Mbunge Lijualikali: Niliteswa na kupigwa sana na askari Magereza

 AJIRA ZA UHAKIKA NJE NJE, BONYEZA HAPA


PETER Lijualikali, Mbunge wa Kilombero, (Chadema) amesema akiwa mfugwa kwa yake kwa siku 79 katika gereza la Ukonga jijini Dar es Salaam, aliteswa na kunyimwa haki zake, anaandika Pendo Omary.


Baada ya kutoka gereza la Ukonga amesema “kuishi gerezani unapaswa kuwa mvumilivu na mwenye busara. Kuna mateso ya kikatili ambayo ambayo wafugwa wanafanyiwa. Kuna wakati niliumwa maralia, daktari akashauri nipumzike. Lakini nilifanyishwa kazi ngumu na kuhatarisha afya yangu.”


“Askari Magereza saikolojia yao bado ipo kikoloni. Nimeshuhudia mtu anapigwa hadi anatambaa. Kuna harassment ambazo nilikuwa nafanyiwa. Nilipigwa sana.


“Gerazani kuna madaraja matatu, daraja la kwanza, la kati na la tatu. Kwa nafasi yangu ya ubunge nilipaswa kuwekwa daraja la kwanza. Ningekufa taifa lingepata hasara kubwa. Lingepoteza zaidi ya bilioni tano kurudia uchaguzi.


“Wakati haya yanafanywa kwa wafugwa wa kawaida, wezi wa meno ya tembo wakiwemo raia wa China wenyewe wanapewa huduma maalum ambazo ni nzuri, tena daraja la kwanza,” amesema Lijualikali.


Lijualikali amesema: “Uhusiano wangu na jeshi kama taasisi ulikuwa mbovu. Lakini uhusiano wangu na askari (mtu mmoja mmoja) haukuwa mbaya sana. Wengine walikuwa wananiambia walitumwa kunifanyia mateso na viongozi wao.”
----

Love Story ya NJIA PANDA,Ni Kali mnoo Jamani.

Kusikiliza au kusoma mwendelezo wake Tembelea www.makapedia.com kisha bofya palipoandikwa NJIA PANDA kila siku saa moja kamili jioni BURE au bofya HAPA

Pia Bofya HAPA kujiunga na what's app channel yetu,tukukumbushe kila siku.


-------------------

NAFASI ZA AJIRA 

JIUNGE NA AJIRA YAKO TELEGRAM GROUP HAPA

INTERNSHIP VACANCIES

GOVERNMENT VACANCIES

NGO'S VACANCIES 

GOODLUCK

Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Je wanasheria mnayasikia haya. Mtanzania haheshimiki. Tafadhali sana Tanzania kama nchi katiba na sheria za nchi zirudiwe tena na sasa. Ni kwa madlshi ya kumlinda Mtanzania mlipa kodi wa polisi na viongozi wote wa seriksli.

    ReplyDelete

Top Post Ad