Hii ndio Sababu iliyofanya 'Mashoga' Kutotajwa Hadharani

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA



Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt Hamis Kigwangalla kwa mara ya kwanza ametoa sababu ya yeye kushindwa kuweka wazi orodha ya watu wanajihusisha na mapenzi ya jinsia moja (mashoga)

Amesema hakuaua kuyataja hadharani majina hayo kwa kuwa nikusikiliza ushauri aliopewa na jamii inayomzunguka.

“Mimi nashaurika, sikuweka majina hadharani kwa sababu nashaurika, listi ya watu ninayo na tunachukuwa hatua kimya kimya hili ni kosa la jinai na mtu anayekutwa na hatia anafungwa kifungo cha miaka 30 jela” Amesema Dkt. Kigwangalla
Dkt. Hamisi Kigwangalla amesema, hayo wakati akiwa kwenye maadhimisho ya siku ya Ustawi wa Jamii Duniani ambayo kitaifa imefanyika jijini Dar es Salaam, katika maadhimisho hayo Kigwangalla ameeleza kuwa kufanya mapenzi ya jinsia moja ni kosa kibaiolojia na hairuhusiwi mtu kuvutiwa na mtu wa jinsia yake.

Aidha, amesema katika sheria iliyotungwa mwaka 2012 ya kukazia adhabu ya mapenzi ya jinsia moja, kuna kipengele kinachotaka mtu achukuliwe hatua endapo ikithibitika amekaa mapozi yasiyoeleweka na ikabainika kuwa ni kwa lengo la mapenzi ya jinsia moja atafunguliwa mashtaka.

Mhe. Kigwangalla amewaonya wanajihusisha na mapenzi ya jinsia moja na kusisitiza kwamba serikali inawachukulia hatua kimya kimya.
----

Utamu wa audio book ya SIRI YA PADRE NA MKE WANGU hauna mfano, sikiliza Sehemu ya 1 bure, Sehemu ya 2 Tsh 2000 tu

Nusu ya mapato ni kwa ajili ya wagonjwa wasiojiweza, Lipia uburudike huku ukitoa sadaka Safi,ni www.makapedia.com au bofya kitabu hapo chini:



 

-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad