Hiki ndicho kinamliza Aika wa Navy Kenzo

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA

Zikiwa zimeshapita siku kadhaa toka kundi la Navy Kenzo waweze kuipeleka mtaani Album yao ya 'AIM' amabayo ina jumla ya ngoma 11 wasanii hao wameonyeshwa kusikitishwa na kuvunjwa moyo na baadhi ya watu ambao wamekuwa wakizivujisha ngoma hizo

Watu waliowanyooshea vidole zaidi ni Bloggers ambao wamekuwa wakichukua nyimbo zao kwenye Album na kuziweka kwenye mitandao ya kijamii.

Akizungumza kwenye kipindi cha Bongo fleva Top 20 Aika alisema kitendo cha baadhi ya watu hususani bloggers kuchukua nyimbo hizo kwenye album na kuziweka mitandaoni kinakuwa kinawavunja moyo kwani kinasababisha biashara yao kupunguza kasi na kuharibu mauzo ya album hiyo mtaani.

Mbali na hilo Aika alisisitiza kuwa anatambua bloggers huenda wanajua wana wa'support' kwa ku-upload nyimbo hizo kwenye mitandao ya jamii ili kusaidia album kuuzika lakini huenda wengine hawajui kile wanachofanya kinawaharibia wao soko la album yao mtaani.
-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. lakini siku hizi watu hawanunui album wanasikiliza miziki mitandaoni soko la album limekufa kwa miaka mingi iliyopita hata wasanii wa kimarekani siku hizi hawauzi album kama zamani

    ReplyDelete

Top Post Ad