Waliokamatwa kwa Dawa za Kulevya Wafikia 349..!!!

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limetoa taarifa ya kukamatwa kwa jumla watuhumiwa 349 akiwemo 'video queen' Agnes Gerald maarufu kwa jina la 'Masogange', katika oparesheni ya kuwasaka watu wanaohusika na dawa za kulevya.

Akizungumza leo Jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro amesema kati ya watuhumiwa hao, wamo wauzaji, wasafirishaji na watumiaji wa dawa za kulevya, na kwamba wataanza kufikishwa mahakamani siku ya kesho, huku mmoja akipandishwa kizimbani leo.

Pia ametoa taarifa ya kijana mmoja anayedaiwa kusambaza taarifa za uongo, ambapo amesema kuwa jeshi hilo linamshikilia kijana huyo ambaye ni mwanafunzi mwenye umri wa miaka 23, anayedaiwa kutaja majina ya viongozi na kuwatuhumu kuwa wanahusika na dawa na dawa za kulevya.

Kuhusu askari 9 waliotuhumiwa kuhusika na dawa hizo, Kamanda Sirro amesema askari hao wamekabidhiwa kwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya kwa ajili ya kuchukuliwa hatua za kisheria.

Kamanda Sirro amesema hadi sasa jumla ya kete 612 pamoja na bangi vimekamatwa na kwamba kuna watu wengine 17 ambao bado jeshi hilo linawafuatilia na watakuwa mbaroni wakati wowote.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad