Katibu Mkuu Umoja wa Matifa Amwakikishia Rais Magufuli Ushirikiano ..!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


KATIBU Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Antonio Guterres amemhakikishia Rais John Magufuli kuwa UN itaimarisha ushirikiano wake na Tanzania katika kutekeleza majukumu mbalimbali, hususan tatizo la wakimbizi.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa, Guterres alisema hayo jana, alipokutana na Rais Magufuli kando ya Mkutano wa 28 wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika (AU), unaoendelea mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.

Guterres aliahidi kuwa UN itaongeza ushirikiano na Tanzania na kwamba itatia msisitizo zaidi katika kukuza wadau mbalimbali wa maendeleo ndani ya jumuiya ya kimataifa, kuchangia juhudi zinazofanywa na Tanzania katika kuwapa hifadhi wakimbizi wa nchi mbalimbali tangu mwaka 1971.

Kwa upande wake, Rais Magufuli alimpongeza Guterres kwa kuchaguliwa kwake hivi karibuni kushika wadhifa huo.

Alisema Tanzania itaendelea kushirikiana kwa karibu na Umoja wa Mataifa. Rais Magufuli pia alimweleza Katibu Mkuu huyo wa UN juhudi mbalimbali, zinazofanywa na Tanzania na Jumuiya ya Afrika Mashariki, kushughulikia mgogoro wa Burundi chini ya Mpatanishi wa mgogoro huo, Rais mstaafu Benjamin Mkapa na alimhakikishia kuwa juhudi hizo zinakwenda vizuri.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad