na wageni wengine. Wikienda liliwapigia simu Diamond na Kiba ili kutaka kujua kilichowasibu mpaka kushindwa kutokea kwenye mwaliko huo.

DIAMOND: “Ni kweli nilialikwa, lakini nilipata dharura ya kifamilia, niko Afrika Kusini.”

Kiba simu yake haikuwa hewani.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hawa wasanii wanaowatu wanaowashauri,bila shaka sio Waislamu.freemason nakadhalika.tusiwalaumu.

    ReplyDelete
  2. Ostadh ni kiongozi wa waislam almasi na ali ni waislam sasa wew e kama uelewi hayo ni matatizo yako @ Abdullah dulla

    ReplyDelete

Top Post Ad