Gwajima asema atamshitaki Makonda kwa Mungu

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima ameendelea kuonyesha msimamo wake wa kumshtaki Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa Rais Magufuli huku akidai endapo ataona hakuna hatua inayochukuliwa atamshtaki kwa Mungu na majibu yatapatikana.

Askofu Gwajima aliyasema hayo Jumapili hii wakati akiongoza ibada ya Jumapili kanisani kwake Ubungo Maji. “Watu wananiuliza, nitamfungulia kesi. “Mimi nawaambia nitamwambia Rais Magufuli kama nilivyosema, kama hakuna kitu kitakachofanyika basi nitamwambia Mungu aliye juu na majibu yatapatikana,” alisema Askofu Gwajima.

Aidha Askofu huyo alisema yeye alipochokozwa haikuwa bahati mbaya ila alidai wanaomchokoza ni sawa na kufungulia koki ya maji yenye mgandamizo mkubwa au wamebusu transfoma ya umeme ambayo ni hatari kwa maisha ya binadamu kuisogelea kama huna utaalamu nayo kwa sababu husababisha kifo.

Hata hivyo Askofu huyo alitoa mstari uliopo kwenye biblia ambao ni Yeremia 22: 11 ambapo alisema kila jambo linatokea kwasababu maalum sio kwa bahati mbaya.
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Gwajima, kama unamzungumzia Mungu wa Israel, wa Ibrahim, na wa Yakobo, ukitaka ufanikishe mashitaka yako kwake, wagawie masikini mali ulizo nazo, kisha uzaliwe upya kama mtoto mdogo, usipofanya hivyo utakuwa unapiga porojo za manabii wa uongo ambao nyakati hizi wamejaa kila kona.

    ReplyDelete
  2. NI KWELI KABISA.NA AFE HAPO HAPO KWA HAKIKA HAWEZI GAWA MALI ALIZO PEWA NA MWENYEZI MUNGU KWA MASIKINI NA YATIMA..

    ReplyDelete
  3. kama mtumishi wa mungu kamwe huwezi lalamika mpaka sasa pasipo kusamehe kama tunavyofundishwa

    ReplyDelete
  4. Chapa kazi acha longolongo, waumejuaje kuwa hagawii maskikini mali zake,unataka awe anakupigia simu kila anapokuwa anasaidia masikini? au unataka nae awe masikini.....

    ReplyDelete

Top Post Ad